Kadhia ya VODACOM na Utaifa wetu: LUNDENDA Kufungwa Kengele Rasmi
Kadhia hii ilianza kama mchezo wa kuigiza na sasa imezigubika siasa za Nchi kwa kutoka katika sura yake ya wali na kuwahusisha wanasiasa wanaoelezwa kuwa na mkono wa kibiashara katika Kampuni hii.
Binafsi nisingependelea sana suala hili kuhusishwa na wamiliki au wanahisa ambao kwa namna moja ushauri na maamuzi yao yatahitajika sasa kutanzua kadhia hii iliyopikwa na watendaji wazembe ambao wao wamewapa dhamana kusimamia mradi huu.
Tatizo kubwa kwa watendaji wengi wa Kitanzania ni udhaifu katika maamuzi ya haraka na mipango ya dharura katika matukio muhimu kwani kila siku huwa tunapanga bila kuwa na mpango wa kando (sio ule wa Kenya katika kampeni za Ukimwi) kuweka hadhari kama jambo hili litajitokeza nini mbadala wake kwa kuwa tunaamini katika nadharia kuliko nguvu za kimaumbile (Nature ambayo ni unpredictable)
Kwa Kampuni kubwa kama VODACOM ambayo inajiendesha kibishara kwa kutegemea mapato yake kwa aslimia 100 kutoka kwa individual consumer in aggressive competitive market arena walipaswa kuwa makini sana na kujihusisha na kadhia yoyote ambayo ingechafua image yao katika jamii.Kutokana na muendelezo wa mijadala mbalimbali juu ya hujuma hii ya VODACOM ambayo sauti ya kwanza ilipazwa kutoka hapa JF, kila mtanzania ana mtazamo wake.
Wapo wanaoona kabisa Kampuni hii imefanya kitendo si cha kiungwana na wengine wanaamini hakuna sababu yoyote ya kuwalaumu VODACOM.Kwa mchambuzi mzuri na mwenye taaluma ya MASOKO hasa Marketing of service, VODACOM hana pakuweka uso wake kwa kadhia hii. Hili ni doa kubwa sana kwao.
Nikiwa napanda Boti kurudi Unguja asubuhi ya leo, nimearifiwa na chanzo changu muhimu kuwa umeandaliwa mpango wa sasa ni kuhakikisha LINO agency International wanajitokeza hadharani na kuelezea mkasa mzima kwa lengo la kubainisha Tatizo na kwa nini shindano la kumska mnyange wa Vodacom lilifanyika katikati ya Simanzi kubwa iliyoligubika Taifa.
Huu ni usanii na mchezo mbaya ambao bado si uungwana.Siku zote waswahili wanasema Muungwana ni Vitendo, VODACOM simameni mbele ya watanzania na muondoe kadhia hii, kwani wanaofanya kazi hapo ni binadamu na waliokosea ni binadamu. Wahusika wawajibike kwa mustakbali wa Kampuni na majaaliwa yake katika ushindani wa soko.
(UPDATES TO FOLLOW............Kutoka PRESS Conference hiyo)
Sote tunafahamu nyie kama wadhamini wakuu mngeamua kusitisha shughuli hiyo ambayo mnaifadhili kwa zaidi ya asilimia 90, LINO hangekuwa na ujanja wala hadithi yoyote mpya zaidi ya kukubali maamuzi yenu, na huu ndio msingi unaowatia katika dhambi hii. Busara na maamzui magumu yakitumika hapa itaonyesha uzalendo na uwajibikaji wa dhati.
ADIOS