Kafulila apewa za uso alivyojibu hoja za Zitto kuhusu ripoti ya CAG

Yani awamu hii inavuruga sheria na taratibu zote tulizojiwekea kama nchi.. Na kuna Wapumbaff wachache wanaoishi kwa kulipwa kuja kuvuruga mijadala humu.. nadhani ile 1.5trn isiyojulikana iliko inatumika kulipa hawa wajinga wajinga!
 
Kafulila na Mwakyembe wote ni Vilaza mbele ya watanzania walioamka, lakini CCM wachache wajinga wajinga kama nyinyi ndiyo mnaweza kukaa mkawasiliza Tumbili kafulila na Mwakyembe wake huko walipokaa wakatumia pesa za Umma kutengeneza Sinema za kijinga badala ya kuzitumia hizo pesa kuwasaidia watanzania wanaotaabika kwa shida nyingi.
Nashukuru kwa kushindwa kunishawishi kubadili msimamo wangu
 
Hata mawaziri wamemkosoa mwenyekiti wa PAC kwa kauli ake na kuzipuuza na kuendelea na utekelezaji.
ulitegemea waseme nini ""? wakati wao ndio wapigaji deal wenyew ..ndio maana nikasema kuwa wewe nitatizo"""
 
Mbona heading za huu uzi zinabadilika hivi? Seriously "someone" amechagua hii heading?

Updates,
Safi moderators. Naona mmeirudisha heading kama ilivyokuwa mwanzo.
 
Tangu kuona uovu uliomo ndani ya siasa nilijitenga kwa kuwa huko ni unafiki, uuaji, uswahili ukweli hupindishwa na haki hununuliwa . Ukiingia siasa lazima tu uwe mdangaji kwa haiba ya kucheza na akili za watu psych
 
Mwenyekiti PAC awakosoa mawaziri wa JPM
pic+pac.gif

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Naghenjwa Kaboyoka

Kwa ufupi
Kaboyoka amesema hoja za CAG zinapaswa kujibiwa na maofisa masuhuli na kurudishwa tena kwa CAG.

By Fidelis Butahe, Mwananchi fbutahe@mwananchi.co.tz
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Naghenjwa Kaboyoka amesema si sahihi mawaziri kujibu taarifa ya ukaguzi ya CAG.

Akizungumza bungeni leo Aprili 16, bungeni, Kaboyoka amesema kilichofanyika sasa ni makosa kwa sababu ukaguzi huo umefanyika mwaka 2016/17.

Amesema kama ni ubadhirifu au matumizi mabaya ya fedha si sahihi waziri kueleza kuwa fedha zilizopotea zimeanza kulipwa, wakati ubadhirifu huo umefanyika mwaka 2016/17.

“Sasa leo tuhoji jambo moja, kama fedha hizo zimepotea hizi wanazoanza kulipa sasa wamezitoa wapi. Kama kulikuwa na cheni ya ulaji tutaijuaje. Hicho ndio kitu cha msingi. Hoja za CAG zinapaswa kujibiwa na maofisa masuhuli na kurudishwa tena kwa CAG ili ahakikishe kama kilichojibiwa ni sahihi,” amesema Kaboyoka.

Wiki iliyopita mawaziri waliitisha mkutano na wanahabari kujibu hoja zilizoibuliwa katika ripoti ya CAG.
Mkuu,hii ilipaswa kuwa mada(thread) inayojitegemea.
 
Tatizi pia LA siasa kila mtu analeta hoja kuponda kitu cha mwenzake hata kama ni jambo jema yaani hawezi kukubali, hivi hata kama jambo ni la kisomi ni kutokana na tafiti hawezi mpizani wake kusifu, akikusifia ujue wewe ni mwenzake.
Mfano mzuri ni report ya professor furani aliyekuwa chama cha upinzani , report yake ilisifiwa pindi wanachuo dodoma wakisimamishwa masomo yao . Lakini baada ya muda mfupi akawa katibu MKUU wa wizara furani na kujivua uanachama wa chama pinzani .

Siasa siku zote niunafiki, uchonganishi, wizi, na ubakaji wa haki za watu.
 
ulitegemea waseme nini ""? wakati wao ndio wapigaji deal wenyew ..ndio maana nikasema kuwa wewe nitatizo"""
Nabaki na msimamo wa hujanishawishi.


MWANASHERIA ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema hatua ya mawaziri kueleza utekelezaji wa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) si kupingana naye ila kutekeleza wajibu wa kutoa taarifa kwa wananchi.

Pia Naibu Spika, ambaye kitaaluma ni mwanasheria, Tulia Ackson amesema sheria haimbani mtu yeyote kusoma na kujadili ripoti ya CAG na kwa kufanya hivyo si kujibu hoja bali ni kutoa mawazo yao.

Mwakyembe alitoa kauli hiyo baada ya kuibuka kwa hoja za kupinga hatua ya mawaziri kuzungumza na waandishi wa habari kuhusiana na hoja zilizotolewa na CAG kwa wizara zao.

"Ukiisoma kwa macho ya kisheria, Sheria ya Ukaguzi Sura ya 418 kama ilivyorekebishwa na Bunge mwaka 2012, sheria hii inawataka maofisa masuhuli waandae taarifa ya kuelezea madhaifu yote aliyoelezea CAG katika maeneo yao.

“Na taarifa yao wanatakiwa wampelekee Katibu Mkuu wa Hazina. Kwa hiyo kila Katibu Mkuu ambaye kuna suala lake limeongelewa anatoa maelezo na mpango kazi na namna ya kutatua hayo na kumpelekea Katibu Mkuu wa Hazina, hayo ni mahitaji ya kikatiba na kisheria.

"Akishapokea sheria inamtaka Katibu Mkuu wa Hazina ajumuishe taarifa hizo na mpango kazi na anaziwasilisha kwa Waziri wa Fedha ambaye anachokifanya ni kuwasilisha mpango kazi na majibu ya serikali bungeni au anaweka mezani bungeni.” Waziri Mwakyembe aliongeza:

"Nikiwakumbusha tu kwamba kifungu cha 30 kifungu kidogo cha 3 cha sheria kinasema bayana kuwa taarifa ya Waziri wa Fedha itawekwa mezani sambamba na taarifa ya ukaguzi wa CAG."

Mwakyembe alisema hatua ya Mawaziri kuelezea utekelezaji wa hoja za serikali si kupingana au kubishana na CAG kwa sababu CAG ndiye mwenye jukumu la kuainisha mapungufu na Mawaziri kuyafanyia kazi mapungufu hayo.

Alisema taarifa ya ukaguzi za CAG tayari zimewekwa mezani na kila mwananchi ana haki ya kusoma na kujadili.

"Kwa sababu hakuna sheria inayosema akishawasilisha CAG atazungumza na waandishi wa habari na ndivyo ilivyo kwa Mawaziri nao hawazuiwi na ndiyo maana badala ya kila Waziri kutafutwa na waandishi mmoja mmoja kwa nyakati tofauti tumeweka utaratibu wa Mawaziri kukutana na waandishi wa habari.”

Alisema kutokana na uhuru huo ndiyo maana hata vyama vya siasa vimeibuka na kuijadili ripoti ya CAG na kusisitiza kuwa hatua ya Mawaziri kuzungumza hawavunji sheria yoyote.

Alisema ni wajibu wa kikatiba walionao kama serikali baada ya kusikia upande mmoja kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi za upande wa pili na kwa wakati.

Awali, Naibu Spika Tulia akitoa muongozo kwa wabunge, alisema kwa mujibu wa kanuni na sheria zilizopo wabunge wasiwe wepesi kuzungumza mambo ambayo hawajayapitia kisheria.

"Sisi tukizungumza tunaonekana tumetoa msimamo fulani kwa sababu ndivyo wananchi wanavyotuona maana sisi ndio wawakilishi wao.

"Kama ambavyo sheria hamkatazi CAG kuzungumza na vyombo vya habari, kwa namna hiyo hiyo haimkatazi yeyote kuizungumzia taarifa ya CAG.”

Alisema sheria haijasema CAG azungumze na vyombo vya habari pia, haijamkataza yeyote ikiwa ni pamoja Waziri au Naibu Waziri kuzungumzia taarifa hiyo.

Dk Tulia alieleza CAG hana mahali anapopeleka taarifa yake bungeni isipokuwa kupitia kwa Waziri, kwa hiyo Mawaziri wanavyotoa maelezo si kwamba wanajibu hoja za CAG, kwani hoja hizo zinajibiwa kwenye kamati kwa mujibu wa sheria.

"Anayejibu kwenye kamati ni ofisa masuhuli husika. Tusitake kuliweka hili jambo kuonesha hakuna utawala wa sheria nchini. Sheria zipo tuzipitie kabla hatujatoa maelezo.”

Aliongeza: "Sheria iko wazi ikishaletwa hapa bungeni kila mtu yupo huru kuizungumzia kwa sababu ipo wazi kwa umma. Yanayojibiwa ni kwenye kamati na mengine ni maoni kama yanayotolewa na vyama ambavyo vimeshaisoma na kuitolea maoni yake.”
 
yule Tumbili nilisoma nae ni mtu anaehangaishwa sana na njaa anapenda kujitutumua aonekana.. ni wa kumdharau tu
Kafulila kweli{ very difficult person}kwa sasa kachagua upande usio sahihi lakini yote ni njaa kali.asingeweza kumiliki lile toto cheupe kule mjengoni bila pesa
 
Hoja ipo vizuri sana ila mwanzoni umeharibu kabisa uliposema wanao wasijihusishe na siasa. Mnasahau kuwa siasa ndyo uchumi na ndyo maendeleo. Alafu hata wewe mbona unajihusisha na siasa alafu anakataza wanao. Unakuwa kama mzazi anaozuia watoto wake wasifanye mapenzi wakat yeye ni kupitia kufanya mapenzi aliwapata ao watoto.
 
Wonders shall never end! Mimi sio mchumi, ila sijaona HOJA HATA MOJA ALIYOJIBU KAFULILA. REPORTS ZA CAG Nazifahamu siku nyingi Enzi za Mzee Utoh, nimejifunza kuzisoma na kuzielewa, Sasa kwa akili kama yako,sitegemei uongee tofauti na ulichoongea. Hakuna jibu lolote KAFULILA alilotoa lililozima Hoja za Zitto! Tuache Uchama, tuwe objective kwenye vitu sensitive Kama hivi kwa sababu ndiyo maisha yetu, NI FEDHA ZETU! Tukianza kuweka ushabiki kisa Vyama vyetu Taifa hili litabaki hapa lilipo Karne na Karne! Change your attitude!
Kiukweli vyama vimetuvuruga hadi inakera, kuna wakati yatupasa tusimame kama taifa. Kinachoshangaza wengi wanafikiri kuhoji ni kosa na ili kumsaidia Raisi yatupasa tusiwe wanafiki,tumshangilie pale panapotupasa kumshangilia na tukiona watendaji wake wameenda wrong ni vizuri kuhoji ili na yeye Mh aone wapi kuna shida ili arekebishe. Naamini sote nia yetu ni njema tu kwa mstakabari wa nchi, tatizo ni misimamo ya vyama hadi tunashindwa kujielewa kipi tushangilie na kipi tuhoji. Na kuhoji isieleweke kama ni kuzomea.
 
Hapa ndipo tulipofika, ndipo Awamu ya 5 ilikotufikisha katika kipindi kifupi sana.

Think tank yao ni ya akina Bashite, Kibajaji, Msukuma, Musiba, Mtoto wa Celina Kombani na huyo Kafulila na wanafiki wengine.

Ukweli ni kuwa tusipoendelea kuipigania nchi yetu hasa kwenye mambo ya msingi na utawala bora tukawaachia hawa "tumbili wazalendo" tutavuna mabua. Pia kwa vile tunajua uwezo wao na tabia zao kuwaachia waharibu nchi wapendevyo bila kuwapinga na kuwazuia ni dhambi kubwa.

Maandamano ya tarehe 26 April yanazidi kunakshiwa na haya madudu na aina ya utetezi wa Kafulila.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom