Tume ya Kuchunguza kadhia ya Law School inapaswa kuwa huru

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,223
35,149
Ni hatua njema kuwa umeonekana umuhimu wa uchunguzi kuhusiana na kadhia ya Law School of Tanzania.

Dk Mwakyembe kuongoza uchunguzi malalamiko mtihani Uanasheria

"Hata hivyo kunahitajika tume huru si tume tu kwa jina."

Ikumbukwe Dr. Mwakyembe amekuwepo sana UDSM Faculty of Law, ambao wao (eti) kwa namna ya pekee sana, wamo kwenye governing body ya LST.

IMG_20221010_064301_842.jpg

"Kesi ya ngedere kula mahindi, njiani kufikishwa kwa hakimu nyani."

Zaidi pia kauli hizi za waziri Dr. Ndumbaro muunda tume zinaongeza mashaka:

1. "Kwamba alitaka kutoa matokeo jina kwa jina ya wanafunzi wenye zero, ati kuwa akazuiwa."

Je waziri anatambua kuwa wenye matokeo yao hawana somo au hata swali walilotaarifiwa kuwa walipata ngapi?

Je waziri anajua kimsingi matokeo ya wanafunzi hawa yamegubikwa na usiri mno, jambo ambalo pia linalalamikiwa?

Je waziri anafahamu yapo matukio ya wanafunzi kusoma "pass" leo na wakasoma "fail" kesho? Kwa hiyo kumbe waziri alikuwa na zero za lini ambazo ni authentic?

Je, waziri anatambua kuwa matokeo hayo ni kiini cha mzozo huu?

Au kwa waziri makaratasi ya TLS wanapotapa tapa kwa lengo la kujinasua kwake ni 'final and terminate?' Kumbe tume ni ya nini basi?

2. "Kwamba waziri anasema LST wamekuwa wakifaulu kwa wastani wa 81%?'

Haya ni baadhi ya matokeo ya cohort zilizopita. Cohort moja haipungui wanafunzi 500.

Cohort 28 pass 169 (less than 30%)
Cohort 29 pass 54 (less than 10%)
Cohort 30 pass 133 (less than 26%)
Cohort 31 pass 28 (less than 5%)

Au ni kuwa waziri analenga kulifanyia siasa suala hili? Kwani average 81% pass anayosema ni kwa cohorts zipi?

3. Tume ya Dr. Mwakyembe haina walalamikaji au hata wawakilishi wa wanafunzi hao. LST ni mlalamikiwa. Je, hawezi kupenyeza rupia ili kujinasua na kadhia hii, kama itamsaidia?

"Waswahili wanasema penye udhia tupia rupia?"

4. LST Ina wafanyakazi takribani 51. Walimu 97 anawatoa wapi Dr. Ndumbaro? Walimu hawa wanafanya kazi zipi ikizingatiwa kwa wakati mmoja huwepo cohort 1 tu shuleni?

Kama ni nia ya kutafuta kiini cha matatizo na ufumbuzi wake wa wa kudumu, ilihitajika tume huru siyo hii ya Ndumbaro au Mwakyembe.

Pungufu ya hapo ni vyema wanafunzi (wanaolalamika) wakawa na uwakilishi kwenye tume hiyo, vinginevyo ya Jecha yanaonekana yale...eee! Yanajongea.
 
Mkuu brazaj , kwanza Nakushukuru sana kwa kuiheshimisha JF , nina hakika bila Juhudi zako za kupambana hapa JF kuhusu sarakasi za law school , hii Tume isingeundwa , Ubarikiwe sana kwa wema wako huo .

Nimeshangazwa na Waziri wa Sheria kushindwa kukujumuisha kwenye tume yake .
 
Mkuu tuko pamoja.

Hakuna anayeomba huruma au fadhila kwenye suala hili.

Kunatakikana haki hapa.
 
Mkuu brazaj , kwanza Nakushukuru sana kwa kuiheshimisha JF , nina hakika bila Juhudi zako za kupambana hapa JF kuhusu sarakasi za law school , hii Tume isingeundwa , Ubarikiwe sana kwa wema wako huo .

Nimeshangazwa na Waziri wa Sheria kushindwa kukujumuisha kwenye tume yake .
Unajuaje kama hajajumuishwa?
 
Ndumbaro nimemsikiliza jana anaonekana kabisa yupo upande wa kuwatetea wale walimu wa huko Law School, mimi naona pale kuna tatizo la msingi, ni kama vile walimu wanapewa mamlaka ya kuchagua nani afaulu, na yupi afeli.

Kauli nyingi alizotoa zilionesha wazi yuko upande wao, mfano; aliposema idadi ya wanafunzi waliofaulu kuwa ni sawa na 81%, huku waliofeli wakiwa 19%, ila kwa waliofaulu akiwa amechanganya wenye supplementary na pass, wakati wenye supplementary kiuhalisia wanatakiwa kurudia mitihani.

Pia, lengo la kuunda hiyo tume, japo wengine walionekana kulaumu uwepo wa Dr. Mwakyembe kama mwenyekiti wake, hasa kutokana na rekodi zake za matukio ya nyuma, kwangu hilo sio kubwa, kubwa ni namna Ndumbaro alivyotoa majibu ya tatizo linalolalamikiwa halafu anaunda tume, sijui hiyo tume aliunda ya nini, huu ni usanii tu, huyu kwangu alishaingilia kazi za hiyo tume aliyoiunda.

Lakini pia, inasemekana, katika wale waliofaulu ambao ni wanafunzi 26, 22 kati yao ni wafanyakazi wa taasisi za umma, hawa wamefaulishwa na taasisi nyingine ya umma, sasa najiuliza, inakuaje wale walio busy na majukumu ya kazi wafaulu kwa kiwango cha juu kuwazidi wale fresh from school, hapa naona dalili za "connection"

Hapa wanakuja wale wavivu wa kufikiri wanasema, watoto wenu hawasomi, sasa ina maana hao wafanyakazi wa umma ndio wanaosoma peke yao? kile chuo kina tatizo la msingi, nauona ukiritimba wa wazi uliopo kati ya walimu na wafanyakazi, hawa wanatakiwa kuhamishwa ili kuondoa hili tatizo.
 
Si mmewekewa mhitimu wa LST jamani, au mliofeli nanyi mlitaka uwakilishi
Umetambua kuwa yahitajika tume huru kwenye mambo yenye kubishaniwa kama haya?

"Mwamba ngoma au ngozi si huvutia upande wake?"

Zingatia umuhimu wa tume huru au yenye kuwahusisha wanaolalamika.

Kumbuka si kila mwanafunzi anaweza kuwa mlalamikajii au mwakilishi wa walalamikaji.

Kwani waliofaulu kwa mlungula, connection, upendeleo nk watamwakilisha nani? Au waliofeli na au wnanunulika?

Zingatia maana ya tume huru au yenye uwakilishi wa walalamikaji
 
Umetambua kuwa yahitajika tume huru kwenye mambo yenye kubishaniwa kama haya?

"Mwamba ngoma au ngozi si huvutia upande wake?"

Zingatia umuhimu wa tume huru au yenye kuwahusisha wanaolalamika.

Kumbuka si kila mwanafunzi anaweza kuwa mlalamikajii au mwakilishi wa walalamikaji.

Kwani waliofaulu kwa mlungula, connection, upendeleo nk watamwakilisha nani? Au waliofeli na au wnanunuloika?

Zingatia maana ya tume huru au yenye uwakilishi wa walalamikaji
Mkuu ww Sapua Sapu zako uje kwenye field acha kulalama
 
Ndumbaro nimemsikiliza jana anaonekana kabisa yupo upande wa kuwatetea wale walimu wa huko Law School, mimi naona pale kuna tatizo la msingi, ni kama vile walimu wanapewa mamlaka ya kuchagua nani afaulu, na yupi afeli.

Kauli nyingi alizotoa zilionesha wazi yuko upande wao, mfano; aliposema idadi ya wanafunzi waliofaulu kuwa ni sawa na 81%, huku waliofeli wakiwa 19%, ila kwa waliofaulu akiwa amechanganya wenye supplementary na pass, wakati wenye supplementary kiuhalisia wanatakiwa kurudia mitihani.

Pia, lengo la kuunda hiyo tume, japo wengine walionekana kulaumu uwepo wa Dr. Mwakyembe kama mwenyekiti wake, hasa kutokana na rekodi zake za matukio ya nyuma, kwangu hilo sio kubwa, kubwa ni namna Ndumbaro alivyotoa majibu ya tatizo linalolalamikiwa halafu anaunda tume, sijui hiyo tume aliunda ya nini, huu ni usanii tu, huyu kwangu alishaingilia kazi za hiyo tume aliyoiunda.

Lakini pia, inasemekana, katika wale waliofaulu ambao ni wanafunzi 26, 22 kati yao ni wafanyakazi wa taasisi za umma, hawa wamefaulishwa na taasisi nyingine ya umma, sasa najiuliza, inakuaje wale walio busy na majukumu ya kazi wafaulu kwa kiwango cha juu kuwazidi wale fresh from school, hapa naona dalili za "connection"

Hapa wanakuja wale wavivu wa kufikiri wanasema, watoto wenu hawasomi, sasa ina maana hao wafanyakazi wa umma ndio wanaosoma peke yao? kile chuo kina tatizo la msingi, nauona ukiritimba wa wazi uliopo kati ya walimu na wafanyakazi, hawa wanatakiwa kuhamishwa ili kuondoa hili tatizo.

Kama tafsiri ya Ndumbaro ni kuwa pass na supp ni kufaulu basi:

IMG_20221009_004441_910.jpg

Kumbe ni ufaulu wa 58%?

Kwa nini UDSM Faculty of Law Iko kwenye Governing Body ya LST? Kwanini siyo Tumaini, Saut nk? Kwanini isiwe rotational?

Lugha za Dr. Ndumbaro muunda tume hazina afya kwa mustakabala wa haki LST.

Suala la reshuffle kamili LST haliepukiki.
 
Tunaharibu elimu yetu na taaluma ya sheria kwa ujumla wake.

Si kila mtu anaweza kuelewa kinachoongelewa hapa. Wenye akili zao wameelewa na sasa wanaongelea umuhimu wa tume.

Wengine hata mkikaa kwa kutulia tu mkaendelea na mada zenu za Simba na Yanga kwani kuna ubaya gani ndugu?
 
Mkuu ww Sapua Sapu zako uje kwenye field acha kulalama
Mna upeo finyu sana, ajabu nawe ndie mhitimu wa hiyo Law School.

Mtu akilalamikia watuhumiwa wa panya rodi kuuwawa mikononi mwa polisi bila kufikishwa mahakamani, mnamuita naye ni panyarodi.

Huyu anayeonesha tatizo la mambo yanavyokwenda pale Law School naye unamuita ana supp, kama vile alikuonesha matokeo yake, kwa upeo wako finyu, mtu akifaulu mahali hawezi kuona tatizo lolote la mahali husika, kwako sharti apasifie tu.

Elimu uliyoipata haijakukomboa kifikra, wewe bado ni mtumwa.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom