Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,902
SIKU moja baada ya Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya, Verena Shumbusho kutamba mbele ya viongozi wa juu wa CCM Taifa kuwa wanachama 497 wa Chadema akiwamo diwani wa Kata ya Nzovwe hapa, Hezron Mwakalobo,wamejiunga na chama hicho,ameibuka na kukana madai hayo. Mbali Diwani huyo, Uongozi wa Chadema mkoani hapa umedai kuwa mwanachama aliyekihama chama hicho ambaye wanamtambua ni mmoja na kwamba kadi 497 zilizopokelewa na CCM si za wanachama wa chama hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana, Mwakalobo alikana madai yaliyotolewa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya kuwa amejiondoa katika Chadema na kwamba madai hayo yalilenga kuudanganya umma wa Watanzania. Mimi ni diwani wa Kata ya Nzovwe kupitia tiketi ya Chadema na nimechaguliwa na wananchi ambao wameniamini na kunipa nafasi ya uongozi alisema na kuongeza kuwa hana nia na wala hajafikiria kujiunga na CCM.
Kwa upande wake Katibu wa Chadema, Mkoa wa Mbeya, Eddo Makata alisema kati ya wanachama 497 waliotangazwa na CCM kuwa wamekihama chama hicho ni mmoja tu, Walen Kaminyoge ambaye ni Katibu wa Jimbo la Mbozi Mashariki ndiye aliyekihama chama hicho. Alisema kadi zilizopokelewa na Viongozi wa CCM si za wanachama wa Chadema. Hivi karibuni Kaminyoge alienda Makao Makuu Dar es Salaam na kuomba apewe kadi 100 kwa ajili ya wanachama wapya, hakuwapa wanachama na ndio hizo kawapa viongozi wa CCM alisema.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya, Verena Shumbusho, kabla ya kumkaribisha Nape kuzungumza katika mkutano huo wa hadhara, alimueleza kuwa wanachama 497 wa Chadema wamejiunga na CCM pamoja na wanafunzi 330 kutoka vyuo vikuu vilivyopo mkoani Mbeya.
Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka jana, Rais Jakaya Kikwete alipokea kadi zaidi ya 3,000 zilizodaiwa ni za wanachama wa chadema wa Jimbo la Mbeya vijijini waliojiunga CCM, hata hivyo ilikuja kudaiwa kuwa kadi hizo zilikuwa si halali.
Akizungumza jana katika viwanja vya Ruanda Nzovwe, Katibu wa Itiadi na ueneza wa CCM Taifa, Nape Nnauye aliwataka wananchi wa Mkoa wa Mbeya kujiunga na chama hicho kwa kuwa ni sawa na nyoka wa shaba, ambapo mtu akiumwa na nyoka wa kawaida akimtazama nyoka huyo atapona.
Mwananchi