PreGE2025 POTOSHI Kada huyu wa CCM ameuawa na Redbrigade wa CHADEMA

PreGE2025 POTOSHI Kada huyu wa CCM ameuawa na Redbrigade wa CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Wakuu

====

Je, kuna ukweli wa taarifa hizi?
 
Tunachokijua
Madai

Julai 24, 2025 baadhi ya watumiaji wa mtandao wa Facebook walichapisha video yenye ujumbe unaosemeka "KADA WA CCM ANASTAZIA MWAMONGI AUAWA NA REDBRIGED WA CHADEMA" ikiwa na utambulisho wa grafiki ya JamiiForums.

Uhalisia wa taarifa hiyo

JamiiCheck imefuatilia na kubaini kuwa taarifa hiyo imehaririwa kupotosha uhalisia.

Taarifa halisi ya tukio hilo ilichapishwa na JamiiForums kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii Julai 22, 2025 ikiwa na grafiki inayosomeka "KADA WA CHADEMA, ANASTAZIA MWAMONGI AUAWA NA WATU WASIOJULIKANA".

Anna alikuwa kada wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye amewahi kushika nafasi ya aliwahi kuwa Mweka Hazina wa Baraza la Wanawake CHADEMA na wala siyo wa chama Cha Mapinduzi (CCM) kama taarifa potoshi inavyoonesha.

Taarifa potoshi imehariri ujumbe uliokuwepo awali kwenye grafiki halisi na kuweka maneno tofauti ambayo pia yametumia Font (mwandiko) tofauti na inayotumiwa na JamiiForums.

Taarifa hiyo potoshi imeziba pia QR code ili watu washindwe kupata taarifa kamili kupitia Jukwaa la JamiiForums.com kama ilivyo kwa Taarifa nyingine zinazochapishwa na chanzo hicho.

JamiiCheck imefuatilia kuhusu uwepo wa kikosi cha Red brigade na kubaini kuwa kikosi hiko kilifutwa mwaka 2019 kwenye marekebisho sheria ya vyama vya siasa, Sura namba 258 iliyofanyiwa Marejeo mwaka 2019 chini ya kifungu cha 8E (1)
Back
Top Bottom