Jitahidi Kaka ,natamani nikusimulie mengi ila haitosaidia ,pambana uchomoke ,mwenzio nilichelewa kufanya hayo ,Sasa nipo nilichobakiza ni ajira tu ila watoto nilishaambiwa si wangu na Sasa wao wamenikana Mimi si baba yao .
Nishakaa jela sikumuona mwanangu Wala huyo mwanamke bad enough natoka Mali zikapigwa mgao ,kikubwa akapewa yeye kidogo ,nikapewa Mimi .
Haikuwa rahisi kukubali ila ujasiri na kukubali kuanza upya Sasa ninaishi Kaka ,ajira naendelea ,maisha na kidogo nilichoachiwa nakizingatia ili kesho isiwe ngumu kwangu .
Ila sio kwamba siamini kwenye mahusiano ,hapana bado naaamini wapo wadada wanajua nini maana ya ndoa na mahusiano hivyo bado najua ipo siku nitampata wa kuendana naye ,though sio Sasa maana nitakuwa muongo kusema simpendi tena mama watoto .
Bado nampenda yule dada na ninaamini alipitiwa ,Kuna muda narudisha muda nyuma na kuamini ipo siku atarudi japo ameshaolewa tena ila kwenye uhalisia ni ngumu .
Nilijaribu kuomba suluhu japo anisamehe anipe hata mtoto mmoja ila haikuwezekana zaidi ya kutishiwa kupelekwa polisi au kushitakiwa ofisini kwangu nikawa mpole .
Bro unapitia magumu ila bado hayajawa kiasi Cha kukupa stress hivyo yasolve mapema kabla hayajawa Kama yangu ,inauma ,uanaume ni kazi ,ni mateso ni tabu ila tumeumbwa kuvumilia wacha tuvumilie na maisha yawndelee.
Stay strong ,anza Sasa kujipanga ,usimdhuru Wala kuwaza kumdhuru utaiharibu kesho yako