Kafumaniwa

Yaani wewe MUME/MKE wa mtu mnapanga kwenda kumfumania MUMEO/MKEO bado haijaniingia akilini
HIyo inaweza kukupa idea ni watu wa aina gani hao...

Lazima wana upeo mdogo sana wa kutambua na kuchanganua mambo
 
Kwenye hii kesi kuna watuhumiwa wawili what about the other(Mwanamke). Iweje wakubaliane kumpiga huyu mwanaume mpaka yuko kwenye hati hati ya kupoteza maisha sasa ina maana huyo mwanamke mke wa mtu ambaye naye kafumaniwa hana kosa??.....There is something fishy here

Katika hali kama hii nashawishika kuamini kwamba huenda hawa waliofumaniwa wanachakachuana na labda huyo mwanamke lengo lake ni kumuua mumewe kwa fikra kwamba ataendelea na huyo mume mwingine.....

Kweli mambo yanabadilika, zamani kwenye biblia ilikuwa watu wakizini mwanamke ndie anayepigwa ila ktk hili mwanaume ndo kala kichapo mwanamke mzimaaaaaaaaaaaa
 
Hao wenye mali watafungwa, lakini mambo kama haya yataendelea tu katika jamii kwa kuwa ni human nature. Human being are born selfish. Kwa hiyo si rahisi mtu kuvumilia kuibiwa. Tumesikia kesi kama hizi nyingi tu na bado tutaendelea kusikia kwa sababu uzinzi utaendelea kuwepo. Na mauaji yataendelea kutokea kwani ni nature toka enzi za cleopatra.
 
mze mwenzangu habari imenishtua sana hii

haya mambo waweza ukiahani utani halafu ukaishia shimo la tewa aisee
Huyu dada ambaye alienda kumfumania mumewe sijui atakuwa alikuwa akimwambia jamaa "Piga huyo piga amezoea sana" sipati picha
 
Maty hebu weka mambo sawa hapa....hii ni habari ya kweli?

Sina imani na Maty.....hii haiwezi kuwa kweli bana.

Itakuwaje wampige mwizi dume peke yake?

Yaani babu nianze tu kuleta utani kwenye ishu kama hii hata kama ningekua nataka watu wajifunze singesema amekufa. Unajua hii habari ilikua inafichwa fichwa kwani mazingira ni ya kutia aibu kwamba mwanaume amefumaniwa halafu mkewe ameshiriki kupigwa kwa mumewe walikua wanaona aibu so ilikua inazungumzwa kindugu tu huyo baba akipona ndio wakae waamue nadhani walijua atapona hata mimi alienipa habari alizinyaka juu juu sasa kwa sababu amekufa sidhani kama kitafichwa kitu hapo na mimi nimesikia tu habari ya upande mmoja wa mkaka kwani ndio namjua
 
Katika hali kama hii nashawishika kuamini kwamba huenda hawa waliofumaniwa wanachakachuana na labda huyo mwanamke lengo lake ni kumuua mumewe kwa fikra kwamba ataendelea na huyo mume mwingine.....

Kweli mambo yanabadilika, zamani kwenye biblia ilikuwa watu wakizini mwanamke ndie anayepigwa ila ktk hili mwanaume ndo kala kichapo mwanamke mzimaaaaaaaaaaaa
Huyu mwanamke atakuwa kilaza kweli
 
Sina imani na Maty.....hii haiwezi kuwa kweli bana.

Itakuwaje wampige mwizi dume peke yake?

mie panaponichanganya zaidi ni mke wa huyu "marehemu"..hapo pananiwia pagumu kuamini kwa kweli..kitendo alichokifanya sio cha kusameheka.
 
Kwa nini unabase kwenye kuwapendela wanaume. Sema basi hata wanawake si mali ya mwanaume mmoja ni wa wote


Wat???, imeniuma sana kifo cha huyo mwanaume. Sifurahii uzinifu lakin pia kutoa roho ya mtu mwingine eti kisa nimemfumani siwezi hata siku moja, siwezi kuua ksb sina uwezo wa kuumba pia, naamini ni mungu peke yake anayewza kuchukua roho za watu ksb hata kuumba mungu anaumba.
Huyo mwanamke aliyeshiriki kumuua mumewe hata sielewi nimweke kundi gani.
hivi wanawake (baadhi) mnadhani hao wanaume ni mali zenu binafsi?.
huyo mwanaume ni binadamu tu at any time he can change kwa uzuri au ubaya lazima uwe tayari kupokea hayo mabadiliko.
Tujifunze kudhibiti hasira zetu...haya mambo ya kuwafanya wanaume mali zetu binafsi siyo sahihi kabisa.
huyu ni mali ya mungu na wazazi wake , wewe ni mshirika wake tu ktk mapenzi basi.

r i p marehemu, roho yako iwekwe mahali panapolingana na matendo yako hapa duniani.ameni

kama umemfumania na unaona hauwezi kumsamehe mwenzi wako achana naye kimapenzi , usimuue, binadamu acheni kujifanya watakatifu eti mnatoa hukumu ya kifo kwa mkosaji.
 
Kamanda... haya mambo ya fumanizi sio "one size fits all"

Kila mtu ana reactions zake... kwa wengine hao waliofumania wangeishia kushtuka na kujinyea hapohapo, wengine wangeita wachungaji, wengine wangeanza kusali, wengine wangeua, wengine wangejaza watu nk

haya mambo bwana... Ndio risk za kutema Big G kwa karanga za kuonja hayo

But killing is too far!!

Kamanda aksante unajua yaani hainiingii akilini kwa kuwa yani...........afu na huyo mkewe (wa kaka alofumaniwa) alikuwa anafurahia kabisa mumewe anavyotwangwa au naye alikuwa buzy kumtwanga mgoni wake?? Kwa nini wasigawane kila mmoja akamtwanga anayemhusu?? Ama kweli siku hizi mambo yamebadilika...................... inakuwaje basi sie tunakuwa na reactions tofauti na wazee wetu?? Au wao hawakuwa wakifumaniana/kuchakachua?

Kamanda haya mambo kwa kweli.
 
Hawa nao waliendaje bila utaalamu! Yaaani cku izi unaenda na silaha zote! Unanunuaaaaaaaa ama basi ntawafundisha siri ningine halafu mwendelee kuwa wazinifu!
 
Dah... basi mie nnavyomuamini Maty, unataka kuniambia nimeingia mkenge??

Jamani hii stori ni ya kweli mnaniumiza mnavyodhani kwamba nimetunga, ila muamini msiamini mimi siwezi hata kuwabishia ni bora ningeambiwa mtu ambae simjui hapa nilipo ingawa sina undugu na huyo mkaka nimechoka kabisa, baada ya msiba naahidi kuwaletea kila kilichojiri ili muamini
 
Na huyo mwanamke (mjane) kafaidika nini na hiyo adhabu aliyompa mumewe? aah labda kapata faida ya huo ujane na mali alizoachiwa na mumewe.
LAKIN je ana ujasiri wa kuwaambia wanawe chanzo cha kifo cha baba yao??
Ukisema upige au uue kila ukifumania sasa utapiga na kuua Wanaume/ Wanawake wangapi?, manake hizi kesi ni nyingi sana sasa hivi.

KWELI HASIRA HASARA.
 
ilitakiwa waadhibiwe wote y mwanaume tuuuu! namuonea huruma huyo mmama aliyepanga na mume wa mwenzie wafanye fumanizi then kaadhibiwa mumewe tu.... imekula kwake ujue! kwan yupo mbioni kuitwa mjane kwa kujitakia kwan kila ki2 kilikua kwenye mpango ambao na yeye alishiriki! duh! kasheshe kama wana offsprings kazi kwake kuwalea...
 
SORRY!, Pia Sawa NYUMBA KUBWA nakubaliana na wewe hata mwanamke siyo mali binafsi ya mwanaume, ila hapo juu niliongelea mwanamke ksb hii issue inamhusu mwanamke kuua mume kisa kafumania.
MWANAMKE AU MWANAUME HAKUNA ALIYE MALI BINAFSI YA MWENZAKE.
 
Duh maty inatisha...jamani kuiba uibe usifumwe ukifumwa mwe!! utatamani usingeiba. Mie niulize kuna sheria yoyote juu ya makosa kama haya? Yaani mfano nikiwapeleka mahakamani sheria inasemaje?? Hawa waliofumaniwa nasemea

Yaani mimi baada ya kusimuliwa kwamba huyo kaka anaumwa mahututi baada ya kupigwa kisa kafumaniwa na mkewe ndio alishiriki nikaamua kulileta hapa jamvini tulijadili kwani sikuona ni kwa nini umpige mtu kisa umemfumania na hasa mkewe kushiriki ila hata sikutegemea kama huyo kaka angekufa
 
Mwanaume kampiga mwanaume mwenzie (mwizi wake) mwanamke aloibiwa inawezekana amejipima na mwanamke mwenzie kaona hamwezi, si unajua kuna mimama mingine imeshiba. Ila kwa kawaida reaction ya kwanza kila mtu anajichagulia mwizi wake, si rahisi kumpiga partner wako (mume/mke)

ilitakiwa waadhibiwe wote y mwanaume tuuuu! namuonea huruma huyo mmama aliyepanga na mume wa mwenzie wafanye fumanizi then kaadhibiwa mumewe tu.... imekula kwake ujue! kwan yupo mbioni kuitwa mjane kwa kujitakia kwan kila ki2 kilikua kwenye mpango ambao na yeye alishiriki! duh! kasheshe kama wana offsprings kazi kwake kuwalea...
 
Na huyo mwanamke (mjane) kafaidika nini na hiyo adhabu aliyompa mumewe? aah labda kapata faida ya huo ujane na mali alizoachiwa na mumewe.
LAKIN je ana ujasiri wa kuwaambia wanawe chanzo cha kifo cha baba yao??
Ukisema upige au uue kila ukifumania sasa utapiga na kuua Wanaume/ Wanawake wangapi?, manake hizi kesi ni nyingi sana sasa
hivi.

KWELI HASIRA HASARA.

Hapo sasa na ndio maana hii ilipotokea ilikua inafichwa fichwa mi alieniambia aliambiwa na dada wa marehemu na ni baada ya mkaka kulazwa na kuwa na hali mbaya ina maana angepigwa kidogo tu na kupona hii stori ingefichwa hata tusingesikia kabisa
 
Hao wapuuzi waombe Mungu jamaa asife,akifa mazee hiyo ni mada na wala sio manslaughter kwa sababu wahusika walikaa wakapanga (malice aforethought),adhabu yake ni kitanzi kwa wote wawili,mke wa mtu na mme wa mtu.Hivi siku hizi kuna K na M za kugombea kweli?
 
Back
Top Bottom