Kamati ya Dkt. Mwakyembe yataka kuwe na Mtihani Maalumu kujiunga Law School

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,357
8,061
Kamati ya Dkt. Harisson Mwakyembe iliyokuwa ikitafuta chanzo cha kufeli wanafunzi wengi katika mitihani ya mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (LST) imeshauri kuundwa upya kozi za Sheria ikiwemo kuanzishwa Mtihani Maalumu wa kuingia LST kama ilivyo kwa mataifa mengine ya Afrika Mashariki.

Pia, Kamati imeshauri Serikali kulirejesha tena Baraza la Elimu ya Sheria (CLE) lililoundwa mwaka 1963 na Sheria ya Bunge na kupewa mamlaka ya kusimamia taaluma zote za sheria nchini.

Dkt. Mwakyembe amesema “Baraza likianza kazi liwe chini na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) ili kupandisha vigezo vya ufaulu wa kidato cha 4 na 6 kwa wanaotaka kusomea Sheria angalau wawe na ufaulu wa masomo 4 ikiwemo Kingereza na Kiswahili,”.

=================

Kamati ya Dk Harisson Mwakyembe iliyokuwa ikitafuta chanzo cha kufeli wanafunzi wengi katika mitihani ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo (LST), imekuja na mwelekeo mpya unaolenga kutibu tatizo hilo.

Miongoni mwa mambo ambayo kamati hiyo imependekeza ni kuanzishwa mtihani maalumu wa kuingia LST kama ilivyo katika mataifa mengine ya Afrika Mashariki.

Kamati hiyo iliyokuwa na wajumbe saba iliundwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Damas Ndumbaro Oktoba 12 baada ya malalamiko na kelele za wanafunzi na wananchi kutokana na hoja iliyoibuliwa na gazeti hili kuhusu idadi kubwa ya wanafunzi waliofeli mtihani wa mwisho kwa elimu ya vitendo LST.

Kwa ujumla ripoti imeonyesha kuna changamoto kutoka kwa wanafunzi, LST na vyuo vinavyotoa shahada ya sheria.

Akisoma muhtasari wa taarifa hiyo, Dk Mwakyembe ambaye kitaalamu ni mwanasheria na mwandishi wa habari alisema baada ya kusikiliza maoni ya wadau 141 wakiwemo viongozi wastaafu wa Serikali, majaji na watumishi wa vyuo vikuu vinavyotoa shahada ya kwanza ya sheria, sasa ni wakati muafaka wa kulifufua Baraza la Elimu ya Sheria (CLE) ambayo imepewa mamlaka ya kusimamia taaluma zote za sheria nchini.

Alisema baraza hilo lina uwezo mkubwa wa kuzitatua changamoto za muda wa shahada ya sheria, udahili wa wanafunzi kwenye vyuo vya sheria na vigezo vyake.

Alisema CLE ilianzishwa mwaka 1963 na sheria ya Bunge, lakini halina sektetarieti ndio maana kunaibuka changamoto hivi sasa katika tasnia ya sheria kwa sababu tangu kuundwa kwake halijawezeshwa kutekeleza majukumu yake.

“Ni wakati mwafaka Serikali iliundie sekretarieti, kuipa bajeti na ofisi yake, ili litekeleza majukumu yake. Suala hili halina budi kutekelezwa mapema, ili CLE ianze kazi mapema iwezekanavyo.

“Baraza likianza kazi litatakiwa kukaa chini na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), ili kupandisha vigezo vya ufaulu wa mitihani ya kidato cha sita na nne kwa wanaotaka kusomea sheria angalau wawe na ufaulu wa masomo manne ikiwemo Kingereza na Kiswahili,” alisema Dk Mwakyembe ambaye ni waziri wa zamani wa Katiba na Sheria.

Alisema uamuzi wa TCU kushusha vigezo vya ufaulu katika mitihani ya kidato cha sita kutoka alama nane (B mbili kwa masomo mawili) hadi alama nne (D mbili kwa masomo mawili), kumewezesha vijana wengi wasio na uwezo kumudu kusoma masomo ya sheria kudahiliwa.

