Mchunguze kabla hujaingia nae kwenye mahusiano

Ben-adam

JF-Expert Member
Jun 2, 2023
765
1,670
Tabia mbovu mbovu za wake zetu walikuwa nazo hata kabla hutujawa nao (kama hujamfundisha wewe basi alikuwa hivyo hata kabla hajakujua)

Wakati sahihi wa kufuatilia tabia na mienendo ya binti ni mwanzo kabisa kabla hujamwambia chochote, lazima uwe mpelelezi kwanza tatizo tunaoa watu tusiowajua tunakutana nao kwenye harakati za maisha na kuona tu! Kutafuta mtu sahhi wa kuishi nae lazima iwe process ndefu.

Mchunguze mapema uepuke dhambi na laana (binti wa watu kawekeza kwako anajua utamuoa na ulimuahidi hivyo, baada ya miaka 3 unamuacha hewani, unafikiri nini kinatokea?)

Nawashauri vijana wenzangu ambao bado hamjaoa muwe wapelelezi wazuri kabla ya kufanya maamuzi.

DHIBITI HISIA, TUMIA AKILI. #Uliza bei kabla hujala.
Ben-adam , Mwalimu Wa Zamu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom