Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 12,152
- 44,110
Kama kuna makosa ya Kidiplomasia ambayo Kagame amewahi kuyafanya basi kosa kubwa zaidi ni kitendo cha kutangaza kuvunja uhusiano wa Kidiplomasia na Belgium sasa. Huo ni mtego ambao ametengenezewa Kagame lakini akashindwa kuung'amua vyema labda kwa sababu ya kiburi, hasira na msongo wa mapambano.
Kwa muda sasa imeelezwa kuwa Belgium huenda ndio taifa kinara wa kunufaika na madini ya DRC kwa mgongo wa Rwanda chini ya utawala wa Kagame, ikifuatiwa na USA, UK na South Africa. Lakini kupitia utawala dhaifu wa Tshekedi kule DRC, taifa hilo la DRC likaamua kutaka kugawa migodi yake kwa kandarasi rasmi za uwekezaji za makampuni yale yale ya Belgium, USA, UK na South Africa jambo ambalo litaua mpango wa Rwanda kuendesha vita kule DRC (maana sponsor wake wamekimbia) kwa ujanja na uharaka Kagame akaamua kutengeneza deal jipya na China na baadaye Russia na hapo akaongeza nguvu kwa M23 kuongeza udhibiti wa maeneo zaidi kule DRC.
Chokochoko zikazidi na sasa zimeshika kasi, na rasmi sasa Kagame katangaza vita ya kidiplomasia dhidi ya jumuiya ya Ulaya kwa kuvunja uhusiano na taifa la Belgium ambalo lina nguvu za kiushawishi katika ulaya.
Kwa sasa Rwanda na Kagame wajiandae kwa mambo haya;
1. Kutengwa kimataifa hususani na ulaya na Marekani.
2. Kuwekewa vikwazo vya kiuchumi (Hata hii Tanzanite anayoivuna hapa Tanzania kwa wingi anaweza kukosa pa kuiuza)
3. Kukosa washirika muhimu wa kibiashara (usishangae hata Bandari za Dar, Mombasa, Beira, Djibout zikazuiwa kushusha au kupandisha Cargo za kibiashara na kijeshi za Rwanda)
4. Kutengenezewa mashtaka ya mauaji ya kivita ili kushtakiwa kwenye mahakama ya kimataifa.
5. Rwanda kuyumba kiuchumi, kitalii, Kidiplomasia.
6. Harakati za kumchafua kimataifa na kumpindua kuanzishwa.