Kafulila amjibu mwenyekiti wa CCM

Kafulila amjibu mwenyekiti wa CCM

1: kama kuna watu (ccm) ambao wanadai maoni ya watu 17000 juu ya kuwa na serikali 3 ni idadi ndogo sana ambayoyo haiakisi matakwa ya watanzania 46ml, je hawa wabunge 600 wanapata wapi nguvu ya kuwa na uwakilishi wa wananchi ili hali wao ni wachache zaidi kuliko hata hao waliotoa maoni juu ya kuwa na serikali 3?

2: Amehoji kama ishu ni kumtii mwl nyerere ambae hakuta kuvunjika kwa muungano,wamesahau kuwa mwl alikuwa anabadilika kulingana na wakati. Mf mwaka 1965 mwl alifuta vyama vingivlakini kulingana na mabadiliko yaliyohitaji mageuzi mwaka 1992 ni mwl uyohuyo aliweze kuwa na vyama vingi ambavyo alivifuta hapo mwanzo. Akauliza je mwl angekufa kabla ya kuanzishwa vyama vingi inamaana mpaka sasa kungekuwa na chama kimoja tu?

3: Viongozi waliopo madarakani leo wafanikishe kuwa na muungano mzuri zaidi wa serikali 3 kwakuwa hii nafasi walionayo hawatakuwa nayo tena miaka ijayo kwani ni dhahir wingi wao (ccm) utapungua hivyo watalazimika kukubali mabadiliko kwa shinikizo kubwa kitu ambacho kitazalisha muundo mbovu zaidi . Hili alitoa kama ushauri kwa viongozi waliopo madarakani kutumia hii nafasi kufanya mabadiliko mazuri tena kwa busara kuliko kusubiri presha hapo baadae.

4: Kama ishu ni mapato ya serikali ya muungano,amependekeza mapato yatokanayo na customs yote yawe ya muungano. Akafafanua kuwa zipo hoja kuwa kuna wanaodai ikiwa hivyo bara(tanganyika) italipa zaidi,akasema hilo sio shida kwani matumizi makubwa ya hiyo fedha yataelekezwavbara pia kwenye maeneo kama ya magereza,ulinzi,uhamiaji,polis nk. Akauliza wanaodai kuwa hili likitekelezwa watu wa bara watabeba huo mzigo,je kwa sasa ni kinani wanabeba huo mzigo?

5: Akaeleza kuwa tafiti zinaonesha kuwa muungano upo kwenye maeneo matatu ambayo ni ; serikali moja, serikali ya shirikisho na ile ya mkataba. Sasa hii yetu ni ya mfumo gani mbona haieleweke inafiti mfumo gani?

6: Akauliza kuwa kwakuwa muungano huu uliopo kwa sasa umedumu kwa takribani miaka 50, na umeshindwa kutatua changamoto zilizojitokeza kwa kipindi chote cha nusu karne, Je viongozi wanataka wapewe karne kangapi zaidi ili waweze kutatua hizi changamoto zilizopo?

7: Akafafanua zaidi kwa kusema wanaomhukumu jaji warioba wanamuonea. Akaeleza kuwa ukifanya tafiti na ukapata majibu kama ya wale walikutangulia kufanya tafiti maana yake ni kwamba hayo majibu ni sahihi. Sasa kwakuwa tume zilizomtangulia jaji warioba pamoja na wataalamu mbalimbali waliwahi kufanya tafiti juu ya muundo wa muungano na kuja na majibu ya serikali 3 inakuwaje leo wakatae hoja ya warioba ilihali inaendana na hoja za watangulizi wake kwenye jambo hilo?

8:Amehoji kama ofisi ya raisi,ya makamu wa raisi na ya waziri mkuu zote zilipendekeza serikali 3 inakuwaje tena ndani ya muda mfupi watu haohao wageuke na kudai serikali 2, au walitoa hayomaoni ili mwishowe waje wamdhalilishe jaji warioba?

9: Akaeleza kuwa yeye ni kijana mdogo lakini anamuheshimu sana jaj warioba. Akadai anashangazwa na watu wakawaida sana ( ambao ni wajumbe wa bunge la katiba - kwa mtizamo wangu lakini) ambao wanamdharau jaji warioba ilihali sio level yao kabisaa kwani jaji warioba yupo next level kabisa na anaheshimika ndani na nje ya nchi, hivyo inakuwaje watu wa kawaida sana wamtreat jaji warioba kwa kiwango cha chini sana ili hali yeye sio level yao?

