muda wa ukombozi
Senior Member
- Jun 28, 2013
- 129
- 118
Jamani nchi hii kama tukiwaachia watu wasio na mapenzi mema, kama chama tawala! Wanavyofanya tutatengeneza taifa lenye mpasuko mkubwa kwa ndani wakati kwa nje litaonekana la amani ya uwoga na unafiki kwa sababu ya kikundi kidogo cha watu wenye maslahi ya ufisadi kwa Taifa! Tukiacha maneno mazuri ya Kafulila yasiyo na shaka ndani yake kwa wale tulioangalia Bunge leo! Kuna mjumbe ambaye naye aliongelea vizuri muundo huu! Wa serikali tatu, na jinsi gani serikali ya Tanganyika ni lazima kwa yoyote mwenye uchungu wa nchi hii, huyu mzee Makaidi aliwapongeza ZNZ kwa kutambua uzalendo wao mapema na kudai nchi yao mapema! Iweje sisi tuikane Tanganyika yetu hii leo, tutawaambia nini wajukuu zetu pale ambapo watakutana na changamoto hapo baadae, na fursa ya kutengeneza katiba ambayo inaacha nchi mbili huru na kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto za muungano tulipata! Ahsante kafulila na Makaidi! Mi nasema ni vizuri tufikirie serikali tatu na sasa bunge liongelee serikali tatu ambazo zitakuwa bora kwa mataifa haya! Kuliko kukataa tatu na kufikiria mbili ambazo kwa miaka hamsini hazikuwa na tija kwa watanzania zaidi ya migongano kila kukicha! Ndg zng tuwe wazalendo kwenye hili! Wabunge na vibaraka mlioteuliwa na Raisi tuwe wa kweli huyo anayekulazimsha leo upende mbili baada ya mwakani hayupo hata akikuchukia leo haijalishi! Tatu ndio mpango.
Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums