Huko barabarani wataumizwa bure wananchi wasio na hatia yeyote kwaajili ya uongo wa wana siasa!
Viongozi wa chadema hawana elimu
Huko barabarani wataumizwa bure wananchi wasio na hatia yeyote kwaajili ya uongo wa wana siasa!
Sababu ya kuiomba hiyo video ni kuondoa unafiki maana with wengine wamesha anza kuamini Ukawa hawakukubali bunge liendelee hadi October 4!Ruttashobolwa;
Hapa ishu siyo kama mimi nataka kuandamana au vipi bali umeleta hoja na tunajadiliana. Ndiyo maana nasema sidhani kama kuna side yoyote tunaoweza kuiamini si Ikulu/CCM, TCD au UKAWA. Lakini kwa kutumia akili yako na mtiririko wa mambo jinsi yanavyokwenda you can simply make decisions on this issue of Katiba! Ndiyo maana nikasema upande utakaoheshimu maoni ya wananchi yaliyokusanywa kitaalamu na kwa mujibu wa sheria na kuwa compresssed kwa mtindo wa Rasimu ya pili ya Katiba chini ya Tume ya Rais iliyoongozwa na Jaji Warioba kiukweli ndiyo upande unaopaswa kuaminiwa na kupewa support na wananchi kwa namna yoyote ile iwe kwa kuandamana au kwa kupaza tu sauti zetu na kwa njia zingine zozote zinazokubalika!!.
BTW, unajicontradict sana kwa namna ulivyoleta uzi wako na na namna unavyo react toka katika mawazo na comments za wachangiaji mbalimbali. Hebu niambie hiyo video ya mazungumzo unayoiomba ni ya nini sasa kama una uhakika kuwa walikubali BMK liendelee hadi tarehe 4/10? Au unalazimisha tu tukuamini wewe na wakati huohuo unaomba video kuonesha kuwa hata wewe hujui lolote kuhusu hayo mazungumzo ila tu kwa sababu Cheyo na TCD amegusa hisia zenu na mnachokitaka na wakati huohuo UKAWA wakatokea kupingana naye? Narudia tena kukuhakikishia kuwa;
Hakuna video au uthibibitisho wowote halisi wa mazungumzo unaoweza kutolewa na Ikulu/CCM yenu,wewe au TCD kwa maana ya Mwenyekiti wake Bwana Mapesa Cheyo kwa sababu moja tu hakuna nia thabiti ya kuukwamua mchakato wa kuandika katiba hii bali kilicho mbele zaidi ya IKULU/CCM ni maslahi ya kisiasa zaidi ambayo yamo katika mchakato huu, kosa dogo tu unamalizwa na opponent kisiasa wako asubuhi tu,wewe na CCM yako mnalijua hili,that's why you are fighting day and night.........but I am very sorry to tell you that you are losing the battle!.
Na rafiki,nikuambie tu huu mchezo wa kisiasa unaochezwa na Ikulu/CCM kwa msaada wa John Cheyo,Mrema na Fahm Dovutwa Nassoro kwa kivuli cha TCD kila mwenye akili timamu ameshaung'amua!!.. Na I am sory too kukuambia kuwa hata wewe unachokifanya katika social networks kama hii ni kama kuendelea kukolezea ulaghai wa CCM tu. Na kama si mchezo wa kisiasa na kweli hayo mazungumzo chini ya mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi yalikuwa na lengo jema, kwa nini yasingekuwa ya wazi na vyombo vya habari kuruhusiwa kuhudhuria na kuripoti kitakachojiri kuliko ilivyo sasa ambapo tuna lazimishwa kuamini au kutoamini chochote miongoni mwa makundi hasimu ya kisiasa siyoaminiana ya CCM/Ikulu vs TCD vs UKAWA?
Si katiba ni mali ya wananchi, sasa kwa nini mambo yawekwe katika hali ya kifichoficho na kipropaganda zaidi? Kwa sbb hata wewe unachokifanya ni kuendeleza propaganda zilezile chafu za CCM!!..But the fact remains that; ishu hii ya katiba mpya ndiyo itakayoinyonga na kuitupilia mbali CCM tunapoelekea katika uchaguzi wa seriakali za mitaa na uchaguzi mkuu 2015, kama unabisha tunza huu uzi halafu tukumbushane mwaka kesho kuanzia mwezi november!!
Ndiyo maana nakuuliza mnapata wapi ujasiri wa kutuombea Ikulu iweke mazungumzo hayo hadharani halafu yaaminike?
Lakini ukae ukijua UKAWA wana imani kabisa na Ikulu ndio maana walikubali mazungumzo nao!
Ndio maana nasema mkanda uwekwe wazi!
Viongozi wa Ukawa wamejaa ubinafsi sana!
Mimi naweza kubishana na Great Thinker na siyo mtu wa Face Book!Wanasema ukiwa muongo jifunze kutunza kumbukumbu. Nyie watu ni wanafiki sana. Unasema vyama vya siasa wanachama wake hawazidi 10m hivyo mamlaka ya viongozi wa TCD kuwasemea watanzania 45m wameyatoa wapi???
Hivi nyie mna ugongwa gani? Make majibu yenu hayaeleweki hata mnataka ni. Mlizaliwa kupinga tu???
Hivi nikuulize swali. Hayo maoni ya warioba ya watu elf170ndiyo umeona ni maoni ya watanzania wote kuliko maafikiano ya viongozi wa TCD wanao ongoza watanzania 10m???
Nyie ni wapumbavu sana make hampendi kuelezwa ukweli. Mmebaki na kazi moja tu ya kumsuribia jirani kafanya nini ili mmpingie tu.
Sababu ya kuiomba hiyo video ni kuondoa unafiki maana with wengine wamesha anza kuamini Ukawa hawakukubali bunge liendelee hadi October 4!
Na swala la maongezi kuwa ya kificho liliombwa na viongozi wa UKAWA waulize!
Ina maana na wewe huamini kama walikubali katiba iliyopo ifanyiwe marekebisho?huamini kuwa walikubali swala la katiba litaendelea baada ya uchaguzi?
Swala la kusema sijui maoni ya wananchi yanatupwa ni inayo jadiliwa si rasimu ya warioba huu ni uongo labda mtwambie zile sura. mbili walizojadili UKAWA zilikuwa kwenye rasimu gani?
Kumbuka bunge limepewa mamlaka ya kubadilisha,kuongeza,kurekebisha chochote kwenye Rasimu na sheria!
Basi tunaweza kukubaliana kuwa hakuna mwenye mamlaka ya kusitisha bunge! Ni vyema tukasubiri hadi October 4 na baadae mchakato wakurekebisha katiba iliyopo!
Kuhusu kuindoa CCM madarakani hizo ni ndoto kabisa na subiri uone dalili za ndoto kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa!