Kafulila apewa za uso alivyojibu hoja za Zitto kuhusu ripoti ya CAG

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
Sisi watu weusi na wa hovyo sana!!Huu mjadala nimeukuta kule "mybroadband"(Jf ya south Africa).Hawa viongozi wa Afrika ni wanafiki sana,baada ya hotuba ile ya Malema pale Orlando Stadium,na documentrary ya jana iliyotolewa hadharani kwa mara ya kwanza na e-tv ikimuonyesha Mama Winnie anavyoeleza "option" alizopewa Mandela ili atoke gerezani,huwezi tena kuwaamini wanasiasa wa Afrika

Ndio maana juzi niliwaambia watoto wangu,kama mimi nikiwa hai au hata nimekufa,ningependa sana wao kama wanangu,wasijiingize ktk siasa.Na jambo hili nalisema nikiwa hai,na walikumbuke nikiwa kaburini.

Maana ktk kua yangu,hakuna tabaka la wanafiki nililokutana nalo kama tabaka la "Wanasiasa".Hakuna tabaka lisiloeleweka kama hili...Iwe upinzani au tawala,wanawaza matumbo yao tu.

Huyu Kafulila,sijui ni tatizo la lugha ya "Kimahesabu"?Unaposema deni "hewa",maana yake ni deni ambalo halijathibitishwa na bunge,wala hakuna mahali ambapo bunge limeazimia pesa itoke ili ikalililpe hilo deni,hata kama deni hilo lipo,mpangaji wa kulilipa na kuidhinisha kulipa ni bunge kwa mujibu wa sheria,sasa kama serikali imeamua kulipa tu bila kupitishwa na bunge,hilo ni deni "hewa"...Au tuite "Ghost Debt".

Yaani kwa mfano,baba akupe shilingi 50 ukalipe deni kwa Mzee Sakawe,lakini njiani ukakutana na Mzee Ambwene,ukampe hiyo hela na hata kama kweli alikuwa anamdai baba yako,hilo ni "deni hewa",sababu baba yako alikupa umpe Mzee Sakawe na wewe umempa Mzee Ambwene.Katika mambo ya utawala bora,huo ni utovu wa nidhamu kwa bunge kama ilivyo utovu wa nidhamu kwa baba yako maana umelipa deni kwa mtu ambaye hukutumwa.Eboo Kafulila,umepatwa na nini?

Anasema kuvunja sheria ni kama Mawaziri wangeenda kuwajibu PAC na LAAC,eti sababu Waandishi sio LAAC wala PAC basi hakuna shida.Eboo!!Sheria inawataka CAG akishasoma hayo mapungufu,basi serikali iyafanyie kazi na si kuyajibu wala kuyatolea ufafanuzi,maana kama wataendelea kutolea ufafanuzi jambo ambalo CAG kalitazama kitaalamu,itakuwa ni kutaka kuficha mapungufu ambayo ni kinyume na utawala bora,CAG yupo kisheria,yale anayosema ni MAPUNGUFU hayaitaji ufafanuzi zaidi ya kuyafanyia kazi.Na sheria iliweka PAC na LAAC,maana haikujua huko mbele atakuja mtu anayejiona "Malaika" hakosei,kwa hiyo kama anaona hapati nafasi kujibu bungeni(kisheria) anaamua kununua muda kwenye vyombo vya habari ili kujisafisha.Kitendo walichofanya mawaziri ni sawa na kusema CAG na report yake wamesema UWONGO hivyo tusiiamini ofisi yake.Hili nalo Kafulila halioni kisa kahamia CCM??

Halafu anasema eti hiyo 1.5 trilion hakuna mahali ilipoandikwa.Lakini anakubali kuwa kulikuwa na 25.3 dhidi ya 23.3,na serikali haijasema hiyo 1.5 imeenda wapi na imeitumia kufanya nini...Kweli kwenye dhana ya utawala bora na uwajibikaji unashindwa kuuliza??Yaani wewe muuza duka wako mahesabu yanaonyesha amekusanya shilingi 10,halafu matumizi ya kuongeza mzigo wa dukani ametumia shilingi 9...ukimuuliza hiyo shilingi moja iko wapi basi unakosea?Utawala bora ambao CAG ni nguzo,unatutaka kuiuliza hiyo shilingi 1,maana inaweza kuwa ndio imeenda kulipa deni la bombadia bila kupitishwa na bunge.Hata hili Kafulila unapinga??Loooh...Umepatwa nini mwanangu???

Kuhoji ATCL ni LAZIMA kwa sasa,sababu ndio moja ya mashirika ambayo yanatumia pesa nyingi za walipa kodi kwa sasa,kununua ndege "cash" sio jambo dogo,tena mpaka ndege aina ya B787-800series,CS300 na bombadia mpyaa!!Bado hutaki liwe kipaumbele katika kukaguliwaa.Hili ni shirika ambalo hata AITA imeliondoa kwenye uanachama sbb ya madeni yake,hili ndio shirika ambalo JPM kwa kujua,ameamua ndege alizonunua azisajili kama ni mali ya TGFA(Tanzania Gvt Flight Agency) na si ATCL,sababu wanajua zikiwa zao tu,wanapokwa kwa madeni,sasa tujiulize bila CAG kuchunguza humu ATCL,huu uwekezaji wa kununua ndege in cash,tutakuwa na TIJA huko mbeleni?Na hapa mwanangu KAFULILA huoni hoja ya ZITTO kweli?

