Kagera Day: Mfuko wa elimu mkoa wa kagera | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kagera Day: Mfuko wa elimu mkoa wa kagera

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Mutensa, Jul 20, 2009.

 1. Mutensa

  Mutensa JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2009
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 426
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kwa mnaokumbuka,
  wana-kagera na wote wenye mapenzi mema walikusanyika kwa jitihada zote kwenda diamond jubilee (kama sisahau) kwa ajili ya kuchangia mfuko wa kusaidiia maendeleo ya elimu mkoa wa kagera. Ni pesa ndefu ilikusanywa siku hiyo na ahadi lukuki za kuchangia katika mfuko huo. Tangu tukio hilo limeisha, hatujasikia tena kilichoendelea. Je, kuna shule zimejengwa, vitabu kununuliwa, au nyumba za walimu kulala zimejengwa. Kuna mwenye chochote anayeweza kutwambia mpango huu umefikia wapi mpaka sasa.
  Je,
  pledge ziliendelea kukusanywa?
  Mpaka sasa zimepatikana sh ngapi na kiasi gani zimetumika na wapi?
  ahsanteni.
   
 2. Robweme

  Robweme Senior Member

  #2
  Jul 21, 2009
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 178
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hata mimi nilisikia kuhusu hiyo michango, ila baada ya hapo kumekuwa na kimya mda mrefu.
  Labda hiyo pesa iko inazungushwa, iliongezeke then ndo ianze kazi.
  Lakini kimya kingi kina mshindo,kaka.
   
 3. epigenetics

  epigenetics JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2009
  Joined: May 25, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
 4. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #4
  Jul 29, 2009
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  remember the 1980's "bijampola" saga?
   
 5. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #5
  Jul 29, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Ni hii habari ya 'mbegu' kule DECI inaongeza wasiwasi.

  Halafu wachangiaji wengine walikumbwa na sekeseke la vita dhidi ya ufisadi, sijui kama waliwasilisha ahadi zao.
   
 6. Mutensa

  Mutensa JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2009
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 426
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kumekucha, watanzania wanapoteza mamilioni hivi hivi kweli??
   
 7. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #7
  Aug 5, 2009
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,556
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Web ya kagera ni www.kagera.go.tz

  lakinikule kagera kuna gazeti moja linaitwa Malengo Yetu linaendeshwa na waandishi wa habari wa huko,limekuwa likiandika sana kuhusu mfuko huo na jinsi fedjha hizo zilivyotafunwa lakini baadaye kiongozi wa mfuko huo aliweza kufafanua masuala kadhaa kuhusu mfuko huo anaiwa mwijage.

  kwa kuwa gazeti halimo kwenye web nafanya kila njia kupata angalu soft copy ya maelezo ya kiongozi huyo ili niweke hapa,
   
 8. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #8
  Aug 5, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Mhh mfuko wenyewe kwenye hiyo tovuti mbona hauelezi ni kiasi gani hasa kilichangwa lakini inaeleza matumizi tu?
  Haya basi ebu wakulu wainuke na kusema! Usije kuwa ufisadi mwingine
   
 9. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #9
  Aug 5, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Si kuna viongozi wahusika?tena ndo wangetakiwa watoe taarifa muhimu kama hiyo yaani kiasi fulani kimepatikana na wachangaji wake..

  On a serious note mkuu, ile ishu hujaielezea tena,still pending? Thanks
   
 10. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #10
  Aug 5, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  BELINDA,
  Nimekusoma mama.
  Busara kama za Bi Clinton.
   
 11. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #11
  Aug 7, 2009
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,556
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Kagera day,sasa Kagera yetu kichocheo cha maendeo ya Elimu mkoani Kagera.
  .Wanaodhani ulikuwa mradi wa wachache wanawaonea waanzilishi !

