Kagame ameingia kwenye mfumo, safari hii hatoboi!

Kagame ameingia kwenye mfumo, safari hii hatoboi!

Yaani Paulo aingie mkataba na China? China mkataba wao upo toka enzi za kabila mdogo na wameu renew mwaka jana. Kisa cha USA kusitisha mazungumzo na DRC ni wachina so DRC wameanza kusema kuwa mkataba wa China ni wa zurumati but why now?
 
Ni aibu kwa Rwanda na Burundi kuitwa nchi, halafu eti zinasumbua miafrika hati mizingu huko ulaya, na amerika.
 
Sidhani kama kutimuliana maofisa wa kibalozi kati ya Rwanda na Ubelgiji ni kwamba Rwanda wametangaza vita.

Ubelgiji hawakupaswa kuamua wawe upande upi wa mgogoro huu bali ni kuwa "neutral" na kujaribu kutatua tatizo, wao wameamua kuwa upande wa Congo DRC ambayo raisi wake ameishi Brussels akipikwa kuwa raisi kibaraka.

Pili, Rwanda si wajinga hivyo kuchukua uamuzi huo kwani wametoa sababu kadhaa ikiwemo ya Ubelgiji kuendeleza tabia za kikoloni Katika kushughulikia matatizo ya Rwanda na Congo DRC.

Hata EU wameweka vikwazo vya kiuchumi kwa Rwanda lakini vikwazo hivyo haviguzi sekta muhimu za viwanda uwekezaji na utalii ambapo bado nchi hiyo yaendelea kuwa na Uchumi Imara unokuwa huku kistratejia ikiimarisha mahusiano ya kiuchumi na kijeshi kwa nchi mbadala za mabeberu kama vile Qatar, Singapore na Uturuki hivyo kufanya utegemezi kuwa una mbadala kwa nchi za kibeberu.

Na mwezi jana CEOs kutoka nchi kadhaa za Afrika walikuwa mjini Kigali kuhudhuria mkutano mkubwa wa uwekezaji Katika teknolojia ya kifedha na pia kulikuwa na tour of Rwanda (ya kweli) ambayo ilivutia wageni lukuki.

Hivyo kufungiana ubalozi na kuwekewa vikwazo vyaweza kuwa ndo nyenzo muhimu lakini zisizo na matokeo mabaya sana kwa Rwanda.

Hata hivyo mimi siungi mkono vita wala kinoendelea huko Congo DRC na M23 kwani mamia ya watu wauliwa bila hatia lakini ni lzama kupatikane suluhisho kupitia majadiliano ambayo hayachagui upande wowote na ni lazima madai ya M23 yasikilizwe na uongozi wa Congo DRC.
  • War propagandists often attack historical understanding as a public that doesn’t understand history, or believes a sanitized form of history is more susceptible to war propaganda.
 
  • War propagandists often attack historical understanding as a public that doesn’t understand history, or believes a sanitized form of history is more susceptible to war propaganda.
its is always important to understand the history behind any event.

People often forget that Rwanda had mass murders in 1959 which led to many Tutsis flee to exile.

It was not only genocide in 1994 which went on to last for 100 days, under the noses of Belgium special forces who came not to halt the massacre but only their actions to rescue foreign passport holders which summed up everything.
 
Kama kuna makosa ya Kidiplomasia ambayo Kagame amewahi kuyafanya basi kosa kubwa zaidi ni kitendo cha kutangaza kuvunja uhusiano wa Kidiplomasia na Belgium sasa. Huo ni mtego ambao ametengenezewa Kagame lakini akashindwa kuung'amua vyema labda kwa sababu ya kiburi, hasira na msongo wa mapambano.

Kwa muda sasa imeelezwa kuwa Belgium huenda ndio taifa kinara wa kunufaika na madini ya DRC kwa mgongo wa Rwanda chini ya utawala wa Kagame, ikifuatiwa na USA, UK na South Africa. Lakini kupitia utawala dhaifu wa Tshekedi kule DRC, taifa hilo la DRC likaamua kutaka kugawa migodi yake kwa kandarasi rasmi za uwekezaji za makampuni yale yale ya Belgium, USA, UK na South Africa jambo ambalo litaua mpango wa Rwanda kuendesha vita kule DRC (maana sponsor wake wamekimbia) kwa ujanja na uharaka Kagame akaamua kutengeneza deal jipya na China na baadaye Russia na hapo akaongeza nguvu kwa M23 kuongeza udhibiti wa maeneo zaidi kule DRC.

Chokochoko zikazidi na sasa zimeshika kasi, na rasmi sasa Kagame katangaza vita ya kidiplomasia dhidi ya jumuiya ya Ulaya kwa kuvunja uhusiano na taifa la Belgium ambalo lina nguvu za kiushawishi katika ulaya.
Kwa sasa Rwanda na Kagame wajiandae kwa mambo haya;
1. Kutengwa kimataifa hususani na ulaya na Marekani.

2. Kuwekewa vikwazo vya kiuchumi (Hata hii Tanzanite anayoivuna hapa Tanzania kwa wingi anaweza kukosa pa kuiuza)

3. Kukosa washirika muhimu wa kibiashara (usishangae hata Bandari za Dar, Mombasa, Beira, Djibout zikazuiwa kushusha au kupandisha Cargo za kibiashara na kijeshi za Rwanda)

4. Kutengenezewa mashtaka ya mauaji ya kivita ili kushtakiwa kwenye mahakama ya kimataifa.

5. Rwanda kuyumba kiuchumi, kitalii, Kidiplomasia.

6. Harakati za kumchafua kimataifa na kumpindua kuanzishwa.
alijiona yeye ni mungu
 
Tanganyika tungepata rais kama kagame tungekuwa mbali sana
 
Back
Top Bottom