barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Mama huyu anaishi na wajukuu wanne na nyumba yake ni moja ya nyumba iliyobomoka kutokana na tetemeko la ardhi mwaka wa jana.
Mama huyu anasema,licha ya kuwa amesikia Serikali inasema michango na misaada iliyotolewa haitawajengea watu nyumba,yeye binafsi angeomba serikali imjengee nyumba hata ya vyumba viwili tu ili aweze kujibanza na wajukuu wake.
Maana hata misaada mingine ya kibinadamu hata yeye hakupata.Mama anaomba Serikali na hasa Rais wamsaidie kukarabati nyumba yake kwani hana uwezo wa kurudishia nyumba yake
Chanzo:Azam Two