  Na Mwijage Charles
  Naandika makala haya baada ya kusoma makala ya Mwandishi Phinias Bashaya iliyochapishwa katika gazeti moja la kila wiki(siyo Malengo Yetu) ikiwa na kichwa kisemacho Wabunge Mkoa wa Kagera Mko wapi ? ambayo kimsingi iligusia fedha zilizopatikana katika harambee iliyoitwa Kagera Day .
  Katika makala hiyo kuhusu fedha za Kagera day mwandishi alijaribu kubainisha kasoro kadhaa zilizojitokeza baada ya harambee hiyo hasa kufutia tetesi kuwa fedha hizo zilikuwa zimetafunwa na wajanja madai ambayo kimsingi ni upotoshaji na kinyume na yaliyokuwa malengo ya Kagera Day.
  Ni ukweli ulio wazi kuwa wabunge wa Kanda ya Ziwa acha Kagera hawana agenda ya pamoja,Hili ni tatizo la siku nyingi na njia mojawapo ya kuliondoa ni kuwasema kama ulivyoanza. Hilo sintalisema zaidi, leo inatosha.
  Mimi binafsi ni mkereketwa wa maendeleo ya Kagera utamaduni nilioujenga kwa zaidi ya miaka 30 iliyopita,Mwaka 1977 nikiwa kidato cha kwanza Nyakato sekondari niliingia katika mashindano ya kubuni jina la timu ya mpira ya mkoa wa Ziwa Magharibi.
  Rwelu Eagles ni pendekezo langu na ungesoma maelezo ya jina hilo ungetambua kweli kuwa mtunzi ana mapenzi ya ziada na mkoa wake. Historia ni ndefu
  lakini March 2007 mimi nilikuwa miongoni mwa watu watano walioanzisha wazo la Kagera day.lilikuwepo wazo la kualika Kakau Band ije Dar mwezi Mei 2007 na kutoa burudani. Katika moja ya vikao vya maandalizi tukapata mwanga kuwa badala ya kuleta kikundi watu wakacheza, kunywa na kulewa tubuni jambo la maana.
  Likaibuka wazo la kuendesha harambee sambamba na burudani ili rasilimali zitakazopatikana zisaidie maendeleo ya Kagera. Vikao vilivyofuatia ndipo elimu ikachaguliwa kwani ilikuwa ndiyo matakwa ya wakati. Najaribu kueleza haya kusudi watanzania wote na wana Kagera ili wanielewe ili hatimaye waniunge mkoni au wanipe hukumu inayonistahili.
  Kama ilivyosikika na

  kutangazwa Kagera day 2007 tulikusanya rasilimali zinazokaribia shillingi 1.5 billioni. Hii ni pesa taslimu, vifaa na ahadi.
  Sehemu kubwa ya makusanyo haya ni ahadi ya Professa Anna ya kujenga sekondari bora ya Wasichana mfano wa Babro ya Kwembe Dar.
  Mchakato unaendelea na mungu atatujalia ujenzi utaanza na kukamilika kama dhamira ya mhasisi ilivyo. Kumbuka huu ni mradi mkubwa unaohusisha wahisani na thamani yake usishangae ikawa kubwa kuliko fedha zilizotamkwa hivyo taratibu zote lazima zifuatwe ikiwemo kupata hati ya kumiliki ardhi.
  Sehemu ya pili ni vifaa halisia kama sementi, Kompyuta, mabati,kalamu na mtambo wa internet vyote hivyo viliwasilishwa mkoani na kugawiwa sawia. Kuhusu vifaa hivi naandaa ripoti ambayo inawahusisha wanufaika ambayo nitaisambaza wa kwa wadau wote. Iwapo mtu yyetote atatambua nia mbaya au ubadhirifu wowote naomba anibonyeze.

  Katika kundi hilo kama mwandishi alivyosema kuna ahadi ambazo bado hazijakusanywa. Napenda nidokeze kuwa hakuna kazi ngumu kama kukusanya ahadi. Ingawa waswahili walisema ahadi ni deni lakini si deni kama la kumkopesha mtu fedha au ng’ombe wa mahari. Lakini jambo moja la kutia moyo ni kuwa walioahidi wakikumbushwa wanaitikia ingawa si kwa kasi ambayo sisi wahitaji tungependa.
  Shughuli hii ilifanyika

  Nove 2007, mwezi January 2009 kuna mhisani mmoja amelipa shillingi 50 millioni.
  Tuliahidiwa kwa niaba ya wahitaji sisi kama kamati wajibu wetu ni kukumbusha na ukumbuke kuwa sisi Watanzania na hasa wana Kagera harambee ni utamaduni mpya na hasa inapohusu maendeleo ya jamii.
  Walioahidi walituahidi sisi kwa niaba ya kamati na naomba wananchi watuvulie tutawafuatilia.
  Hadithi ya wawindaji mia sungura mmoja. Makusanyo ya Kagera Day ni makubwa kwa namna yoyote ile lakini mahitaji ya elimu Kagera ni makubwa sana.
  Ili elimu Kagera iweze kuwa sawa unahitaji kuwekeza billioni 45 katika kujenga miundo mbinu ya kielimu. Tulikuwa na nia ya kupambana na lengo hili kwa kipindi cha miaka 6 mpaka 7 lakini hali halisi sivyo ilivyo.
  Katika kuhangaika tukabuni mpango wa Nguvu ya pamoja. Hii lengo lake ni kupandikiza utamaduni wa harambee katika jamii lakini ni pia ni kuondoa mkorogano wa Dar Es laamu walikusanya billioni, Arusha millioni 400, Chicago $ 350000 na sisi walengwa hatujapata kitu.
  Tunalenga kupunguza maneno na malalamiko ya ziko wapo fedha zetu tulizochangiwa.
  Pia tunalenga kupata suluhisho la kugawana hicho kidogo kinachopatina. Tunataka wananchi wenyewe katika mradi wao wawaalike wale wanaodhani wanaweza kuwasaidia, wapokee michango na ahadi na watekeleze mradi.
  Kagera day au Kagera Yetu secretariati ibaki na kazi ya kusaidia mbinu na mikakati ya kuendesha shughuli hizo ikiwemo uhamasishaji. Pia Kagera Yetu kwa kutumia rasilimali watu tulizonazo ijikite katika miradi mikubwa.
  Mwaka jana tumejaribu njia hii, Ibuga Muleba walikusanya 4.5 na kusogeza boma la vyumba vinne vya madarasa, Kagoma Muleba tuliahidiwa 8.4 mill, Ruzinga waliahidiwa 8, Kamachumu 15 mill na Itoju Moyo mtakatifu wa Yesu shughuli ilikuwa ni uhamasishaji. Tumeanza na imewezekana.
  Wananchi watambue kuwa njia hiyo hapo juu itatatua mambo mengi likiwemo la kujenga maabara ziszokuwa na vifaa. Mkoa wa Kagera asilimia 8 tu ya sekondari zake ndiyo yenye angalau maabara.
  Niko tayari kutofautiana na Mwandishi wa makala hiyo katika hili! Sekondari ikiwa na Jengo la maabara ni rahisi kwa wananchi, mashirika na serikali kuchangia vifaa.
  Mimi nakumbuka nimewahi kusaidia upatikanaji wa vifaa vya maabara kwa sekondari ya Rutabo vyenye thamani ya millioni 10.
  Ninapozungumza sasa kuna mzigo wa vifaa vya maabara unatolewa forodha Dar na atakayenufaika sharti awe na maabara. Ndugu wa Kagera tunaihangaikia Kagera yetu lakini mambo si rahisi kama watu wanavyofikiri. Kumbuka majukumu yote haya ni kazi ya kujitolea tunayo majukumu ya msingi ya kutafuta mkate wa watoto na wategemezi wengine. ‘Bojo kwakwo entasiima ekalya omutima gwemanzi’!
  Maabara zilizojengwa zitawekwa vifaa na kama nilivyoonyesha hapo juu safari ni ndefu. Sekondari ya Makyurugusi- Chato iliyofadhiriwa maabara chini ya Kagera Day sasa hivi vyumba viwili vinatumika kama madarasa. Ni rahisi chumba cha Maabara kutumika kama darasa na kinyume chake si sawa.
  Lengo la Kagera day ambayo inabadilika na kuwa Kagera Yetu ni kuchochea chachu ya wana Kagera popote walipo kushiriki na kushirikishwa katika maendeleo ya mkoa wetu. Sisi tulianzisha wazo hilo tunaomba mtukosoe kwa nia ya kujenga na kutupa moyo.
  Timu ya Kagera Yetu ni watu mahiri wenye upendo na nchi yao lakini zaidi walioandaliwa na jamii hivyo wanawajibu wa kurudisha kwa jamii.
  Hata hivyo kumejitokeza changamoto kadhaa mfano waanzilishi wa Kagera day walikuwa na matumaini makubwa, kuirejesha Kagera katika nafasi yake kimaendeleo. Lakini na walengwa nao walikuwa na matumaini makubwa, kusubiri mamilioni wao waje kutumia.
  Aidha Kamati imwekuwa na mawasiliano duni na wadau wake suala linalofanyiwa kazi ikiwemo kufufua tovuti yake.
  Pia uchache wa kikosi cha utendaji nao ni changamoto kwani lengo ni kuhudumia Kagera nzima lakini timu ina watu wachache wanaoelewa lengo na madhumunu na walioko tayari kufanyakazi hii.
  Lakini yote hayo ni masuala ya muda si ndipo tumeanza, matumaini mkubwa!
  Mtu yeyote anayedhani kazi hiyo ni rahisi nampa fursa ya kufanya haya kwa mfano (Free offer) Naoba kila mtu asome ‘model’ hiyo ya Nguvu ya pamoja na aiuze kwa tarafa na kata alikozaliwa.
  Iwapo watakuwa tayari mtu anipe taarifa ya siku 60 nitakuwa mshereheshaji na uwe na imani vyumba vinne vya madarasa vikitushinda tutabakiza sakafu tu.
  Mimi naamini kwa ushirikiano tunaweza kupiga hatua kubwa kimaeneleo kila mmoja atimize wajibu wake.

  Mwandishi wa makala haya ni Katibu wa Kagera Yetu iliyobadilishwa jina kutoka Kagera Day anaishi Jijini Dar Es salaam na anapatikana kupitia
  Email:
  cmwijage@chevron.com
  Chanzo:Gazeti Malengo Yetu la aprikl 2009 ,Linachapishwa mkoani kagera halipo kwenye mtandao
   
Loading...