10: Muundo wa serikali 3 ndio utakaotatua changamoto za sasa na zijazo,kuliko kufichaficha mambo kwa kisingizio cha serikali mbili kwani huko tuendako kutakuwa kigumu sana.

11: kasema chama tawala mna wasomi wazuri tu,maprofesa wengi tu hivi kweli wameshindwa kuliona hili

12:...
mkuu yegella nimeiongeza size tu tuweze kuisoma vizuri!

Asante sana mkuu..
 
JK alisema lini na wapi kuwa Jeshi litachukua nchi wananchi wakiamua Serikali 3? Mbona mnapenda sana kuzusha mambo?

mkuu inamaana hukumsikia alivyokuwa anabwata bungeni siku anazindua bunge la katiba..
 
Jamii ipi unayosema? Ni ile ya watu elfu 17?

daah, mkuu kwa hiyo kikwete siyo rais wa nchi hii maana waliompigia kura 5 mil tu kati ya watanzania 46 mil bado kwenye mil 5 uchakachuzi ni mwanzo mwisho...
 
Tatizo vijana humu wanaposikia maoni ya wananchi sijui wanapata picha gani, wananchi huku vijijini hawako aware hata kama kuna muungano. Wananchi wako bize kupalilia mahindi, wanasiasa huku utasikia mi nimetumwa na wananchi wa ubungo, msitusingizie wanannchi parurareni wenyewe huko na ma agent wenu humu jf: bwahahaha!

najiuliza hata hiyo elimu ya kukuwezesha kufukua JF na kutype haya nani amekuwezesha maana ulipaswa kuwa milembe..
 
The above statement, by virtue of the Republic of Tanganyika and the Republic of Zanzibar People, shall be hereby accepted by the majority in the society.

And this is true also to Prof Lipumba in lieu of his clarification defending minority wing!
 
Tatizo vijana humu wanaposikia maoni ya wananchi sijui wanapata picha gani, wananchi huku vijijini hawako aware hata kama kuna muungano. Wananchi wako bize kupalilia mahindi, wanasiasa huku utasikia mi nimetumwa na wananchi wa ubungo, msitusingizie wanannchi parurareni wenyewe huko na ma agent wenu humu jf: bwahahaha!

Unenayo yaweza kua kweli, maana hapa hapa Tanzania kuna waziri moja (jina lake halali silijui), alishindwa kujua nchi yake imetokana na muungano wa nini na nini.
Endeleeni tu kupalili mahindi ikiwezekana mpalilie hata mchicha, kesho tutakupeni uwaziri tena.
 
Mleta thread usichokipenda sio lazima ukipe majina. Pumba maana yake nini, acha kutumia vibaya uhuru wa kwenye keyboard. Usipost kama umekulia mtaani. Juzi nilimuangalia Mnyika baada ya kumuita Kikwete dhaifu adabu imemrudia anamuita mh rais.
 
The Tanganyika citizens of Bukoba, part of Tanzania

Awards David Zacharia Kafulila (MP)

a Doctorate Degree for His proper use of Common Sense

in the Struggle to Liberate Tanganyika.

​

Tuseme UKAWA kwa ujumla wao
 
mkuu inamaana hukumsikia alivyokuwa anabwata bungeni siku anazindua bunge la katiba..

Msamehe bure, inaonekana anadandia gari kwa mbele na hakusikiliza hotuba ya mkulu wa kaya.
 
Mleta thread usichokipenda sio lazima ukipe majina. Pumba maana yake nini, acha kutumia vibaya uhuru wa kwenye keyboard. Usipost kama umekulia mtaani. Juzi nilimuangalia Mnyika baada ya kumuita Kikwete dhaifu adabu imemrudia anamuita mh rais.

Usiseme wananchi hawajui!
Sema wewe mwenyewe hujui!
Watashindwaje kujua wakati wanasoma Muungano shule ya msingi?!
Au unao uhakika kwamba elimu waliyoipata ni duni kiasi cha kuwapotezea kumbukumbu?!
 
Usiseme wananchi hawajui!
Sema wewe mwenyewe hujui!
Watashindwaje kujua wakati wanasoma Muungano shule ya msingi?!
Au unao uhakika kwamba elimu waliyoipata ni duni kiasi cha kuwapotezea kumbukumbu?!

Umenikariri dogo, quote hiyo sijazungumzia muungano anza tena.
 
Huyu kijana kanikosha sana tena sana,hususani hapo alipowalinganisha wanaomkashifu jaji warioba na hao makada waccm kusema kweli katika wabunge wote wa ccm waliomo kwenye bunge maalum la katiba wawe ma prof,dr au vyovyote vile kiheshima hakuna anayeweza kumfikia mzee wetu warioba na wala haiji kutokea kwa hao makkada wa ccm kufikia level ya jaji warioba.big up kafulila big up ukawa big up jaji warioba watanganyika tuko nyuma yenu.
 
kama kuna mtu hakumuelewa kafulila leo basi huyo ana matatizo siyo bure.

Kwa watakaoweza angalieni upya mawasilisho ya wachache na hasa angalieni body language za mawaziri mmoja mmoja utagundua jinsi wengi wao wanavyojuta kimya kimya kuwa upande unaopingana na Ukweli(facts).bila wao kujua walikuwa wanaakisi mawazo yao.
 
Mleta thread usichokipenda sio lazima ukipe majina. Pumba maana yake nini, acha kutumia vibaya uhuru wa kwenye keyboard. Usipost kama umekulia mtaani. Juzi nilimuangalia Mnyika baada ya kumuita Kikwete dhaifu adabu imemrudia anamuita mh rais.

Sio uongo Jk aliongea PUMBA dhidi ya Tanganyika yetu.
 
Jamani nchi hii kama tukiwaachia watu wasio na mapenzi mema, kama chama tawala! Wanavyofanya tutatengeneza taifa lenye mpasuko mkubwa kwa ndani wakati kwa nje litaonekana la amani ya uwoga na unafiki kwa sababu ya kikundi kidogo cha watu wenye maslahi ya ufisadi kwa Taifa! Tukiacha maneno mazuri ya Kafulila yasiyo na shaka ndani yake kwa wale tulioangalia Bunge leo! Kuna mjumbe ambaye naye aliongelea vizuri muundo huu! Wa serikali tatu, na jinsi gani serikali ya Tanganyika ni lazima kwa yoyote mwenye uchungu wa nchi hii, huyu mzee Makaidi aliwapongeza ZNZ kwa kutambua uzalendo wao mapema na kudai nchi yao mapema! Iweje sisi tuikane Tanganyika yetu hii leo, tutawaambia nini wajukuu zetu pale ambapo watakutana na changamoto hapo baadae, na fursa ya kutengeneza katiba ambayo inaacha nchi mbili huru na kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto za muungano tulipata! Ahsante kafulila na Makaidi! Mi nasema ni vizuri tufikirie serikali tatu na sasa bunge liongelee serikali tatu ambazo zitakuwa bora kwa mataifa haya! Kuliko kukataa tatu na kufikiria mbili ambazo kwa miaka hamsini hazikuwa na tija kwa watanzania zaidi ya migongano kila kukicha! Ndg zng tuwe wazalendo kwenye hili! Wabunge na vibaraka mlioteuliwa na Raisi tuwe wa kweli huyo anayekulazimsha leo upende mbili baada ya mwakani hayupo hata akikuchukia leo haijalishi! Tatu ndio mpango.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
Iwapo hili la katiba, mkuu wa nchi na timu yake wameshikilia misimamo ambayo imejaa hisia zaida,sishangai sasa ni kwa vipi na kwa nini nchi tatu za EAC zimeamua kufanya mambo yao na kuitenga Tz, Tatizo ni lile lile la wale wale kushikilia misimamo isiyoeleweka hata kwa majirani zetu na mkuu yule yule na timu yake ile ile.
 
Kafulila ametoa hoja zake kwa Busara sana..
Tunahitaji watu wa kujenga hoja kwa weldi kama Kafulila.
Hata Rais wa nchi ni vyema akajifunza kutoa hoja kwa Hekima na weledi kama Kafulila..
 
Back
Top Bottom