Kafara halina rivasi

Kafara halina rivasi

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,096
Reaction score
828,928
Wote tunamfahamu nyoka. Nyoka hana rivasi. Yaani nyoka ni tofauti kabisa na viumbehai wengine; hawezi kurudi kinyumenyume kama kifurukobe. Pikipiki imeiga mfumo huo wa nyoka - haina reverse gear.
Ndugu zangu wa JF, tunapopata muda wa kushauriana mawili matatu ni lazima na ni muhimu tufanye hivyo. Haya ni maandishi hayafutiki, huwezi jua yatamfaa nani, lini na wapi

Furaha ya kila mtu ni kuwa na mafanikio ya kiuchumi na kumiliki mapesa mengi. Yaani kuwa tajiri wa viwango tofauti. Na katika hili la kusaka mafanikio ya kiuchumi kuna wengi wetu tumedanganywa kutumia njia za mkato.

Njia za mkato ziko nyingi tu lakini zote zina risk zake. Ni vyema mtu akatafakari kuhusu minimum risk kwakuwa ukiutaka utajiri na mafanikio katika umri mdogo unaweza kuishia pabaya sana.

Tukiachana na njia nyingine zote za mkato, hebu leo tujikite kwenye hili la makafara na maagano kupitia uchawi na ushirikina. Hili wengi wetu huliona la salama zaidi lakini ndio baya kabisa.

Unapokuwa kwenye harakati za kusaka mafanikio ya kiuchumi lazima utakutana na hili jambo kupitia mawakala maalum wa ulimwengu wa giza. Hawa watakushawishi na kukupa mifano hai ya watu waliofanya hivyo na wakafanikiwa bila madhara yoyote, kitu kitakachokushinda kuuliza ni kwanini yeye hafanyi.

Kafara na viapo vya kusaka mafanikio ya kiuchumi na utajiri hujumuisha damu. Damu ya kiumbe hai hasa wanyama wafugwao kama kuku, mbuzi ng'ombe nk. Ili kupata damu yao inabidi umuue. Kwahiyo unayakatisha maisha yake kimwili ili wewe upate. Maisha haya kuna wakati hukatishwa kwa ukatili mkubwa na maumivu. Hivyo damu yake huwa juu yako. Kisasi cha malipizi huzaliwa hapa. Madhara yako utayaona kitakapokuwa na kukomaa.

Hilo ni jambo la kwanza. Jambo la pili, kila kiumbe hai kina life span yake hapa duniani kimwili. Hivyo unapomtumia kiumbe kwenye kafara unakuwa umekatisha maisha yake kimwili lakini sio kiroho. Kuna muda wake life span ukifika hufa kweli sasa kama umemtumia kwa makafara basi lazima uyumbe.

Unapoyumba kwenye mafanikio yako kiuchumi itabidi urudi kwa mtaalam wako naye bila kukwambia ukweli atakwambia nyota imeshuka hivyo ni vema kukoleza. Hapa kafara huwa tofauti na la mwanzo lakini pia kuna wakati wa kutaka kuondoka kwenye stage moja kwenda nyingine hapa napo kafara ni tofauti.

Kadiri unavyofanikiwa na kadiri unavyopata changamoto za kulinda utajiri wako ndivyo utakavyozidi kutoa makafara makubwa zaidi mpaka kufikia kafara la binadamu baki na hatimaye ndugu, uzao wako na mwisho kabisa shina lako ambalo ni mzazi.

Makafara hayana rivasi. Kutoa kafara dogo kuliko lililotangulia ni kurudi nyuma kiuchumi. Nani anaweza kukubali?

Huwezi kuliacha kafara labda tu ukubali kufilisika na kubaki masikini wa kutupwa. Hii ndiyo pekee inaweza kuwa salama kwako.

Binadamu tumeumbiwa maadui. Mtu anaweza kukuchukia tu bila sababu yoyote hasa kama una mafanikio fulani. Hivyo basi, ukichanganya damu za roho zinazokulilia ulizitoa Kwenye makafara na hizi chuki nyingine za kawaida za kibinadamu utajikuta una mali lakini huna amani, huna raha huna furaha.

Muda wako mwingi utatawaliwa na mashaka mengi. Mashaka ya kujilinda wewe na utajiri wako. Mashaka ya kujilinda na maadui na washindani wako. Mashaka ya kujilinda na damu ulizomwaga. Unakuwa huna amani ya rohoni na muda mwingi ni mtu wa ratiba, mipango na kukimbiakimbia. Kulala kwako saa sita usiku kuamka saa 11 alfajiri.

Kafara haina rivasi wala mwisho mwema. Kafara huambatana na viapo, viapo hivi ni kuuza roho yako kwa shetani. Gharama ya kuikomboa huwa ni kubwa mno na wengi wameshindwa.

Tafuta mali lakini epuka kafara za damu na viapo vya kutii mamlaka za kuzimu.
 
Duu ndugu kaimu kamishna kaka mwandamizi msaidizi Mshana Jr nimeamka saa kumi na moja kasoro dk sita nikaenda ku soso kisha nikarudi mezani...inawezekana na mimi ninatoa kafara ila kwa njia ya amani kwa kuwa kafara yangu ipo kwenye kalamu na nyenzo nayotumia ni vidole vyangu. Kongole kwa kutambua tunavyoandika vitabakihai kizazi hata kizazi baada ya sisi kufa na miili yetu kuharibika. So ni dhahiri mawazo yetu yatakuwa rejeaaka mingi ijayo!
 
Duu ndugu kaimu kamishna kaka mwandamizi msaidizi Mshana Jr nimeamka saa kumi na moja kasoro dk sita nikaenda ku soso kisha nikarudi mezani...inawezekana na mimi ninatoa kafara ila kwa njia ya amani kwa kuwa kafara yangu ipo kwenye kalamu na nyenzo nayotumia ni vidole vyangu. Kongole kwa kutambua tunavyoandika vitabakihai kizazi hata kizazi baada ya sisi kufa na miili yetu kuharibika. So ni dhahiri mawazo yetu yatakuwa rejeaaka mingi ijayo!
tunazo kafara lakini ni kafara salama
Kafara za kujituma katika kazi
Kafara za nidhamu katika muda
Kafara za nidhamu katika mapato na matumizi
Kafara za kujitoa kwa ajili ya wengine
Kafara za ukweli, uwazi na uaminifu katika mahusiano
 
Umenena mkuu
tunazo kafara lakini ni kafara salama
Kafara za kujituma katika kazi
Kafara za nidhamu katika muda
Kafara za nidhamu katika mapato na matumizi
Kafara za kujitoa kwa ajili ya wengine
Kafara za ukweli, uwazi na uaminifu katika mahusiano
 
tunazo kafara lakini ni kafara salama
Kafara za kujituma katika kazi
Kafara za nidhamu katika muda
Kafara za nidhamu katika mapato na matumizi
Kafara za kujitoa kwa ajili ya wengine
Kafara za ukweli, uwazi na uaminifu katika mahusiano
Kwa muktadha huu tuseme kafara ni commitment ya jambo lolote unalofanya kwa kukusudia!
 
Mshana Jr
Mbona umenichanganya? Hapa https://www.jamiiforums.com/index.php?threads/1163936/ unasema wanyama damu yao hainuki. Lakini sasa unadai inanuka hivyo nayo hudai kisasi.

Naomba ufafanuzi Mkuu

Bazazi
Ya wanyama ni kwenye kafara zaidi... Unamtoa kafara ili ufanikiwe... Hiyo ya damu ya mtu hunuka ni kwenye ishu hizi za makusudi huko barabarani.. Lakini kama umenisoma vema kafara la binadamu ndio kafara kubwa na la mwisho... Hivyo bafo unaweza kuona nguvu ya damu ya mtu dhidi ya mnyama
 
Yatosha kusema kwamba hata ukimpenda mtu sanaaaaaa kiasi cha kumkabidhi hati miliki ya furaha na amani ya moyo wako to the extenthata akifanya mambo yasiyo na hiyana bado hujali basi umejitoa kafara kwa ajili yake in the name of penzi.
For sure...
 
Back
Top Bottom