Pia alisema kumekuwa na uwezo mdogo wa wanafunzi wanaoruhusiwa kusoma sheria baadaye kujiunga LST kumudu lugha ya kufundishia ya kiingereza, akisema tatizo hilo lina athari kubwa katika uelewa wa masomo ya kujieleza

Pia alisema CLE itakaa chini na vyuo vikuu mbalimbali ili kuhakikisha somo la stadi za lugha linakuwa sehemu muhimu ya masomo ya shahada ya kwanza ya sheria.

Mbali na hilo, Dk Mwakyembe alisema CLE itatekeleza suala la kupokea maombi ya kuingia LST kwa wahitimu ambao baada ya kumaliza shahada ya kwanza ya sheria walijiunga na kampuni za uwakili au kazi zozote za kimahakama na kampuni za uwakili.

Alisema suala la mwanafunzi bila kusoma LST hana sifa ya kuwa wakili au kuajiriwa katika utumishi wa umma, kumesababisha mafuriko LST.

“Kuhuisha mtaalaa wa Taifa wa elimu ya sheria na wa elimu ya sheria kwa vitendo, ili kuendana na wakati, kuhakikisha sharti la uwiano wa walimu na wakufunzi linazingatiwa katika vyuo husika na taasisi. Vyuo vyote vya sheria viwe na na ikama stahili iliyopitishwa CLE kwa kuzingatia piramidi ya elimu.

“Vyuo vyote vya sheria nchini vinatoa shahada ya kwanza ya sheria kwa kipindi cha miaka minne pamoja na kukaa chini na shule ya sheria, vitivo pamoja na taasisi kukubaliana kuhusu masomo ya msingi ya kufundishwa kwa mwaka wa nne wa shahada ya kwanza ya sheria,” alisema Dk Mwakyembe.

Alisema matokeo yaliyotangazwa na LST yalizua tafrani miongoni mwa wananchi huku wengine wakihisi wanafunzi wanaonewa, wanazuiliwa kwa makusudi kuwa mawakili, lakini wadau waliozungumza na kamati hiyo walifananisha mfumo wa ufaulu wa taasisi hiyo na ule wa shule za msingi na sekondari.

“Shule za msingi na sekondari mtu akifeli ndio kwaheri, lakini tofauti na vyuo vikuu ambavyo unapewa fursa ya kurudia kwa kufanya mtihani ulioshindwa. LST inabeba uzito mkubwa kwa jamii ina wajibu wa kujenga jukwaa la mawasiliano ya karibu na wananchi ikiwemo vyombo vya habari,” alisema.

Pia, alisema kamati ilipokea malalamiko ya wanafunzi wa LST waliolalamika kuwa kwa mujibu wa kununi za rufaa za taasisi hiyo inatoa fursa wanafunzi kukataa rufaa ndani ya siku 14 baada ya kutangazwa matokeo endapo hawakubaliani na mchakato huo kwa sababu ya uonevu kwenye usahishaji.

Hata hivyo, wanafunzi wanadai fursa hiyo sio chanya, ni kama kiini macho kwa sababu mtu anakataa rufaa bila kuona karatasi yake ya mtihani ilivyosahihishwa au bila kuelezwa na msahihishaji swali gani alishindwa kujibu vizuri.

“Kamati imeona msingi wa hoja ya wananfunzi, utaratibu haujakaa vizuri kwa sababu haumpi haki mlalamikaji kujua msingi wa malalamiko yake. Tunashauri LST ifanye marekebisho, ili kutoa fursa kwa mkufunzi kuanisha swali aliloshindwa mwanafunzi,” alisema. Pia Dk Mwakyembe alisema wanafunzi wa LST waliulalamika uongozi wa taasisi hiyo, kukaa kwa miezi saba na mitihani iliyofanyika bila kutoa sababu za msingi kwao. Alisema hali inawafanya wanafunzi kutojua udhaifu na ubora wao na namna ya kujipanga.

“Kamati inashauri LST iondokane na utaratibu huu usiokuwa na tija na usio wa kawaida kwa taasisi za kitaaluma na wahakikishe watahiniwa wanapata matokeo ya mitihani mapema,” alisema.

Alichokisema Dk Ndumbaro

Akizungumza baada ya kupokea ripoti hiyo, Dk Ndumbaro alisema, “tumepokea tunakwenda msituni kusoma neno kwa neno, pendekezo kwa pendekezo, changamoto kwa changamoto.”

Mnisawa alisema wamebaini kuna upungufu kutoka kwa wanafunzi, vyuo na LST, lakini Serikali ikakaa chini na kuyafanyia kazi mapendekezo na ushauri wa kamati hiyo, itapunguza changamoto zilizopo.

MWANANCHI
 
Siasa na ubinafsi wa wakubwa unaua elimu yetu. Waziri anaona kabsaa kijana wake hana uwezo analazimisha tu apitishwe.
 
HII KAMATI IMEFANYA UCHUNGUZI GANI NA IMEGUNDUA NINI..?

NA HIZO NJIA ZA UTATUZI NI KAMA NI MABODI NA MASEKRETARIETI TU YAANZISHWE...

HAKUNA MABADILIKO YA KIMTAALA AU VINGINEVYO.
 
Mimi huwa nashangaa sana jinsi serikali ya CCM inavyosiasisha elimu na kuidunisha kila kukicha. Nakumbuka wakati nasoma shule ya sekondari miaka mingi iliyopita pass mark ya kuingia kidato cha tatu ilikuwa 30%. Baadaye serikali ilishusha pass mark hadi 21% baada ya wanafunzi wengi kufeli. Hata hivyo ufaulu ulizidi kushuka na kuilazimisha serikali sikivu ya CCM kushusha tena pass mark hadi 18%. Hii nayo haikufua dafu. Ufaulu ulizidi kushuka.

Baada ya kuona njia ya kushusha pass mark imeshindwa kufua dafu, sasa wakaamua kabisa kufuta pass mark na kuruhusu hata waliofeli kuingia kidato cha tatu. Kwa hali hii, mtihani huu wa kidato cha pili umekosa maana kwa sababu ya kisiasa. Wanafunzi hawana hofu ya kufeli, wame relax bila kusoma. Sasa elimu imekuwa kama kokoro linalozoa kila aina ya uchafu unaojikusanya ndani yake.

Hawa wanafunzi wasiokuwa na uwezo wanaoswagwa tu kama mbuzi hadi kidato cha nne, udhaifu wao huonekana baada ya kufanya mtihani huu wa mwisho ambapo kila mwaka serikali imekuwa makini sana kuhakikisha mitihani inayotungwa ni rahisi sana ili kufaulisha vilaza wengi zaidi. Hata hivyo, bado ufaulu umekuwa ukishuka siku hadi siku.

Wanafunzi hawa vilaza wakimaliza kidato cha sita nako hutungiwa mitihani laini. Pamoja na urahisi wa mitihani na ulaini wa kusahihisha, hujikuta wameingia vyuo vikuu na ukilaza wao hivyo kushindwa kumudu masomo, sio tu kwenye masomo ya sheria lakini katika masomo yote. Hapa ndipo serikali sikivu ya CCM ilipoifikisha elimu ya nchi hii.
 
Vipi wale vilaza wanao pitia chocho ya certificate na diploma
 
Kamati ya Dkt. Harisson Mwakyembe iliyokuwa ikitafuta chanzo cha kufeli wanafunzi wengi katika mitihani ya mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (LST) imeshauri kuundwa upya kozi za Sheria ikiwemo kuanzishwa Mtihani Maalumu wa kuingia LST kama ilivyo kwa mataifa mengine ya Afrika Mashariki.

Pia, Kamati imeshauri Serikali kulirejesha tena Baraza la Elimu ya Sheria (CLE) lililoundwa mwaka 1963 na Sheria ya Bunge na kupewa mamlaka ya kusimamia taaluma zote za sheria nchini.

Dkt. Mwakyembe amesema “Baraza likianza kazi liwe chini na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) ili kupandisha vigezo vya ufaulu wa kidato cha 4 na 6 kwa wanaotaka kusomea Sheria angalau wawe na ufaulu wa masomo 4 ikiwemo Kingereza na Kiswahili,”.

=================

Kamati ya Dk Harisson Mwakyembe iliyokuwa ikitafuta chanzo cha kufeli wanafunzi wengi katika mitihani ya mafunzo ya uanasheria kwa vitendo (LST), imekuja na mwelekeo mpya unaolenga kutibu tatizo hilo.

Miongoni mwa mambo ambayo kamati hiyo imependekeza ni kuanzishwa mtihani maalumu wa kuingia LST kama ilivyo katika mataifa mengine ya Afrika Mashariki.

Kamati hiyo iliyokuwa na wajumbe saba iliundwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Damas Ndumbaro Oktoba 12 baada ya malalamiko na kelele za wanafunzi na wananchi kutokana na hoja iliyoibuliwa na gazeti hili kuhusu idadi kubwa ya wanafunzi waliofeli mtihani wa mwisho kwa elimu ya vitendo LST.

Kwa ujumla ripoti imeonyesha kuna changamoto kutoka kwa wanafunzi, LST na vyuo vinavyotoa shahada ya sheria.

Akisoma muhtasari wa taarifa hiyo, Dk Mwakyembe ambaye kitaalamu ni mwanasheria na mwandishi wa habari alisema baada ya kusikiliza maoni ya wadau 141 wakiwemo viongozi wastaafu wa Serikali, majaji na watumishi wa vyuo vikuu vinavyotoa shahada ya kwanza ya sheria, sasa ni wakati muafaka wa kulifufua Baraza la Elimu ya Sheria (CLE) ambayo imepewa mamlaka ya kusimamia taaluma zote za sheria nchini.

Alisema baraza hilo lina uwezo mkubwa wa kuzitatua changamoto za muda wa shahada ya sheria, udahili wa wanafunzi kwenye vyuo vya sheria na vigezo vyake.

Alisema CLE ilianzishwa mwaka 1963 na sheria ya Bunge, lakini halina sektetarieti ndio maana kunaibuka changamoto hivi sasa katika tasnia ya sheria kwa sababu tangu kuundwa kwake halijawezeshwa kutekeleza majukumu yake.

“Ni wakati mwafaka Serikali iliundie sekretarieti, kuipa bajeti na ofisi yake, ili litekeleza majukumu yake. Suala hili halina budi kutekelezwa mapema, ili CLE ianze kazi mapema iwezekanavyo.

“Baraza likianza kazi litatakiwa kukaa chini na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), ili kupandisha vigezo vya ufaulu wa mitihani ya kidato cha sita na nne kwa wanaotaka kusomea sheria angalau wawe na ufaulu wa masomo manne ikiwemo Kingereza na Kiswahili,” alisema Dk Mwakyembe ambaye ni waziri wa zamani wa Katiba na Sheria.

Alisema uamuzi wa TCU kushusha vigezo vya ufaulu katika mitihani ya kidato cha sita kutoka alama nane (B mbili kwa masomo mawili) hadi alama nne (D mbili kwa masomo mawili), kumewezesha vijana wengi wasio na uwezo kumudu kusoma masomo ya sheria kudahiliwa.

Pia alisema kumekuwa na uwezo mdogo wa wanafunzi wanaoruhusiwa kusoma sheria baadaye kujiunga LST kumudu lugha ya kufundishia ya kiingereza, akisema tatizo hilo lina athari kubwa katika uelewa wa masomo ya kujieleza

Pia alisema CLE itakaa chini na vyuo vikuu mbalimbali ili kuhakikisha somo la stadi za lugha linakuwa sehemu muhimu ya masomo ya shahada ya kwanza ya sheria.

Mbali na hilo, Dk Mwakyembe alisema CLE itatekeleza suala la kupokea maombi ya kuingia LST kwa wahitimu ambao baada ya kumaliza shahada ya kwanza ya sheria walijiunga na kampuni za uwakili au kazi zozote za kimahakama na kampuni za uwakili.

