Baraza la Mawaziri la serikali ya Tanzania limepokea taarifa ya awali ya ajali ya ndege ya Precision Air iliyotokea Novemba 6, 2022

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,023
1,609
Baraza la Mawaziri la serikali ya Tanzania limepokea taarifa ya awali ya ajali ya ndege ya Precision Air iliyotokea Novemba 6, 2022, Bukoba mkoani Kagera na kugharimu maisha ya watu 19.

Kauli hiyo imetolewa hii leo Novemba 14, 2022, jijini Dodoma na Msemaji Mkuu wa serikali kufuatia maelekezo ya Baraza la Mawaziri lililoketi hii leo na Rais Samia Ikulu ya Chamwino.

"Leo kikao cha Baraza la Mawaziri kikiongozwa na Rais Samia kimekutana hapa Dodoma, na Baraza la Mawaziri limepokea taarifa ya awali ya ajali ya Ndege ya Precision Air na hatua zilizochukuliwa baada ya ajali," amesema Msigwa

Aidha Msemaji ameongeza kuwa "Baraza la Mawaziri limewaelekeza wataalam wa ndani kushirikiana na wataalam kutoka nje ya nchi katika kufanya uchunguzi na kupata chanzo cha ajali pamoja na kupata mapendekezo ya hatua zinazotakiwa kuchukuliwa mara baada ya ajali kutokea,".

Baraza la Mawaziri pia limeelekeza kwamba vitengo vyote vinavyohusika na kukabiliana na majanga nchini viimarishwe ili kuongeza uwezo zaidi wa kukabiliana na majanga yanapotokea.

Chanzo: EATV
 
Eneo ninalokaa tuna zaidi ya siku sita bila kuona tone la maji kwenye mabomba. Fikiria vyoo vya ndani bila maji hali inakuwaje. Kinachosikitisha zaidi ni viongozi wetu wako busy na siasa kama vile hili sio janga linalohitaji dharura. Kitakachofuata ni mlipuko wa magonjwa.

Nashauri baraza la mawaziri likae na lije na suruhisho, huo ndio uongozi badala ya kuzunguka mitaani na ma V8 yenu ndani ya viyoyozi mkisifiana.
 
Picha: Rais Samia aongoza kikao cha dharura cha Baraza la Mawaziri​

BAB20A58-1B4C-470F-92DA-6ECBE099A7E2.jpeg

15BA9F0B-D68B-435D-B755-6E13B17F0C35.jpeg

77A0E047-5B0B-4506-8E99-C8E011847774.jpeg
 
Eneo ninalokaa tuna zaidi ya siku sita bila kuona tone la maji kwenye mabomba. Fikiria vyoo vya ndani bila maji hali inakuwaje. Kinachosikitisha zaidi ni viongozi wetu wako busy na siasa kama vile hili sio janga linalohitaji dharura. Kitakachofuata ni mlipuko wa magonjwa.

Nashauri baraza la mawaziri likae na lije na suruhisho, huo ndio uongozi badala ya kuzunguka mitaani na ma v8 yenu ndani ya viyoyozi mkisifiana.
Watakwambia anaupiga mwingi, Kwa hiyo mi-5 tena 🙄
 
Dar es salaam ijiandae kwa kipindupindu. Maana Maji ya visima vingi vinapakana na vyoo vya watu kwa kuwa viongozi wao wanapendelewa kupata Maji kila siku hawawezi kuchukua hatua za haraka kuwaepusha wananchi na hii hali. Wananchi kesho twendeni tukaandamane hapo ikulu hadi kieleweke
 
Eneo ninalokaa tuna zaidi ya siku sita bila kuona tone la maji kwenye mabomba. Fikiria vyoo vya ndani bila maji hali inakuwaje. Kinachosikitisha zaidi ni viongozi wetu wako busy na siasa kama vile hili sio janga linalohitaji dharura. Kitakachofuata ni mlipuko wa magonjwa.

Nashauri baraza la mawaziri likae na lije na suruhisho, huo ndio uongozi badala ya kuzunguka mitaani na ma v8 yenu ndani ya viyoyozi mkisifiana.
Hameni nendeni mikoani huko mmejazana sana Dar mpaka maji hakuna.
 
Mimi ninakaa Mbezi Beach Africana DSM, Karibu na Art Galary Upande wa chini ya Bagamoyo Road Kama unatokea Tango Bovu. Leo hii Ni wiki ya 4 hakuna tone la maji kwenye mabomba. Upande wa juu wa Bagamoyo Road wao hawakatiwi maji (yanatoka kila siku). Wanasema ati mabomba Yao yameunganishwa na Bomba la Jeshini na Ikulu na Muhimbili Hospital.
 
Buda wao hawana shida ya maji, kwani wamekwambia wanapanga foleni ama wanaoga yale ya chumvi chumvi. Ni sawa na kulalamika shida ya foleni DSM wakati mhusika mkuu wa foleni kamanda anapita free na riders ikimfagilia traffic's na hata kupita upande wa kulia against traffic's flow akiwahi kazini

Sent from my LM-Q730 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom