Uchaguzi 2020 Agnesta Lambert (CHADEMA): Kete ya ushindi/mpasuko Segerea

D 2de A

Senior Member
Jun 7, 2013
183
32
Wakati joto la uchaguzi mkuu likizidi kupanda, matumbo ya waliopendekezwa na mikutano mikuu ya majimbo na kata nayo yanazidi kupata moto.

Ni siku kadhaa zimepita tangu mchakato wa kura za maoni ndani ya vyama utamatishwe kwa majina kupelekwa Kamati tendaji za wilaya (kwa madiwani) na Kamati Kuu (kwa wagombea Ubunge).

Bi Agnesta Lambert mwanamke hodari wakupangilia maneno awapo jukwaani na mtaalamu wa siasa za mtu kwa mtu (man to man) ni mmoja ya washindi wa kura za maoni akitokea jimbo la Segerea ambalo Mh. John Mrema nae alipigiwa kura na kushika nafasi ya pili nyuma ya Bi. Agnesta ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa Baraza la Wanawake Taifa (BAWACHA).

Bi. Agnesta ni Mshindi wa Tuzo maalumu iliyotolewa na CHADEMA kwenye Mkutano mkuu uliofanyika mwezi December mwaka 2019 baada yakuibuka kinara wa Kiongozi mwenye ushawishi wa siasa za field kwakufanikiwa kuwa kiongozi wa aliyefanikiwa kwa kiwango cha juu katika zoezi zima la Ujenzi wa Chama akianzia Dar Es Salaam, Kilimanjaro na baadae katika Mkoa wa Singida ambako alikuwa Kiongozi mkuu wa Operesheni ngazi ya mkoa.

Agnesta ni mwanamke maarufu miongoni mwa Viongozi wanawake wa CHADEMA kutoka na haiba yake yakusaidia watu na tabia yake ya uchezi pindi linapokuja swala zima la kukipigania chama chake.

Ni Agnesta huyu ambaye mwaka 2015 alishinda kura za maoni nafasi ya viti maalumu lakini hakupewa kipaumbele miongoni mwa wanawake walioteuliwa.

Hata hivyo haikumvunja moyo, aliendelea kukipenda na kukipigania chama kwa jasho la damu. Aidha aliendelea kujenga chama kwakuunganisha makundi ya wanawake na vijana katika jimbo la Segerea kwa lengo lakuinuana kiuchumi.

Nani wakumshinda Agnesta Lambert jimbo la Segerea? Ni Kiongozi gani wa CHADEMA aliyejenga chama au kufahamika kwa kazi zake zakuwezesha watu kiuchumi na kujenga chama kama Agnesta? Labda Diwani aliyemaliza muda wake wa kata ya Tabata ambaye nae alikuwa moto wakuotea mbali.

Ushahidi wa mazingira uko bayana kwamba Agnesta ndiye kete ya ushindi au mpasuko ndani ya CHADEMA katika jimbo la Segerea. CHADEMA kama wanataka kushinda Segerea ni sharti waheshimu maoni ya Wapiga kura waliompendekeza Agnesta mbele ya John Mrema mtu mwenye karana ya Ushehereshaji katika majukwaa ya kampeni.

Wanawake na Vijana wa Segerea wakati wote wamekuwa wakiimba jina la bi Agnesta Lambert. Wamewekeza imani yao kubwa kwa mwanamke huyu na mwanasiasa guru.

Mpinzani wa Agnesta ni Mtu thabiti jukwaani ila kwanamna Agnesta alivyojijenga ndugu Mrema hatokuwa na lugha yakuwashawishi wapiga kura wakamwelewa.

Pia ni wazi kuwa Mrema ni maarufu lakini sio maarufu katika jimbo la Segerea kama alivyo Agnesta. Kwa kazi aliyofanya kwenye zoezi la CHADEMA ni msingi kule Kilimanjaro, Dar Es Salaam na Singida ni nani asiyetamani Agnesta awe mgombea Ubunge? Ni watu wenye nia ovu ndani ya CHADEMA na wafuasi wa CCM pekee ndo ambao wasingetamani kumwona Agnesta akipeoerusha bendera ya CHADEMA.

CHADEMA ni lazima iwe na mshipa wa aibu na itende haki bila kupepesa macho. Kamati kuu ni sharti imtendee haki bi Agnesta kwakurudisha jina lake. Ni sharti waheshimu maoni ya Wapiga kura waliompendekeza kuwa mgombea wao.

Walimdhulumu ubunge wa viti maalumu mwaka 2015 sasa inatosha wasirudie tena makosa ambayo yatakugharimu chama kwakutaka kumfurahisha mtu mmoja au kikundi cha watu fulani.

Maamuzi ya Kamati Kuu ya CHADEMA kwenye jimbo la Segerea yatakuwa kielelezo na ushahidi wa haki au hila ndani yq chama. Ni uamuzi wakuje ga imani au kubomoa imani kwa majimbo mengine.

Agnesta ni kete ya ushindi kwa Segerea kama akipitishwa ila anaweza kuwa kete ya mpasuko ndani ya chama kama asipopitishwa.

Kamati kuu ya CHAMDEMA kazi kwenu, kusuka au kunyoa!

1b20ce69-accf-44e2-ad08-96c7278ebb2b.jpg
 
Mbona nasikia kahamishiwa jimbonla pembeni na Segerea na Mrema kaachwa Segerea?
 
Agnesta ndiye kete ya ushindi au mpasuko ndani ya CHADEMA katika jimbo la Segerea. CHADEMA kama wanataka kushinda Segerea
Hapa Angesta aandike maumivu. Akikwepa mtego wa kuwaachia ACT (maana kuna ushirikiano unakuja) mtego wa kumwachia Jimbo bosi wake Mrema utamnasa.
 
Wakati joto la uchaguzi mkuu likizidi kupanda, matumbo ya waliopendekezwa na mikutano mikuu ya majimbo na kata nayo yanazidi kupata moto.

Ni siku kadhaa zimepita tangu mchakato wa kura za maoni ndani ya vyama utamatishwe kwa majina kupelekwa Kamati tendaji za wilaya (kwa madiwani) na Kamati Kuu (kwa wagombea Ubunge)...

SEGEREA
Jumla ya kura 144

Agness lambert 76
John Mrema 56
Masatu Wasira 7
Gango Kidera 3
Andrew 1
Kura zilizoharibika 1

Kwa matokeo haya hata Mimi nimejiuliza MREMA KAPITAJE?

#YNWA
 
If you fail to plan, you plan to fail. Chadema must be ultra careful.
 
Hilo Jimbo acha liende CCM tu...Pole dada kwa huu uonevu.
 
Wakati joto la uchaguzi mkuu likizidi kupanda, matumbo ya waliopendekezwa na mikutano mikuu ya majimbo na kata nayo yanazidi kupata moto.

Ni siku kadhaa zimepita tangu mchakato wa kura za maoni ndani ya vyama utamatishwe kwa majina kupelekwa Kamati tendaji za wilaya (kwa madiwani) na Kamati Kuu (kwa wagombea Ubunge)...
Wajumbe wa kamat mdada amewafata hadi huku jaribun kumuelewa
 
Wakati joto la uchaguzi mkuu likizidi kupanda, matumbo ya waliopendekezwa na mikutano mikuu ya majimbo na kata nayo yanazidi kupata moto.

Ni siku kadhaa zimepita tangu mchakato wa kura za maoni ndani ya vyama utamatishwe kwa majina kupelekwa Kamati tendaji za wilaya (kwa madiwani) na Kamati Kuu (kwa wagombea Ubunge)...
kuna mtu ndani ya Chadema kanidokeza anasema ni strategy ya chama chao kuwa wote wawili (John Mrema na Agnesta Lambert) lazima waingie bungeni kwani wote ni wazuri.

so, anadai mkakati wao ni Agnesta kutinga bungeni kwa tiketi ya viti maalumu.
 
Back
Top Bottom