Kada wa CHADEMA achinjwa akisherehekea ushindi

Kada wa CHADEMA achinjwa akisherehekea ushindi

ccm wamekosa hekina, roho za hao marehem zitawafanya vibaya daima.
 
Nyie ndo wapumbavu kweli kweli mnachinjana kwa sababu ya uenyekiti wa kijijii tuuu mbona title ndogo sana

Rudia tena kusoma ulichokiandika halafu jitafakari je wewe ni mtu ambaye unastahili kuitwa mtu aliye na akili timamu?
 
Mume wa mwenyekiti wa kitongoji cha Kapela CHADEMA Kata ya Igulwa Wilaya ya Bukombe Ndugu Bundala amechinjwa jana wakati wa kusherehekea ushindi wa mke wake muda wa saa mbili usiku tarehe 15/12/2014 Ushirombo Mjini.

Bi Lucia (CHADEMA) alishinda kitongoji hicho Juzi kwa Kura 435 dhidi ya 220 za Benedict (CCM) aliyekuwa mgombea wa CCM Bw Benedict amekuwa akiongoza Kitongoji hiki kwa miaka 25 mpaka juzi alipobwagwa na Bi Lucia wa CHADEMA.

CCM anahusishwa kwa kiasi kikubwa na mauaji hayo.

Taarifa zaidi zitafuata.
..si wachukue sheria mkononi
 
Damu hii haitadondoka bure itawalilia wahusika wote popote watakapokuwa Mungu tupe moyo wa kusubiri na tuone mateso yote watakayopata wahusika
 
thread yako imekaa kishabiki zaidi mtoi. nadhani ni vizuri ungekuja na habari zenye mashiko kuliko kuanza kuwanyoshea kidole mahasimu wenu kisiasa. sisi tusio na upande tuna-doubt.

Back
Top Bottom