Kagera: Ratiba ya kuaga miili ya waliofariki ajali ya ndege ya Precision Air, Waziri Mkuu anazungumza, leo 07-11-2022

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,971
12,291
Hivi ndivyo mambo yalivyo leo Novemba 7, 2022 kuhusu utaratibu wa kuaga miili 19 ya watu waliofariki katika ajali ya ndege ya Precision Air iliyotokea jana Novemba 6, 2022 Mkoani Kagera.




KAGERA: WAVUVI WALIOSAIDIA UOKOZI KUPEWA MAFUNZO MAALUM
Wavuvi ambao wapo jirani na Uwanja wa Ndege wa Mkoani Kagera wanatarajiwa kupewa mafunzo maalum ya uokozi kutokana na kutoa msaada wa uokozi katika ajali ya ndege hiyo kutua ziwani

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema β€œNaagiza Katibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia kitengo ambacho kinaratibu wajasiriamali kuwapa mafundisho na kuona namna wanaweza kuwasaidia na kuweka vizuri ushirika wao.”
 
Mbona hawa ndugu zetu huku barabarani na hizi ajali za mabus wanakufa mara kwa mara idadi ya kutisha kuanzia 20 - 30 mara kwa mara lakini hakuna mazishi ya hivi zaidi ya kulazwa chini na ndugu kutambua miili na kuizika huku na ndugu zao wenyewe.

Ndugu wapewe miili yao na serikali ighalamikie gharama za mazishi, fedha za makusanyiko kama haya watu wajazane na viongozi wasafiri tena kwa gharama za serikali.... Baadala yake hela zikanunue patrol boats mbili na kuajili divers permanently wawe shift kwenye hizo boats na boat captain all the time.
 
Hata ubalozi wa Marekani umetoa salamu za pole,ila kwenye ajali za Mabasi hua wapo kimya tu.
 
Hatar sn !!
 
Hata ubalozi wa Marekani umetoa salamu za pole,ila kwenye ajali za Mabasi hua wapo kimya tu.
Hapo sasa !!
So sad 😒

Kuna wakati huoni faida ya maisha, tunahangaika na maisha ili iweje wakati pumzi ikitolewa hapo unabaki mpweke kaburini πŸ™†πŸ˜’πŸ˜’πŸ˜’
Mimi huwa nawaza hivyo hivyo!! Hii dunia usiipapatikie saaana mtu ukajiona kama vile umefika !! Hapa ni mapito tu tena hakuna muda maalum tutaondoka tu , haijalishi wewe ni nani na unamiliki vitu gani!! One way ticket inatuhusu sote. !! Tusinyanyase na tusidhalilishe wengine ! Hapa sio Home. !!
 
Maisha ni kama fumbo tu,



Jiheshimu,
Waheshimu wenzako.
Mpende Mungu,
Tafuta riziki yako kwa njia ya halali wala usimdhulumu mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…