Peter Msigwa asema hali ni mbaya katika Hifadhi ya Ngorongoro na jitihada za haraka kuinusuru zinahitajika

PendoLyimo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
878
955
MCHUNGAJI MSIGWA AFUNGUKA SAKATA LA NGORONGORO:- WALIPWE FIDIA WAHAMISHWE, WANA HAKI ZAO

Mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA ambaye pia ni Mwenyekiti wa kanda ya Nyasa wa chama hicho, aliyewahi pia kuwa mbunge wa Iringa mjini na waziri kivuli wa Wizara ya Maliasili na utalii Mchungaji Peter Msigwa amesema hali ni mbaya katika hifadhi ya Ngorongoro na jitihada za haraka kuinusuru hifadhi hiyo zinahitajika huku akiilaumu Serikali ya chama cha mapinduzi(CCM) kwa kutaka kuiuwa hifadhi hiyo.

Mchungaji Msigwa ameishangaa Serikali kwa kushindwa kufanya maamuzi sahihi kwa wakati kuinusuru hifadhi hiyo licha ya kuwa na ongezeko kubwa la watu na mifugo linalohatarisha ustawi wa watu, wanyama na uhifadhi wa eneo la Ngorongoro kwa kuogopa kupoteza kura za uchaguzi bila kujali maslahi mapana ya taifa nay a eneo husika yanayotokana na shughuli mbalimbali ikiwemo utalii.

“Serikali ya chama cha Mapinduzi inatukosea sana; kama haiwezi kutunza mali ambazo tumewapa, wanatukosea sana, hizi mali, Tanapa, Serengeti, Ngorongoro, Mkomazi, Ruaha, kila kitu kitulo, hii sio mali ya CCM ni mali ya Taifa kwahiyo CCM imepewa dhamana ya kutunza, wanapokuwa wazembe kiasi hiki, watu mpaka wanajenga mle ndani, mle ndani wanafuga Ng’ombe wanaozidi zaidi maanake wanatukosea sisi na ndio maana tunataka tuwatoe Madarakani wanashindwa kutunza mali za umma ambazo wamepewa dhamana wazitunze”. Alisema Msigwa.

Ameongeza kuwa hali ya watu wa Ngorongoro ni mbaya na maeishauri serikali kutoa fidia itakayowashawishi wakazi hao kuhama kwenda sehemu bora zaidi watakazopatiwa huduma na mahitaji yanayoendana na changamoto za sasa huku akiwaasa wasomi wa kabila la Kimaasai ambao wanapaza sauti kutokea Dar es Salaam kushinikiza wananchi wanyonge wa Ngorongoro wasibadilishiwe maiosha yao kwa kisingizio cha sheria ambayo kimsingi sio msaafu wala biblia na imetokana na matakwa ya kikoloni, kiasi cha kuwazuia wakazi wa eneo hilo kushindwa kujenga nyumba za kisasa miundombinu bora ya huduma za kijamii nk, huku akiwashangaa wabunge waliopita na wa sasa wa eno hilo kuwa mstari wa mbele katika uvunjifu wa sheria wanaoyoitetea.

Huu ndio ukweli.

Watu na mifugo ya binadamu wanazidi kuongezeka kwa kasi na kuharibu ecosystem ya Ngorongoro.

Tanzania kuna Mapori mengi tu ambayo Watu wanaweza kuhamishiwa huko lakini huwezi kuhamisha Nature ya Ngorongoro kuipeleka sehemu nyingine.

Wanasiasa wanalifumbia macho hili swala mwisho wa siku hifadhi itakosa viumbe wa asili.

Kama lengo ni kupata utalii wa watu na wanyama waishio eneo moja basi na kuwe na idadi maalum ya hao watu na mifugo yao, idadi ambayo haita athiri Hifadhi hiyo.

La sivyo hifadhi itakufa muda sio mrefu.
 
Shida ya watanzania kama ilivyo wanasiasa wengi Wana "subsistence thinking" wanaangalia hapa tu, leo, hatujui kwamba watakuwepo watanzania kama sisi in the next 100 years, ambapo most of us if not all hatutakuwepo.

Na kibaya zaidi uwezo wetu waku analyze mambo ni kama urefu wa pua. Kwa waliopata angalau D ya hesabu na kuendelea, kama ulipata "F" achana na hili swali, in 1960s wamasai walikuwa elfu 8 Leo 2022 wako estimated kuwa laki na nusu na mifugo laki 2, mathematically compute na fanya projection ya miaka 30 ijayo watakuwa wangapi na mifugo mingapi, thus you can be able think objectively and unbiased uharibifu wa hiyo mbuga utakavyokuwa.

Shida ya mtu mweusi unlike hao wazungu, ni ubinafsi ndio maana tunapata gas "tunauza" kwa kwa mikataba ya kipumbafu, tuna bwawa la Nyerere unasikia kuna wanasiasa wana team up kuhujumu Yani ni kama tuna laana vile, only an average IQ itaelewa bila hatua kuchukuwa Leo na Sasa hiyo mbuga haitakuwa mbuga in the next 30 years, and it only takes a "D" in mathematics to understand that.
 
Sensa ianzie huko, na itungwe sheria kila mtu azae watoto atakao watunzia nje ya hifadhi. Vijana kuanzia miaka 25 wasiishi ndani ya hifadhi. Ndani ya miaka 10 tutakuwa tumeokoa hifadhi.
 
Huu ndio ukweli.
Watu na mifugo ya binadamu wanazidi kuongezeka kwa kasi na kuharibu ecosystem ya Ngorongoro.

Tanzania kuna Mapori mengi tu ambayo Watu wanaweza kuhamishiwa huko lakini huwezi kuhamisha Nature ya Ngorongoro kuipeleka sehemu nyingine.

Wanasiasa wanalifumbia macho hili swala mwisho wa siku hifadhi itakosa viumbe wa asili.

Kama lengo ni kupata utalii wa watu na wanyama waishio eneo moja basi na kuwe na idadi maalum ya hao watu na mifugo yao, idadi ambayo haita athiri Hifadhi hiyo.

La sivyo hifadhi itakufa muda sio mrefu.
Hakika.
Heko mwake mchungaji
 
Shida ya watanzania kama ilivyo wanasiasa wengi Wana "subsistence thinking" wanaangalia hapa tu, leo, hatujui kwamba watakuwepo watanzania kama sisi in the next 100 years, ambapo most of us if not all hatutakuwepo.

Na kibaya zaidi uwezo wetu waku analyze mambo ni kama urefu wa pua. Kwa waliopata angalau D ya hesabu na kuendelea, kama ulipata "F" achana na hili swali, in 1960s wamasai walikuwa elfu 8 Leo 2022 wako estimated kuwa laki na nusu na mifugo laki 2, mathematically compute na fanya projection ya miaka 30 ijayo watakuwa wangapi na mifugo mingapi, thus you can be able think objectively and unbiased uharibifu wa hiyo mbuga utakavyokuwa.

Shida ya mtu mweusi unlike hao wazungu, ni ubinafsi ndio maana tunapata gas "tunauza" kwa kwa mikataba ya kipumbafu, tuna bwawa la Nyerere unasikia kuna wanasiasa wana team up kuhujumu Yani ni kama tuna laana vile, only an average IQ itaelewa bila hatua kuchukuwa Leo na Sasa hiyo mbuga haitakuwa mbuga in the next 30 years, and it only takes a "D" in mathematics to understand that.
Brilliant argument
 
Sensa ianzie huko,na itungwe sheria kila mtu azae watoto atakao watunzia nje ya hifadhi.Vijana kuanzia miaka 25 wasiishi ndani ya hifadhi.Ndani ya miaka 10 tutakuwa tumeokoa hifadhi.
Mfumo huu tuliuishi miaka ya 199x huko fort ikoma Serengeti, mtu mwenye familia asingeweza kuishi na kijana wake mkubwa eneo lile, leo maasai kila mtu ni kelele tu m ooh wanaonewa, oooh ndiyo kwao nani kasema Tanzania ni ngorongoro tu!.

Kuna wamasai wamehamia Handeni huko mbona hawajafukuzwa na maisha yanaendelea, hawa wana bahati taarifa zipo karibu sana, imean teckinolojia inawabeba.
 
Huu ndio ukweli.
Watu na mifugo ya binadamu wanazidi kuongezeka kwa kasi na kuharibu ecosystem ya Ngorongoro.

Tanzania kuna Mapori mengi tu ambayo Watu wanaweza kuhamishiwa huko lakini huwezi kuhamisha Nature ya Ngorongoro kuipeleka sehemu nyingine.

Wanasiasa wanalifumbia macho hili swala mwisho wa siku hifadhi itakosa viumbe wa asili.

Kama lengo ni kupata utalii wa watu na wanyama waishio eneo moja basi na kuwe na idadi maalum ya hao watu na mifugo yao, idadi ambayo haita athiri Hifadhi hiyo.

La sivyo hifadhi itakufa muda sio mrefu.

Msigwa kaelezea vizuri bila kuumauma au kupaka mafuta maneno, kikubwa nilichogundua ni unafiki wa wanasiasa wetu kulinda matumbo yao wasije wakakosa kura kwenye chaguzi zijazo, tatizo linafanana na ugumu wa uvamizi wa machinga Tanzania mzima huku wakiwa hawana ubunifu mbadala wa re allocation yao
 
Maoni ya mtu yeyote hayaondoi maslahi ya Wamaasai katika hifadhi. Walioanzisha walikuwa wanajua binadamu huzaliana.
Acheni chuki na dharau.
Sisi hatusikilizi maoni ya vilaza kama ninyi mliolipwa hela za NCAA.
Sisi tunaangalia maslahi yetu.
Kama hujafunzwa kutanguliza maslahi yako, kosa sio letu. Kosa ni walezi wako.
Sisi tuna pumzi kwenye kudai maslahi yetu.
Hatutishwi na yeyote.
Sisi tupo kwenye mjadala na Serikali katika ngazi ya Waziri Mkuu.
Sio vilaza kama wewe mleta mada, Msigwa, Balile au Kitenge.
Wote hao ni wasaka tonge.
 
Shida ya watanzania kama ilivyo wanasiasa wengi Wana "subsistence thinking" wanaangalia hapa tu, leo, hatujui kwamba watakuwepo watanzania kama sisi in the next 100 years, ambapo most of us if not all hatutakuwepo.

Na kibaya zaidi uwezo wetu waku analyze mambo ni kama urefu wa pua. Kwa waliopata angalau D ya hesabu na kuendelea, kama ulipata "F" achana na hili swali, in 1960s wamasai walikuwa elfu 8 Leo 2022 wako estimated kuwa laki na nusu na mifugo laki 2, mathematically compute na fanya projection ya miaka 30 ijayo watakuwa wangapi na mifugo mingapi, thus you can be able think objectively and unbiased uharibifu wa hiyo mbuga utakavyokuwa.

Shida ya mtu mweusi unlike hao wazungu, ni ubinafsi ndio maana tunapata gas "tunauza" kwa kwa mikataba ya kipumbafu, tuna bwawa la Nyerere unasikia kuna wanasiasa wana team up kuhujumu Yani ni kama tuna laana vile, only an average IQ itaelewa bila hatua kuchukuwa Leo na Sasa hiyo mbuga haitakuwa mbuga in the next 30 years, and it only takes a "D" in mathematics to understand that.
Kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake..
Bora hifadhi ipotezwe na wamasai kuliko kuiachia ccm ifaidi peke yake.
Dhahabu, Almasi, Serengeti, Mikumi, Serous, maziwa na bahari wameshindwa kuzitumia kwa miaka
60 hiyo ngorongoro ndio itaondoa umaskini leo?
Huo upendo dhidi ya maliasili za taifa umetoka wapi?
Kutetea wamasi watolewe ni kutete uovu wa ccm there is no benefit tutapata kwa kuwatoa wa masai
kama taifa zaidi ya ccm kuendelea kuneemeka na ujinga wa watanzania.
 
Kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake..
Bora hifadhi ipotezwe na wamasai kuliko kuiachia ccm ifaidi peke yake.
Dhahabu, Almasi, Serengeti, Mikumi, Serous, maziwa na bahari wameshindwa kuzitumiakwa miaka
60 hiyo ngorongoro ndio itaondoa umaskini leo?
Huo upendo dhidi ya maliasili za taifa umetoka wapi?
"Itaondoa umasikini Leo" ndio subsistence thinking" nayo ongelea, hauna ndugu, jirani, rafiki amezaa mtoto, ana mimba,? Etc, just know hii nchi itakuwepo after we are long gone, CCM haitadumu milele, Tanzania na watanzania watakuwepo mpaka mwisho wa Dunia hii, hatuwezi kuwa watu tuna akili na mawazo ya kijinga hivi tutegemee maisha yetu yatabadilika, or you think Tanzania inaisha siku ukifa? Sijui waafrika tumewekewa blanket gani kichwani!!?
 
Hahaha!!! who told youTanzania itakuwepo milele?
Ni kukumbushe tu miaka sitini iliyopita Mmasai na Msukuma hawakuwai kufikiri kama watakuwa sehemu moja
na kuishi pamoja kama brother au watu wanaotoka sehemu moja.
Be reaalistic thinking and be in the present moment.
Wamasai kuwepo pale na vizazi vyao huo ndio urithi tosha.
 
Kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake..
Bora hifadhi ipotezwe na wamasai kuliko kuiachia ccm ifaidi peke yake.
Dhahabu, Almasi, Serengeti, Mikumi, Serous, maziwa na bahari wameshindwa kuzitumia kwa miaka
60 hiyo ngorongoro ndio itaondoa umaskini leo?
Huo upendo dhidi ya maliasili za taifa umetoka wapi?
Kutetea wamasi watolewe ni uovu wa ccm there is no benefit tutapata kwa kuwatoa wa masai
kama taifa zaidi ya ccm kuendelea kuneemeka na ujinga wa watanzania.
Ndio nashangaa na mimi. Nchi ina rasilimali lukuki zisizo athiri utu lkn wasakatonge wamekomalia Wamaasai watolewe NCA. Kama sio hujuma ni nini?
Kuna mbuga za Wanyama kibao lkn wasakatonge wamekomalia NCA tu.
Kwanini promotion ya mbuga kama Ruaha, Selous, Kitulo, Katavi haufanyiki?
Msigwa badala ya kukomaa Ruaha iwasaidie wananchi wa Iringa, yeye amekomaa na NCA kisa katupiwa Fupa.
 
Na kuna watu wanashangilia hawa wanasiasa huwa wana agenda zao ukiwa mfuasi hutumii
akili utaishia kuwatajirisha bila kujua ukizani unatetea jambo la maana.
 
Wanasiasa wa nchi hii wamezidi kwa kusaka tonge aisee. Na wanawatumia waandishi vilaza na wasakotonge kama Kitenge.
Kama kitenge sio kilaza alete vyeti vyake vya taaluma hapa kuanzia form four hadi transcript ya chuo kikuu.
 
Back
Top Bottom