Kabla hujamuoa mfanyie majaribio yafuatayo

Kabla hujamuoa mfanyie majaribio yafuatayo

Raymanu KE

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2022
Posts
10,637
Reaction score
19,990
Kwa wale mabachela ambao bado hamjao njooni niwasanue kitu maybe kitakuja kuwafaa kwenye kuchagua mwanamke wa kuishi naye ndani Kama mkeo.

Unapoanza mahusiano na mwanamke lazima ufanye vitu viwili vinavyoitwa " Risk taking" na " feasibility test". Feasibility testing Ni kufanya taathmini kwa kutumia mbinu mbali mbali kwa lengo la kutaka kujua Kama Kweli huyu mwanamke ataweza kukidhi vigezo vinavyohitajika.

Mwanaume unatakiwa udate na wanawake kadhaa( minimum 5) angalau uweze kuwafanyia tests mbali mbali ili uchague mwanamke mmoja wa kuishi naye Kama mkeo( Kama atakuwa ametusua tests/mitihani zako zote). Wiki Moja tu inatosha kumtest mchumba wako kwa hiyo mpe mwaliko wa wiki Moja Kisha Anza kumfanyia tests zifuatazo;
[emoji116][emoji116][emoji116]

1. Mpe nguo zako chafua afu chukua kiti ukae pembeni uone jinsi atavyofua.
Akichukua shati, fulana na suruali zako Kisha akazichanganya kwenye besheni Moja Basi hiyo Ni ishara tosha kwamba huyo mwanamke wako Ni mchafu wa kiwango Cha flyover.

Atakuwa amekiuka kanuni za ufuaji. Mtu anapofua nguo za mwanaume/ mume wake anatakiwa afue Kama ifuatavyo;

Aanze na shati,vests fulana,suruali,jampers au koti Kisha socks afu amalize na viatu.Hii ndo itifaki inayozingatiwa kwenye usafi wa mavazi tofauti na hapo Basi huo ni uchafu. Kwa hyo mwanamke wako akishindwa kuzingatia hyo itifaki Basi piga chini haraka huyo no mchafu.

2. Chukua noti kadhaa za pesa Kisha uzikunje na uziweke kwenye mojawapo ya suruali zako kimaksudi
Kisha mpe huyo mchumba wako afue.Usimwambie Kama Kuna uwezakano wa pesa kuwa kwenye nguo yako ila we kausha tu afu nenda zako kijiweni ukapige stori na Wana. Kisha Rudi ndani baada ya muda mfupi afu ukae kimya tu au umpongeze kwa kazi nzuri aliyofanya ya kukufulia.

Hapo Sasa mwanamke mwenyewe atamua aidha kukupa zile pesa alizopata kwenye nguo yako wakati anafua ama akaushe tu ajifanye hakuzikuta ila wewe mwenyewe unajua lengo lako. Akikupa Basi shukuru maana huyo atakuwa mwaminifu ila akinyamazia Basi piga chini haraka maana hapo utakuwa umefuga mwizi atakuja kukuibia Mali zako [emoji23]

3. Usafi wa ndani kwa ujumla
Sasa Hapa Ni hivi,kabla huyo mchumba wako hajafika kwako kwa ajili ya mwaliko uliompa,hebu mess up Kila kitu,Yaani tawanya mashuka ya kitanda chako Ana ikiwezekana tandika shuka chafu afu chukua shuka Safi uiweke pembeni.Nenda sebuleni vuruga Kila kitu. Fungua kabati lako afu changanya sahani na vikombe.

Alifika ndani we kaushia tu Wala usimwambie chochote ajiongeze mwenyewe maana tayari atakuwa ameshaona mess iliyopo. Akishindwa kujiongeza eti anajifanya hajaona upuuzi uliopo Basi huyo piga chini Mara Moja coz huyo atakuja kukuabisha mbele za wageni wako siku Moja.Fukuza tafuta mwingine.

4. Mapishi yake jiko
Akija kwako lazima atapika mule.Mambo ya kula hotelini yatakuwa ndio baaasi. Wahi dukani kwa mangi nunua unga wa ngano mixer mafuta ya mboga( oil) Kisha mlete umwambie umetamani kula chapati laini kbsa. Akikuletea mezani vitu vya ajabu ajanu( chapati zilizokauka afu hazina shape ya kueleweka) huyo piga chini Mara Moja arudi kwao mamake amfundishe kupika.

5. Mapokezi yake ukirudi kazini.
Rudi nyumbani jioni kbsa afu jifanye umechoka.Timba na mizigo mizito( tuseme shopping ya ndani) afu mbishie mlangoni then angalia reaction yake. Mwanamke anayejielewa akiona situation Kama hii ataacha Kila kitu akimbie kuja kukulaki mlango na kukupa pole za kazini na kukusaidia kuweka ndani mizigo.

Kisha akuandalie maji ya vugu vugu Kisha akupelekee bafuni na towel lako.Kisha akutengee nguo za kubadilishia. Tofauti na hivyo Basi huyo no mzembe piga chini haraka.

Vijana wa kiume ambao ndo kwanza mpo kwenye harakati za kutafuta wanawake wa kuishi nao Kama mke ebu chukueni hizi mbinu mzifanyie kazi afu mtakuja kunishukuru baadae. Ngoja nipige Kenya Cane Moja nisuuze Koo kwanza Kisha nirudi kusoma comments za wanazengo.
 
Duuh unatafuta mke au housegirl? By the way kumbe ndiyo maana siku hizi mnalalamika sana kwamba "wanawake kabla hamjawaoa wanakuwa wife material ila wakishaingia kwenye ndoa tu wanabadilika na kuanza kuonesha makucha yao" kumbe ninyi wenyewe ndiyo mnataka wanawake wawaigizie maisha?
 
𝐀𝐢𝐬𝐞𝐞𝐞𝐞 𝐧𝐚𝐬𝐞𝐦𝐚 𝐡𝐢𝐯𝐢 𝐮𝐩𝐮𝐮𝐳𝐢 𝐡𝐮𝐨 𝐤𝐢𝐣𝐚𝐧𝐚 𝐲𝐞𝐲𝐨𝐭𝐞 𝐚𝐬𝐢𝐣𝐚𝐫𝐢𝐛𝐮 𝐦𝐚𝐚𝐧𝐚 𝐡𝐚𝐢𝐭𝐚 𝐤𝐮𝐬𝐚𝐢𝐝𝐢 𝐜𝐡𝐨𝐜𝐡𝐨𝐭𝐞 𝐳𝐚𝐢𝐝𝐢 𝐭𝐮 𝐲𝐚 𝐤𝐮𝐦𝐜𝐡𝐞𝐳𝐞𝐚 𝐦𝐭𝐨𝐭𝐨 𝐰𝐚 𝐰𝐚𝐭𝐮 𝐤𝐢𝐬𝐡𝐚 𝐮𝐦𝐮𝐚𝐜𝐡𝐞,
𝐍𝐝𝐢𝐨 𝐦𝐚𝐚𝐧𝐚 𝐦𝐢𝐚𝐤𝐚 𝐲𝐚 𝐬𝐢𝐤𝐮 𝐡𝐢𝐳𝐢 𝐡𝐚𝐭𝐮𝐩𝐚𝐭𝐢 𝐦𝐚𝐛𝐢𝐧𝐭𝐢 𝐩𝐮𝐫𝐞 𝐤𝐰𝐚 𝐬𝐚𝐛𝐚𝐛𝐮 𝐰𝐚𝐧𝐚𝐤𝐮𝐰𝐚 𝐰𝐚𝐬𝐡𝐚𝐭𝐮𝐦𝐢𝐤𝐢𝐚 𝐦𝐚𝐢𝐬𝐡𝐚 𝐲𝐚 𝐧𝐝𝐨𝐚 𝐤𝐚𝐛𝐥𝐚 𝐲𝐚 𝐤𝐮𝐢𝐧𝐠𝐢𝐚 𝐧𝐝𝐨𝐚𝐧𝐢,
 
Back
Top Bottom