Kabati la nguo la Mmiliki wa Facebook

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,870
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg


Nilikuwa napita huku na huko katika mitandao,hatimaye nikakutana na maisha ya uvaaji wa nguo za mmiliki wa mtandao wa facebook MARK ZUCKEBERG.Huyu jamaa ametoa picha ya kabati la nguo zake,na kuelezea kuwa ndio kabati la nguo zake za kila siku azivaazo

Mark anasema ili asipoteze akili nyingi kwa mkewe na kwake juu ya nini avae na ni nmana gani anatakiwa kuvaa,ameamua kuwa na nguo za aina moja katika kabati yake na kutoa "tender"(zabuni) kwa kampuni kumtengenezea aina hiyo ya nguo,

pia ameamua kununua nyumba iliyo karibu kabisa na Makao Makuu ya Facebook ili asiwe anatumia usafiri wa aina yoyote zaidi ya kutembea toka nyumbani mpaka ofisini.

Ukifuatilia hata katika makongamano yake na mihadhara ya kitaaluma ktk vyuo na maeneo mbalimbali unaweza dhania kuwa Mark huwa habadilishi nguo,kumbe ana kabati lililojaa nguo za aina moja
 
Nimekubali yote uliyosema, zaidi anayo pia suti moja nyeusi, tai ya kuvalia hiyo suti na pia shati jeupe la kuvalia hiyo suti nyeusi ... baasiiii
 
Ni kweli. Kuna muda mwingi na nguvu kubwa inapotea katika kuchagua nguo za kuvaa.
 
Hii idea nilishawahi ionaa kwenye movie flani ya zamani sana inaitwa FLY kuna professor humo ndani anavaa suti na viatu vyote vya rangi sawa reason yake nae ilikua hiyo hiyo kwamba asiangaike asubui kuwaza avae nini.I think thats where Mark got the idea
 
Hii idea nilishawahi ionaa kwenye movie flani ya zamani sana inaitwa FLY kuna professor humo ndani anavaa suti na viatu vyote vya rangi sawa reason yake nae ilikua hiyo hiyo kwamba asiangaike asubui kuwaza avae nini.I think thats where Mark got the idea
na Pengine kamuiga Mr.Warren Buffet.....Huyu mzee lifestyle yake ni ya kipekee sana..
 
Back
Top Bottom