MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 33,569
- 53,583
Wakuu Mwadilifu na mseveni muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar umejaa usanii wa hali ya juu nitakutajieni sababu mbili kuu.
1.Muungano ambao mtanganyika akienda Zanzibar hana tofauti na mgeni toka Kenya au Sudan.
a, Mtanganyika hana haki ya kuchaguliwa au kuchagua viongozi akikanyaga ardhi ya Zanzibar.
b. Mtanganyika hana haki ya kumiliki ardhi ya Zanzibar .
c. Mtanganyika lazima aombe kibali cha ukaazi Zanzibar
d. Mtanganyika hawezi kuajiriwa na SMZ
e. Mtanganyika si chochote si lolote akikanyaka ardhi ya Zanzibar
f. Mzanzibar ana uraia wa nchi mbili,kwanza ana uraia wa Zanzibar pili ana uraia wa Tanzania.
g. Mtanganyika anawajibika kubeba gharama zote za muungano,ulinzi na usalama wazanzibar hawachangii chochote hata hili bunge la katiba Zanzibar haijatoa ndururu.
h. Makusanyo ya kodi upande wa Zanzibar yanabaki huko huko Zanzibar.
Mnaofikiri huu muungano si wakisanii niambieni nini faida za muungano kwa waTanganyika.
Najua sifai kuweka pua langu kwa hili, lakini kama haya ni kweli na sio propaganda, basi japo munajiita muunga ila uhusiano wenu hamna tofauti na jinsi mimi Mkenya na Mtanzania tunahusiana, yaani nchi mbili tofauti. Inafaa muungane na kuwa nchi moja. Haya napita tu msinipige makumbo, hayanihusu ila dunia kijiji siku hizi.