Kafara Katika Kuvuta Wateja Katika Biashara Yako

Kafara Katika Kuvuta Wateja Katika Biashara Yako

Abtali Mwerevu

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2013
Posts
773
Reaction score
668
Katika mfumo wa maisha tunayoishi, imejengwa misingi kwamba, wengi wawe masikini na matajiri wachache. Kwa hivyo, kama upo kundi la umasikini, kutoka humo siyo kazi nyepesi, ni lazima uzijue kanuni za kiulimwengu.

Kuanzisha biashara ni jambo jepesi kupata wateja ni jambo gumu. Wateja wengi ni mlango wa utajiri, kama biashara zote zingepata wateja wengi, matajiri wangekuwa wengi duniani. Changamoto ipo katika kuwapata wateja, na hii husababisha biashara nyingi zife! Biashara nyingi zinazosalia inapatikana hela ya kula tu. Ukipambana kwa bidii sana utajenga nyumba na utahamia kabla haijakamilika!

Kwa hivyo kumbe kuwapata wateja ni jambo gumu kwa sababu wateja wengi ni mlango wa utajiri, utajiri hauji kwa lelemama, lazima uzifahamu kanuni!

Kutegemea bahati ni njia mojawapo ya kupata wateja wengi katika biashara yako, lakini njia ya uhakika zaidi ni kutoa kafara ya mnyama! Kafara ya mnyama si jambo geni, hata katika dini nyingi lipo jambo hili.

Mchanganuo wa Kanuni ya bahati

Mara nyingi kutegemea bahati kutakupa wateja 0 mpaka 10 kwa siku. Sawa na faida ya Tsh. 0 mpaka Tsh. 10,000 kwa siku.

Mchanganuo wa Kafara ya Mnyama

Kafara ya kuku


itakupatia wateja 10 mpaka 20 kwa siku. Sawa na faida ya Tsh. 10,000 mpaka 20,000.

Kafara ya mbuzi

itakupatia wateja 20 mpaka 40 kwa siku. Sawa na faida ya Tsh. 20,000 mpaka Tsh. 40,000 kwa siku.

Kafara ya ng’ombe

itakupatia wateja 40 mpaka 80 au zaidi kwa siku. Sawa na faida ya Tsh. 40,000 mpaka Tsh. 80,000 au zaidi kwa siku. Kafara ya ng’ombe ndiyo kafara pekee ambayo inaweza kukupa wateja wengi zaidi ya kiasi kilichotajwa, pengine ndiyo sababu Chief God Love (Kijana anayesaidia watu kupata fedha: simfahamu, namsikia tu…) inasemekana kwamba huko Bunju matajiri humfuata na huchinja ng’ombe wengi sana kwa ajili ya kafara.

Namna ya kufanya

Chinja mnyama wako wewe mwenyewe au tafuta msaidizi. Kinga damu yake katika kikombe.

Chimba shimo katika eneo lako la biashara. Weka ile damu ya mnyama kisha fukia.

Kama ni kuku tamka maneno haya unapofukia:

ULIMWENGU, POKEA SADAKA HII YA KUKU, NAMI NAOMBA WATEJA KATIKA BIASHARA YANGU, KWA KIPIMO CHA KUKU.

Kama ni mbuzi tamka maneno haya unapofukia:

ULIMWENGU, POKEA SADAKA HII YA MBUZI, NAMI NAOMBA WATEJA KATIKA BIASHARA YANGU, KWA KIPIMO CHA MBUZI.

Kama ni ng’ombe tamka maneno haya unapofukia:

ULIMWENGU, POKEA SADAKA HII YA NG’OMBE, NAMI NAOMBA WATEJA KATIKA BIASHARA YANGU, KWA KIPIMO CHA NG’OMBE.

Kama huwezi kuchimba katika eneo lako la biashara kutokana na mazingira kuwa magumu, tafuta ndoo, ijaze udongo, iweke sehemu ambayo haina vurugu, chimba humo shimo na toa sadaka. ndoo hiyo ikae muda wa miezi mitatu ndipo iondolewe.

Nyama iliyobaki kule nyumbani unaruhusiwa kuila, kama huwezi kuimaliza, wagawie majirani na hairuhusiwi kuiuza.

Baada ya dawa nini kifanyike?

Kuwa mtu mwema, usiwe chanzo cha ugomvi na watu. Kamwe tafuta kila mbinu usigombane na wateja wako, ikitokea uwe umechokozwa sana na hakukuwa na namna nyingine.

Unapokutana na wateja wako wa zamani, hata kama walihama kununua katika biashara yako, wasalimie kwa furaha huku ukiwaambia wafike tena katika biashara yako kuna mambo mapya na bei zimeshuka.

Kwa kuwa ulimwengu utakuzawadia mema, nawe jifunze kutoa, ishike kanuni hii, mteja yeyote atakayekuletea mteja mpya, mpe bidhaa moja ya bure!

Kama umechoka kutegemea bahati kuwasubiri wateja katika biashara yako, ijaribu njia hii. Kwa kuurejeshea ulimwengu kilicho chake, nao utakurejeshea kwa kipimo kitakachokufurahisha.

Kama Una Swali, Uliza Nitajibu, au Wasiliana Nami Moja Kwa Moja Kwa Kugusa Hapa.
 
Mtafika kwenye maziwa na aslali mkiwa mmechoka sana... Wengine mtapata ukilema njiani na hamtofika
 
Kwa taarifa zaidi waguse hapo sio basi sawa,,,,, !

Kenge mpaka aone damu zinamtoka ndo ajue kaumia
 
Hakuna kazi ngumu kama kumshauri mtu anaetaka kutapeliwa.

Kenge hasikii mpaka atokwe damu.
 
Kuna binti namfahamu kafanya hadi ulozi ili apate mLi kama kak ake lzm alifikia kuuza gari
 
Wewe umefanya hivi na sasa uko wapi kati ya hapa ?
Milionea
Lakinea
Bilionea
Tirionea
Shilingi nea
Katika kiwango cha fedha sina uhakika kwa sababu huwa sihifadhi fedha badala yake hununua vitu. Kwa upande wa wateja, biashara yangu sifanyi biashara ya vitu bali natoa huduma, mimi ni mwalimu na katika shule yangu nina idadi ya wanafunzi wasiopungua 40, lakini hawazidi 80.
 
Hakuna kazi ngumu kama kumshauri mtu anaetaka kutapeliwa.

Kenge hasikii mpaka atokwe damu.
Mkuu, unatapeliwa nini hapo ikiwa tiba yote imeelezwa bila kuacha kitu? Hapo mtu anaweza akacheza na andiko akatengeneza mambo yake bila hata kuwasiliana nami.
 
Back
Top Bottom