Alisema suala la mwanafunzi bila kusoma LST hana sifa ya kuwa wakili au kuajiriwa katika utumishi wa umma, kumesababisha mafuriko LST.

“Kuhuisha mtaalaa wa Taifa wa elimu ya sheria na wa elimu ya sheria kwa vitendo, ili kuendana na wakati, kuhakikisha sharti la uwiano wa walimu na wakufunzi linazingatiwa katika vyuo husika na taasisi. Vyuo vyote vya sheria viwe na na ikama stahili iliyopitishwa CLE kwa kuzingatia piramidi ya elimu.

“Vyuo vyote vya sheria nchini vinatoa shahada ya kwanza ya sheria kwa kipindi cha miaka minne pamoja na kukaa chini na shule ya sheria, vitivo pamoja na taasisi kukubaliana kuhusu masomo ya msingi ya kufundishwa kwa mwaka wa nne wa shahada ya kwanza ya sheria,” alisema Dk Mwakyembe.

Alisema matokeo yaliyotangazwa na LST yalizua tafrani miongoni mwa wananchi huku wengine wakihisi wanafunzi wanaonewa, wanazuiliwa kwa makusudi kuwa mawakili, lakini wadau waliozungumza na kamati hiyo walifananisha mfumo wa ufaulu wa taasisi hiyo na ule wa shule za msingi na sekondari.

“Shule za msingi na sekondari mtu akifeli ndio kwaheri, lakini tofauti na vyuo vikuu ambavyo unapewa fursa ya kurudia kwa kufanya mtihani ulioshindwa. LST inabeba uzito mkubwa kwa jamii ina wajibu wa kujenga jukwaa la mawasiliano ya karibu na wananchi ikiwemo vyombo vya habari,” alisema.

Pia, alisema kamati ilipokea malalamiko ya wanafunzi wa LST waliolalamika kuwa kwa mujibu wa kununi za rufaa za taasisi hiyo inatoa fursa wanafunzi kukataa rufaa ndani ya siku 14 baada ya kutangazwa matokeo endapo hawakubaliani na mchakato huo kwa sababu ya uonevu kwenye usahishaji.

Hata hivyo, wanafunzi wanadai fursa hiyo sio chanya, ni kama kiini macho kwa sababu mtu anakataa rufaa bila kuona karatasi yake ya mtihani ilivyosahihishwa au bila kuelezwa na msahihishaji swali gani alishindwa kujibu vizuri.

“Kamati imeona msingi wa hoja ya wananfunzi, utaratibu haujakaa vizuri kwa sababu haumpi haki mlalamikaji kujua msingi wa malalamiko yake. Tunashauri LST ifanye marekebisho, ili kutoa fursa kwa mkufunzi kuanisha swali aliloshindwa mwanafunzi,” alisema. Pia Dk Mwakyembe alisema wanafunzi wa LST waliulalamika uongozi wa taasisi hiyo, kukaa kwa miezi saba na mitihani iliyofanyika bila kutoa sababu za msingi kwao. Alisema hali inawafanya wanafunzi kutojua udhaifu na ubora wao na namna ya kujipanga.

“Kamati inashauri LST iondokane na utaratibu huu usiokuwa na tija na usio wa kawaida kwa taasisi za kitaaluma na wahakikishe watahiniwa wanapata matokeo ya mitihani mapema,” alisema.

Alichokisema Dk Ndumbaro

Akizungumza baada ya kupokea ripoti hiyo, Dk Ndumbaro alisema, “tumepokea tunakwenda msituni kusoma neno kwa neno, pendekezo kwa pendekezo, changamoto kwa changamoto.”

Mnisawa alisema wamebaini kuna upungufu kutoka kwa wanafunzi, vyuo na LST, lakini Serikali ikakaa chini na kuyafanyia kazi mapendekezo na ushauri wa kamati hiyo, itapunguza changamoto zilizopo.

MWANANCHI
Hivi serikali sikivu ya CCM inapoingiza siasa kwenye elimu inanufaikaje? Hii nchi ni ya kiqumer sana.
 
Back
Top Bottom