Kagoma mimi kuishika simu yake

PierreLiquid

JF-Expert Member
Oct 16, 2019
596
2,279
Habari wakuu, natumaini mu wazima katiaka pilika za kimaisha. Leo mimi ndugu yenu, mdogo wenu naomba kujua maana ya ili linalonikumba.

Mimi ni kijana makamu ya 25Me nipo kwenye mahusiano na binti mmoja nimemzidi 3years na mahusiano yetu naweza kusema yana zaidi ya miaka miwili changamoto zinakuwepo ila mwisho wa siku tunarudiana, kiukwl kadiri muda unavyokwenda naona upendo wangu kwa huyu binti unaongezeka mno.

Tuachane na na hayo twende kwenye point yangu, huyu mwenzangu anatabia ya kutumia muda mwingi saba na simu yangu yani huwa anapekuwa sana simu yangu kipindi tukiwa wote kuanzia sms, picha,watsap, instragram, fb kote.

Ila kwa bahati nzuri kiukweli mimi nimekuwa sahivi sina mambo mengi kama apo awali hivyo huwa namuachia akague mpaka anachoka, naweza kusema anawivu sana nakumbuka kuna siku alikuta conservaton watsap yng na mwanamke fulani ni mteja wangu wa biashara sasa alituma sms akiwa na simu yng akafanya kuchati nae ili ajue kama kuna lolote jambo ila hakukuwa na lolote.

Kiukwel sijui kama ni wivu au haniamini. Juzi amekuja kwangu kama kawaida kachukua simu yangu, nikajiongeza nikasema acha leo na mimi nimpime, nikamwambia na wew nipatie simu yako leo sio kila siku unakagua yangu tuu.

Kiukweli Hakuwa tayar kufanya ivo na tulizungushana sana ndani mpaka ikafikia hatua mimi nikakasirika ila yeye akaniambia P mm siwez kukupa simu najua tutagombana uku tension yake ikiwa ni kufuta baadhi ya sms mimi nikawa nafocuse na yeye tuu.

Nikamwambia kulikoni ufute iko unachonificha ni bora unionyeshe haijalishi kitanikwazwa kiasi gani ila nafsi yangu itaridhia na ntakusamehe km kutakuwepo na sintofahamu ila kiukwel aliridhia kufuta kuliko kunionyesha.

Najikuta uaminifu kwa uyu mpendwa unapungua na nakua namashaka. Kwann alinificha na ni kitu gani iko ndio maswali ninayojiuliza mpaka sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom