Rais Samia: Kijana aliyeongoza Uokoaji atafutiwe nafasi Jeshi la uokozi

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,845
141,767
Ni agizo kutoka kwa Rais Samia,
Amiri Jeshi Mkuu, ameagiza Waziri wa Mambo ya Ndani Masauni kuanza mchakato wa ajira ya huyo kijana mara moja.

Kijana huyu ndiyo alizamia na kwenda kufungua mlango wa ndege na hatimaye abiria 24 wa Precision Air iliyozama kuokolewa.

Source: TBC

======

Waziri mkuu akiwa kwenye shughuli ya kuaga miili ya kuaga marehemu waliopata ajali kwenye ndege ya Precision, amesema Rais Samia ametoa agizo kijana aliyewanusuru watu waliokwama kwenye ndege hiyo atafutiwe nafasi kwenye Jeshi la uokozi.

Pia Serikali kugharamia mazishi ya wote waliofariki kwenye ajali hiyo.

=====

MAJALIWA JACKSON AMECHUKULIWA RASMI NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI



Kijana huyo maarufu kama "MaJa Munyama" ambaye alifanikiwa kufungua mlango wa Ndege ya Precision Air iliyopata ajali Ziwa Victoria ameondoka Bukoba kwa ajili ya kuanza mafunzo rasmi ya Uokoaji

Leo Novemba 7, 2022 Rais Samia aliagiza kijana huyo aingizwe Jeshi la Uokoaji ikiwa ni pongezi ya Ujasiri wa kuifikia Ndege na kuvunja mlango uliofanya watu 24 kuokolewa kwenye maji.
 
Rais Samia aagiza jeshi la mambo ya ndani ya nchi kumpatia nafasi ndani ya jeshi la uokoaji kijana majaliwa Alie fungua mlango wa ndege wakati wa zoezi la uokoaji Waziri Mkuu kassim majaliwa ameyasema hayo akihutubia huko kaitaba.
 
Yule kijana jasiri Aliyesaidia Kuokoa abiria ajali ya ndege amepewa kazi kwenye Jeshi la Zimamoto.

Serikali imeagiza taarifa zake zichukuliwe na angizwe Zimamoto mara moja.

Huu ni ushindi mkubwa kwa serikali, hii itatoa motisha kwa wananchi kuweza kusaidia kwenye majanga mbalimbali
Safiiii
 
Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza Majaliwa Jackson almaarufu Majamunyama ambaye ni mmoja wa vijana waliojitokeza kusaidia kuokoa watu wakati ndege ya Precision Air ilipozama kwenye maji Ziwa Victoria jana Novemba 6, 2022, apewe ajira katika Jeshi la Uokozi.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema “Nawapongeza wote mlioshiriki katika kufanya kazi ya uokozi, pia Rais Samia ameagiza kijana huyo ambaye alisaidia kufungua mlango na kuokoa watu waliokuwemo ndani ya ndege apelekwe Jeshini akapewe mafunzo zaidi na kuendelea kuonesha ujasiri kama aliouonesha.”
 
Back
Top Bottom