Haya maswalia yanamikataba,hauwezi kukurupuka ukasema naondoa udhamini,unashitakiwa na unashindwa.Pili hela ya udhamini haitolewi siku ya tukio,labda uelewa wako mdogo mkuu
Hapa vodacom wamekosea jamani. Hata hao LINO pia wamekosea kabisa. Unaju hata kama vodacom walitishia kutowapa udhamini basi LINO wao wangeonyesha msimamo wao. Hapa inabidi tuchukue hatua zaidi ikiwa ni pamoja na kutomtambua mshindi wa hilo shindano.
Mimi nitashangaa kabisa eti huyo mlimbwende anajihusisha katika shughuli za kusaidia jamii. Ni jamii ipi hasa anilenga wakati tangu mwanzo hakuwa na huruma kama hiyo? Huyu pia yapaswa tumkatae kwa sauti kuu, tumwambie hatukutambui na pia hatutaki misaada yako. Iweje utukumbuke leo wakati ulitudharau siku tulipopatwa na majonzi makuu ya taifa letu?
Hapa ili vodacom wajisafishe kwa jamii ni lazima wafanye haya mambo yafuatayo
1.Kwanza inatakiwa kuwafukuza kazi wale wahusika wa moja kwa moja na jamii(Mkurugenzi wa mahusiano ya jamii, hapa ni Mwamvita Makamba), pia meneja mahusiano bwana Salumu mwalimu.
2.Wasitishe huduma kwa huyu mshindi wa miss Tanzania kwa kipindi chake choote atakachokuwepo katika taji lake.
3.Wafute udhamini kwa mashindano ya miss Tanzania kuanzia mwakani.
4.Waombe radhi hadharani kwa kitendo chao cha kukosa utu.
5.Wajitathimini upya mahusiano yao na jamiii kwa sasa na penye tatizo walishughulikie mara moja. Hapa waje na sura mpya kabisa kwenye safu ya uongozi na si kuwaona tena Mwamvita Makamba na Salum Mwalimu.
Vodacom chukueni hatua vinginevyo mtaangamia kibiashara. Ninyi ni kampuni achaneni na mambo ya kuwabeba watu waliosababisha muwe katika hili zogo.