Ni kweli IKULU kwa sasa ndio mpangaji wa matumizi ya serikali ya kila siku,Ikulu imepoka madaraka yote ya kifedha.Kibubu cha nchi sasa kinamilikiwa na mtu mmoja.Ndio maana kwa sasa,mashirika na kampuni zilizo chini ya serikali "Account" zake zipo BOT,kila wanachokusanya wanapeleka BOT,kule Mzee ndio anaminya batton ya wapi achukue na wapi atumie.Si ajabu anasimama anasema IGP ntakupa bilioni 10 ujenge nyumba,anasimama anasema Uhamiaji ntakupa bilioni 10 ujenge HQ Dodoma,sasa hizo 10 billion,ni bunge gani limepitisha?Hata hili hujui kuwa kwa sasa Rais ndio Hazina?Mwanangu Kafulila...

TRA inakusanya pesa kama "Wakala",yaani sio sehemu ya makusanyo kama kodi,ni pesa ambazo hapo mwanzoni huwezi kuziona kama "kodi" sbabu mashirika kama TBS,TPA,TCRA,TCAA,TFDA,TAA nk yalikuwa yanakusanya yenyewe kwa mujibu wa sheria ya Gvt Agency ya mwaka 1999(?),sasa TRA inaturundikia kana kwamba ni makusanyo ya kodi na kuimba kuwa kodi ukusanyaji umepanda!!!Hili nalo hulioniiiiii!!!Siasa na njaaa ni balaa...A man with an empty stomach can not be a good political adviser.
 
Njaa mbaya sana. Ndio maana Namuheshimu sana Freeman Mbowe ,this guy could have a price tag but he is not that cheap. Basic principle is to never trust a human being.Usaliti kwa wanasiasa ni jambo la kawaida wapo waliosalitiwa na ndugu zao wa damu,kama Yuda alimsaliti Masihi kwa vipande vya Pesa sembuse binadamu dhaifu wa karne ya Ishirini na moja..

Kitu pekee kinachosimama ni Ukweli..auseme Mbowe au Bashite utabaki kuwa hivyo...
 
Mbona hata huyu Barafu hana chochote alichojibu. Kafulila ameuwa hoja za Zito na wajinga wote wa ufipa.
Wonders shall never end! Mimi sio mchumi, ila sijaona HOJA HATA MOJA ALIYOJIBU KAFULILA. REPORTS ZA CAG Nazifahamu siku nyingi Enzi za Mzee Utoh, nimejifunza kuzisoma na kuzielewa, Sasa kwa akili kama yako,sitegemei uongee tofauti na ulichoongea. Hakuna jibu lolote KAFULILA alilotoa lililozima Hoja za Zitto! Tuache Uchama, tuwe objective kwenye vitu sensitive Kama hivi kwa sababu ndiyo maisha yetu, NI FEDHA ZETU! Tukianza kuweka ushabiki kisa Vyama vyetu Taifa hili litabaki hapa lilipo Karne na Karne! Change your attitude!
 
Njaa mbaya sana. Ndio maana Namuheshimu sana Freeman Mbowe ,this guy could have a price tag but he is not that cheap. Basic principle is to never trust a human being.Usaliti kwa wanasiasa ni jambo la kawaida wapo waliosalitiwa na ndugu zao wa damu,kama Yuda alimsaliti Masihi kwa vipande vya Pesa sembuse binadamu dhaifu wa karne ya Ishirini na moja..

Kitu pekee kinachosimama ni Ukweli..auseme Mbowe au Bashite utabaki kuwa hivyo...
Kweli kabisa, price tag yake mpaka sasa ni Lowasa tu kaifikia.
 
Kuna moja hapo limeandikwa hadi mwili unasisimka, nimelisikia jioni Hii Toka kwa mtu. Yaani kuanzia Bajeti ijayo, tusahau kabisa kabisa matumizi au implementation ya Bajeti kufuata mtiririko. We are finished
 
Poleni, naona Ndugu David, kawashughulikia kihoja sawa sawa. Mtasema yote leo. Go go gooo Ndugu David! Pumzi hawana hawa!
Hivi ndo umefika huku mkuu.Mambo ya msingi kushadadia kama simba na yanga??
Kweli siasa zinatufanya maslai ya Umma hatuyapi tena kipaumbele tunaangalia maslai ya pande zetu.
 
Mkuu nisaidie kitu,maana naona km hisia zangu zinanipeleka kubaya,naomba unijuze hizo masharti alizopewa Winnie ili Mzee madiba atoke lupango maana hyo documentary cjaiona
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom