Kabla ya Rais Magufuli, Tanzania haikuwa inajulikana sana. Sasa hivi inajulikana kila pembe ya Dunia

Hapa tunazungumzia mataifa ya nje yanatuonaje, sio Fundi Mchundo anafikiria nini. Huko hawana njia ya kuangalia uhalisia hivyo wanategemea makaratasi.

Amandla...
Wanajidanganya,hata ukienda Usa kuna watu kibao hawana furaha na wengine wanalala nje. Kwa hiyo makaratasi sio kipimo.
 
Propaganda ushenzi.

Nimekaa Japan miaka 5 iliyopita nipo kwenye train nimekutana na watu kama mara tano wananiuliza unatoka wapi nawaambia Tanzania wanaanza kunipa story za Serengeti.

Sasa hivi Tanzania imeanza kua notorius, inafahamika kwa ujinga badala ya kufahamika kwa mazuri kama zamani, sasa hivi ukisema unatoka Tanzania wanakuuliza kwa yule rais anayeamini uchawi. Acheni kutulisha matango. Ujinga wa jiwe haujifichi
 
Wewe kilaza kweli uchawi wa kutaka siku tatu za maombi nchi nzima na kuchangia kwaya

Japani wanasali sana ee japani ya rombo hiyo
Propaganda ushenzi.
Nimekaa Japan miaka 5 iliyopita nipo kwenye train nimekutana na watu kama mara tano wananiuliza unatoka wapi nawaambia Tanzania wanaanza kunipa story za Serengeti.
Sasa hivi Tanzania imeanza kua notorius, inafahamika kwa ujinga badala ya kufahamika kwa mazuri kama zamani, sasa hivi ukisema unatoka Tanzania wanakuuliza kwa yule rais anayeamini uchawi. Acheni kutulisha matango. Ujinga wa jiwe haujifichi
 
Ni sawa na kucheza kamali unashinda then unapitia mtaani ukitamba!!
 
Aah chakupanga kujulikana inategemea vipi Kama ni positive au negative hapo mtazamo wako upi. Maana baada ya Lisu kupigwa risasi imechangia kujulikana pia.
 
Wacha kuandika utumbo, kwahiyo enzi za mwalimu tulivyokua tunalisha Africa nzima chakula hukusikia? Au zile jitihada za ukombozi wa Africa ambazo Tz ilikua frontline huzijui? Kila kitabu na zama zake ila kusifia sana mnamharibia focus mzee wa watu! Praise and worshipers muwage na akiba ya maneno basi!
 
yaani tutajionea maajabu sana mwaka huu,yaani Nyerere haikuitambulisha Tanzania kabisa! haya wanasema tukue tuyaone
 
Haya ndiyo matatizo ya kuzaliwa kwenye mikesha ya mwenge baada ya CCM kuzaliwa mwaka 1977.

Kuna wakati Tanzania ilijulikana kama kisiwa cha Amani si barani Afrika tu bali duniani na watalii walipigana vikumbo kukitembelea kisiwa hicho

Kuna wakati mwakilishi wa Tanzania akiongea kwenye mkutano wa UN wawakilishi wa mataifa yote hupigana vikumbo kusikiliza masimamo wa Tanzania.

Kuna wakati umoja wa Afrika (OAU) kabla ya kuchukua maamuzi yoyote ulisubiri msimamo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na tamko la Rais wake.

Kuna wakati Mtanzania hakuhitaji viza kuingia nchi zilizokuwa za Jumuiya ya Madola, nchi nyingi za Ulaya na Asia, na ulipotua katika nchi hizo hukupekuliwa.

Kuna wakati nchi nyingi za Afrika ziliiona Tanzania kama mfano wa kuigwa na miji mingi mikubwa ilikuwa na barabara zilipopewa jina la Rais wa Tanzania.

Kuna wakati wapigania uhuru kutoka nchi mbali mbali ya Afrika waliweka kambi nchini Tanzania na waliitegemea Tanzania kwa misaada ya hali na mali.

Kuna wakati viongozi wa nchi zilizoendelea walipigania fursa ya kuitembelea Tanzania wakiwa tayari kutoa misaada ya kimaendeleo na kiuchumi.

Kuna wakati watoto wengi waliozaliwa ndani na nje ya Tanzania walipewa jina la aliyekuwa Kiongozi wa Tanzania kwa jinsi lilivyojulikana na lilivyoheshimika.

Kuna wakati viongozi wa mashirika ya fedha ya kimataifa katika kutimiza majukumu yao kwa nchi mbali mbali walitafuta kwanza ushauri wa uongozi wa Tanzania.

Kuna wakati kiongozi wa Tanzania alipotembelea nchi yoyote ile alitunukiwa vyeti vya heshima na wananchi wa mataifa hayo kujitokeza kwa mamilioni kumlaki.

Kuna wakati Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilikuwa na heshima kama taifa na wananchi wake waliona fahari kujitambulisha kama raia bila kusita wala kuona aibu.

Those were the days my friend...
...Those were the days, oh yes those were the days!
 
Propaganda ushenzi.

Nimekaa Japan miaka 5 iliyopita nipo kwenye train nimekutana na watu kama mara tano wananiuliza unatoka wapi nawaambia Tanzania wanaanza kunipa story za Serengeti.

Sasa hivi Tanzania imeanza kua notorius, inafahamika kwa ujinga badala ya kufahamika kwa mazuri kama zamani, sasa hivi ukisema unatoka Tanzania wanakuuliza kwa yule rais anayeamini uchawi. Acheni kutulisha matango. Ujinga wa jiwe haujifichi
Du kujifukiza na kutumia mitishamba kama dawa ni uchawi? Je unafahamu kama hizo dawa nyingi za wazungu zimechakatwa kutoka kwenye mitishamba hiyo hiyo? Jamani kupata elimu ya mkoloni isitufanye tuache baadhi ya tamaduni ambazo zilikuwa na manufaa kwa jamii zetu. Ujue kabla ya ukoloni Waafrica tulikuwa na tiba zetu za asili na watu walitibiwa wakapona , si ajabu hata wewe ukiwa mdogo umetibiwa na hiyo mitishamba. Then leo unaikashifu kuwa ni uchawi, basi kama ni hivyo China inaongoza kwa uchawi maana ndo watumiaji wazuri wa mitishamba kama tiba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom