Kagasheki: Msigwa analipwa na mafisadi kuwatetea

Kagasheki: Msigwa analipwa na mafisadi kuwatetea

Status
Not open for further replies.

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2013
Posts
18,949
Reaction score
4,645
Vyombo vya habari leo likiwemo gazeti la Uhuru vimeripoti kuwa mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa analipwa na mafisadi ili awatetee kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo bungeni.

Hayo yalisemwa na waziri wa Mali Asili na Utalii, Balozi Kagasheki kuwa miongoni mwa mafisadi ambao anawatetea ni pamoja na wale wanaofanya hujuma kwenye hifadhi za wanyama pori.

Wito wangu kwa Msigwa: Ni vema akafanya kazi ya kutetea watu waliomchagua siyo mafisadi.
 
"gazeti la uhuru"!!!!
Msigwa si ndio huyu ambaye kinana mla tembo wetu anapelekana naye mahakani kila siku? hao anaowatetea ni wakina nani? kajipange mkuu
 
Kawaida ya wapiga kelele wengi bungeni ni kutaka wasikike na mafisadi.
 
Tuambie kwamba gazeti limeandika kwamba Msigwa alifanya nini katika kuwatetea mafisadi, vinginevyo habari hizi zitakuwa zimekaa kipropaganda zaidi na hasa zinapoandikwa na upande wa Kinana.
 
nakumbuka maneno ya samweli sitta kuwa msigwa siyo mchungaji bali ni..........lakini wazanzibar walisema msigwa ni mchungaji wa ...........kazi kweli ndiyo matatizo ya wabunge ambao hawana adabu.
 
Kumbe zile kelele alizokuwa anapiga mara kumtuhumu kinana ilikuwa ni danganya toto kuwahadaa watu yeye ni mhusika wa uharifu.
 
Hahahahahaaa..... ccm wameanza kukimbia vivuli vyao wenyewe..

Hizi tuhuma za Msigwa kuwatetea Mafisadi zinaweza kuwa na ukweli ndani yake, Msigwa anavyopenda pesa, utafikiri Mchagga.
 
Kawaida ya wapiga kelele wengi bungeni ni kutaka wasikike na mafisadi.

ni kweli mkuu msigwa hana jipya zaidi ya kupiga kelele na kudandia kutuhumu watu kumbe anataka mafisadi wamuone ili akachukue chake.
 
UHURU Gazeti la chama cha Mapinduzi kama lilivyo Gazeti la Tanzania Daima nalo mlengo wake unaeleweka hivyo habari hiyo kwa mimi binfsi siipi uzito mkubwa kama Gazeti lenyewe linavyotaka kutuaminisha.
 
Kumbe zile kelele alizokuwa anapiga mara kumtuhumu kinana ilikuwa ni danganya toto kuwahadaa watu yeye ni mhusika wa uharifu.

Bila kumung'unya maneno Msigwa alitamka hadharani kuwa Kinana ni jangili mla tembo na hadi leo Kinana ameshindwa kwenda mahakamani, hao uhuru watamke Msigwa analipwa na fisadi nani, au wanataka kutuambia Kinana anamlipa Msigwa... too cheap propaganda...
 
Anawateteaje mafisadi? Na hao mafisadi ni kina nani?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom