Kabla hujaamua kupanga au kununua nyumba ya kuishi ni muhimu kukusanya taarifa kwanza kuhusu nyumba au mtaa wenyewe

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,907
6,700
Anasimulia Bwana Joakim

Hiyo siku nilirudi nyumbani nikiwa hoi kwa uchovu, hivyo baada ya kula na kuoga moja kwa moja nikajiingiza chumbani kulala.

Lakini ilipofika alfajiri nikajikuta nimeamkia sakafuni sebuleni tena nikiwa na begi, buti na mavazi yaleyale kama niliyotoka nayo jana.

Nikapigwa na mshangao mkubwa huku taratibu nikiwa najiinua kutoka pale nilipo.

Mara ghafla mdogo wangu akatokea kutoka chumbani kwake.

Nikamuuliza " jana mlikaa sebuleni hadi saa ngapi?"

Akajibu " Mpaka ilivyoisha revenge, saa nne usiku"

Nikamuuliza " sasa hapa nimekuja saa ngapi wakati nililala mapema sana kabla yenu?"

Akajibu " Mimi mwenyewe nashangaa kwasababu hata nguo zako ulibadilisha na begi lako uliingia nalo ndani "

Baada ya kusikia hivyo, nikaanza kuogopa huku kichwani nikijisemea kuwa "hii sasa imezidi "

Nikasimama taratibu na kuelekea chumbani kwangu nikiwa na muonekano kama vile ndio narudi kazini.

Sasa ile naingia tu ndani, nikajiona Mimi nimejilaza kwenye kitanda kilekile nilicholala Mimi na huyo mimi ananishangaa Mimi.

Aisee nilitoka nduki kuelekea nje ya nyumba huku nikipiga kelele za kuomba msaada kwa majirani.

Ndugu Joakim anasema, hiyo ndio ilikuwa siku ya mwisho kwa Mimi kuishi nyumba ile.

Sikutaka kuchukua chochote kilicho changu na hata nguo nilizotoka nazo nilizichoma moto.

Ni nyumba iliyokuwa na maajabu kiasi kwamba hakuna mpangaji aliyeweza kuvumilia.

Yani hata mwenye nyumba mwenyewe alishindwa kuishi kwenye nyumba yake mwenyewe.
 
rope.jpg
 
Huwezi kujua kuwa Dunia Ina mambo mpaka likukute jambo. Kuna mambo ukihadithiwa unaweza kuhisi ni mambo ya kufikirika lakini wahenga wanasema kuishi kwingi ni kuona mengi.

Niliwahi kupanga nyumba moja nyakati fulani, siku moja usiku nimelala na nimezima taa lakini naamka kati kati ya Usiku naamka nakuta taa inawaka hali ya kuwa nilikwisha izima, nikasema pengine nilisahau kuzima, nikazima tena, narudi kitandani inawaka nikizima inawashwa, nikajua leo Nina wageni wasioonekana na wameamua kunichezea akili. Nikaiacha nikaenda zangu kulala.

DUNIA NI ZAIDI YA UIJUAVYO....
 
Ndiyo maana mimi huwa napenda sana nyumba yangu niijenge mwenyewe from the scratch, majumba ya kununua ni mtihani sana maana watu wanafanya makafara na mazindiko ya ajabu ajabu... Kuna nyumba jamaa alinunua na wakati mafundi wanaivunja kubadili muundo wake wa zamani wakakuta mifupa ya mtoto aliyezikwa humo ndani.
 
Back
Top Bottom