Kaburi ambalo limekuwa gumzo Morogoro

Kaburi ambalo limekuwa gumzo Morogoro

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,113
Reaction score
34,953
kwa wale waliobahatika kufika katika eneo la kuwapumzisha ndugu na jamaa zetu makaburi ya KORA mjini Morogoro (barabara ya DSM ya zamani) kwa kipindi cha hivi karibuni yaani kama miezi miwili ivi watakuwa wamejionea ilo kaburi.

Ni kaburi lililopambwa kwa nakshi za gharama na kuezekwa kwa zege kama nyumba ya mfalme.
Kwa mujibu wa maelezo yatolewayo na mafundi waliopewa kufanya shughuli ya ujenzi katika eneo hilo, wamesema kaburi hilo limegharimu si chini ya shilingi milioni 25 fedha halali za kitanzania.

Pia inasemekana marehemu ni ndugu wa tajiri mmoja aliyekuwa akiishi nje ya nchi, kwahiyo vifaa vya ujenzi wa kaburi hilo vimeagizwa kutoka ughaibuni.

*sasa hii si kufuru jaman, ivi kuna maandiko gani yanasema tufanye haya?? Hata kama ni upendo au heshima kiasi gani sisi sote hatuna thamani tukishakufa na twapaswa kujitambua, lasivyo tutajiongezea dhambi za bure kwa Mwenyezi Mungu (sw)*

#picha: by Abdulatif Edmund



306090_360691237382497_928041030_n.jpg


 
hizo gharama za Milioni 25 ni uongo uliokithiri, ila pia sio vibaya kuweka kumbukumbu ya mahala alipohifadhiwa mpendwa aliyetangulia!
 
25M si kweli ni uzushi. Watajijua na kaburi lao

Ni kweli hilo kaburi linazidi hata milioni 25, ukiachia hiyo zege huko chini limewekewa madirisha ya alminium, kuna mabomba ya kuingiza maji safi ya baridi na moto, kuna mfumo wa kutoa maji taka. Wame install simu ya waya na kuna WiFi, lina AC na automatic generator pia limefungwa panel za watt 40 za sola. Kuna TV LED 3D samsung 60" , kuna decoder ya dstv PVR HD iliyolipiwa premium kwa miaka mitatu, kuna dispenser ya maji na micro wave, blender na jiko gesi. Sofa seater za leather corner, laptop mbili aina ya macbook pro, kapeti la manyoa kutoka uturuki, PS3, jacuzzi na vingine sikuweza kuvijua majina maana sijawahi kuviona.
 


*sasa hii si kufuru jaman, ivi kuna maandiko gani yanasema tufanye haya?? Hata kama ni upendo au heshima kiasi gani sisi sote hatuna thamani tukishakufa na twapaswa kujitambua, lasivyo tutajiongezea dhambi za bure kwa Mwenyezi Mungu (sw)*

ACHA VIJI WIVU VYA KIKUDA.

KWANI WAPI PAMEANDIKWA KUREMBA KABURI NI DHAMBI MBELE ZA MUNGU?
kUPAMBA KABURI WAMEVUNJA AMRI YA NGAPI YA MUNGU?
 
Ni kweli hilo kaburi linazidi hata milioni 25, ukiachia hiyo zege huko chini limewekewa madirisha ya alminium, kuna mabomba ya kuingiza maji safi ya baridi na moto, kuna mfumo wa kutoa maji taka. Wame install simu ya waya na kuna WiFi, lina AC na automatic generator pia limefungwa panel za watt 40 za sola. Kuna TV LED 3D samsung 60" , kuna decoder ya dstv PVR HD iliyolipiwa premium kwa miaka mitatu, kuna dispenser ya maji na micro wave, blender na jiko gesi. Sofa seater za leather corner, laptop mbili aina ya macbook pro, kapeti la manyoa kutoka uturuki, PS3, jacuzzi na vingine sikuweza kuvijua majina maana sijawahi kuviona.

umesahau ile carina kurahisisha usafiri kwa marehemu
 
Kilichoagizwa toka ugaibuni imamaani
1-cement
2-matofali
3-kokoto
4-nilu
3-mchanga
sababu kulingana na picha yako hayondiyo material yalitotumika.

Milidhani kunakitu cha hajabu kulingana na tittle yako.kwani kuja kujenga alipititsha mchango kama nimfuko wake wewe kinakukera nini mpaka unakwenda kuwauliza mafundi ghalama zilizotumika.kaka humiza kichwa upate njia za kutafuta pesa hachana na kifatilia mambo ya watu hayatakisaidia
 
Kitu alichoumia jamaa hapo ni huu umaskini tulio nao yeye kapiga hesabu ya millioni 25 kwenye kaburi,wakati yeye anaishi kwa chini ya dola moja kwa siku ndicho hicho kilichomwumiza kichwa ndio hivyo maisha mkuu pambana na wewe siku moja utatoka na utazikwa kaburi la sh milioni 50
 
Wakuu mwenye picha la kaburi la Bob Sambeke aliweke hapa tunataka kuliona na lake liko katika viwango gani manake ile gari iliyobeba mwili wa marehemu ni nooma
 
Invisible sir wa jf mobile hatuoni picha. Mfano kwenye thread hii sioni hiyo picha ya kaburi
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli hilo kaburi linazidi
hata milioni 25, ukiachia hiyo zege huko chini limewekewa madirisha ya
alminium, kuna mabomba ya kuingiza maji safi ya baridi na moto, kuna
mfumo wa kutoa maji taka. Wame install simu ya waya na kuna WiFi, lina
AC na automatic generator pia limefungwa panel za watt 40 za sola. Kuna
TV LED 3D samsung 60" , kuna decoder ya dstv PVR HD iliyolipiwa premium
kwa miaka mitatu, kuna dispenser ya maji na micro wave, blender na jiko
gesi. Sofa seater za leather corner, laptop mbili aina ya macbook pro,
kapeti la manyoa kutoka uturuki, PS3, jacuzzi na vingine sikuweza
kuvijua majina maana sijawahi kuviona.

nadhani hayo mabomba ya maji safi ni kwa ajili ya maji ya kunywa kwa marehemu pale akiwa anaangalia hzo tv..pia wangeweka na baa humo humo na wangemzka na mkewe awe anapga mechi marehemu wao.
 
Back
Top Bottom