mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,663
- 18,037
Tatizo la Law School ni mchanganyiko wa factors nyingi zinazoingiliana. Si busara kuchukua sababu moja au mbili tu na kuhitimisha zipo sababu za kimfumo, mitaala ya LST na vyuo vikuu kutoendana, sababu za kijamii ikiwemo rushwa za ngono na nyinginezo, mfumo wa elimu duni kwa ujumla nchini, uwezo wa walimu, ubabe wa kielimu(superiority & negative mindset) kwa walimu na manyanyaso, sababu za kiuchumi, uhaba wa vitendea kazi kwa elimu ya vitendo, mkazo wa nadharia na kuota nafas kido mafunzo ya vitendo, maandalizi hafifu ya wanafunzi kwenye vipindi na psychological feeling kuwa chuo hicho ni vigumu kufaulu hii ni kwa walimu na wanafunzi ndicho kinachozunguka akilini lazima wafelishwe. Teaching methodology and approach haimwandai mwanafunzi na masuala ya kiutawala yakiwemo LST kusajiri wote wanaoomba bila kufanya vetting na upembuzi wa kutosha kuchukua wenye uwezo tu badal
Mapesa yamejaa sikia: Hii inapaswa kuwa 100% practical legal training na siyo 50% theoretical (semester 1) kisha 50% legal practical training na mwisho kufanya mtihani wa mwisho wa Theory Paper!! Waliofeli wamefele mtihani wa mwisho uliobase kwenye theory!!Wanafunzi someni acheni kuingiza siasa.Siasa ikiingizwa hapo matokeo yake tutapata wanasheria watakaokuja kupitisha mikataba ya kuumiza nchi kama ile ya gesi ya mtwara.walimu washikilie hapohapo hakuna cha tume uchwara wala nini.Tumeshuhudia mikataba mingi nchini hii imekuwa ya kipuuzi sana kumbe sababu ni uwezo mdogo wa wanaopata nafasi toka chuoni
Suluhisho: Semister zote mbili zihusishe field placement maeneo mbali mbali ambako sheria hufanya kazi kwa vitendo kama mahakamani, makampuni ya mawakili, ofisi za mawakili wa serikali, takukuru nk Kuwe na rotations huko na assessment ifanyikie huko na hiyo assessment ifanywe na mawakili na mahakimu walioko huko field na si walimu wa chuo ambao hawana uzoefu wowote wa vitendo wao ni nadharia tu.