Kabla na baada ya ndoa

Kabla na baada ya ndoa

Mkataba wa hisia huwa haudumu, ni utapeli..!
Natafuta ajira alishatufundisha sana hili jambo. Kwamba Mwanamke kitu pekee anachowekeza kwako ni hisia tu amazo hubadilika kulingana na hali, wakati, na mazingira na ndio maana hawaoni hatari kuachana.

Wakati mwanaume umewekeza kwake muda, pesa, uchumi, mipango, familia.

Hawa watu hamwezi kuwa sinia moja
 
Nipo kwenye ndoa huu mwaka wa sita na nilioa single mother ila kwa yanayoendelea najikuta nipo kwenye wakati mgumu sana wa kimaamuzi juu ya mustakabari wa ndoa yangu

KABLA YA NDOA
Mwanamke alikuwa ananielewa sana, ananisikiliza, ananiheshimu, ni mwepesi kusema samahani

Mwepesi sana kutoka nae out na ni kama alikuwa anaenjoy kiasi flani

Kitandani hakuwa haba, kujituma kama kote mpaka nakuwa nammiss kila nikiwa mbali nae, tulikuwa na uwezo kugegedana popote pale tunapojihisi tupo peke etu, iwe ofisini, garini, dkn, jikoni, sebuleni fainali chumbani ndiyo balaa zito

Nazimiss sana nyakati zile

BAADA YA NDOA
Mwanzo haukuwa mbaya sana wala mzuri sana ila ni vile unajipa moyo kwamba yanapita tu

Kusema samahani ni mpaka tuwe tunakaribia kuachana

Nikimuomba tutoke out haoneshi kufurahia tena kama zamani lakini pia hata akikubali mpo maeneo lakini akili yake ipo nyumbani, ni kama anatoka kuniridhisha mimi na haachi kulalamika kwamba pesa inaharibika, wakati mara nyingi anasisitiza tutume hela kwa ndugu zake na tunatuma na huwa halalamiki kwamba tunaharibu pesa

Penzi ni kama nimesusiwa(D2) nikimuuliza mbona hunyumbuliki au kujituma kama enzi zile anasema hana mazoezi. Na mimi nikimpotezea anaanza kulalamika eti sina hisia nae. Kiufupi anataka mie nifanye kila kitu(inaboa). Kiukweli kuna muda nakuwa na hamu sana ila kumfikia ndiyo nashindwa mpk natamani kujichukulia sheria mkononi

Nimeshaongea nae sana kuhusu tofauti zetu ila hakuna linalobadilika moja kwa moja. Kwa sasa namezea japo naumia ndani kwa ndani

Kitu kingine nimekuja kujua kwamba ni mkali sana hasa kwa watoto kiasi mpaka najisikia vibaya. Kwake yeye hakuna mtu anayejua zaidi yake.

Najikuta mpweke zaidi kuliko nilivyokuwa mpweke kabla sijaoa. Na kabla sijaoa vita yangu kubwa ilikuwa kujiweka vizuri kiuchumi ila baada ya ndoa nahisi nimejiongezea vita nyingine tena kubwa kuliko ile niliyokuwa napigana nayo kwa kipindi kirefu

Nikisema bado nampenda nitakuwa ninaudanganya moyo wangu unless naendelea tu kuishi nae kwa sababu ya watoto na heshima niliyojijengea kwa jamii ila nawaza mpaka lini nitaishi maisha haya

Taasisi ya ndoa ni ya wachache sisi wengine tumedandia tu na ndiyo zinatutafuna. NACHOMOKAJE HAPA? View attachment 3156830
Natamani hii picha ya AI iwe ndiyo picha yako halisi, maana imesadifu stori yako😆😆.

Ijapo haujatupa stori ya chanzo cha mahusiano yenu kimapenzi, lakini nahisi ulitegeshewa ili kubebeshwa majukumu!

Wenzetu hawa wana akili sana, unaigiziwa hadi unajaa, jamani nyie!

Kwetu wadau ukitufikishia ishu za namna hiyo usitegemee 'negatives' toka kwetu mazee, haturuhusiwi!

Kilichobakia mbele yako ni kufanya maamuzi binafsi kama yale uliyofanya 'kuvuta jiko'!

Wee fikiria mwanamke alikuwa ni single mom, af'ukajishitukia upo naye kwenye ndoa, wadhanini ishu ndogo hiyo ya kuishauri kichwa kichwa?
 
Back
Top Bottom