Kabati la Mr | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kabati la Mr

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Nasra82, Nov 22, 2010.

 1. N

  Nasra82 Member

  #1
  Nov 22, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Salaam aleykum!
  Wapendwa naomba mnijuze, mme wangu kila akisafiri anafunga kabati lake la nguo hii inaashiria nn? kipindi cha nyuma nilikuwa nampangia nguo zake baada ya kizinyoosha nikakuta kanga na haikuwa ya kwangu, nilimuuliza sikupata jibu la kueleweka, siku iliyofuata akafunga kabisa na kuondoka na funguo kw bahati mbaya nilikuwa sijamaliza kunyoosha nguo zote hivo nilipomaliza nafungua kabati limefungwa nikaweka nguo ktk kabati yangu mpk jioni alivorudi nikampatia nguo zake, j2 nilikuwa nafanya usafi wa nguo zake nimeshazinyoosha naenda kufungua kabati lake nakuta kafunga na hayupo nchini na atakaa huko km 1 month hivi jamani nimuelewe vp au ni kawaida kwa wanaume kufunga makabati? au anaficha nn? hii inanipa mawazo naona mnieleweshe
   
 2. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #2
  Nov 22, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hii mpya! wataalam watujuze hapa
   
 3. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #3
  Nov 22, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Ulishachakachuliwa Nasra. Kuwa tu mpole. Lakini katika maelezo yako unaonyesha hujamwuliza yeye mwenyewe binafsi kwanini anafunga kabati yawezakana atakuwa na jibu sahihi kwako. alafu sijui wengine mnakuwa na ndoa za namna gani hizo za kila mtu na chake hadi makabati jamani kwa kweli ni kazi.
   
 4. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #4
  Nov 22, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Hii mpya ndoa zina mambo hebu jaribu kukaa nae umuulize kwa nini anafunga kabati lake wakati wewe na yeye tayari ni kitu kimoja.
  usijekuta mmeo anatunza mkono wa albino ndani ya kabati
   
 5. M

  MONTESQUIEU JF-Expert Member

  #5
  Nov 22, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 847
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hapendi kuchakachuliwa
   
 6. R

  Renegade JF-Expert Member

  #6
  Nov 22, 2010
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 3,761
  Likes Received: 1,062
  Trophy Points: 280
  mhhhhhhhh, HAPA NI SIRI NDANI YA KABATI. Mngoje akirudi kaa naye chini umuulize kwanini akuamini? Wakati wewe ndiye mkewe? Akirespond positive muombe funguo, Na kama atarespond negative basi jua kuwa hapo anasiri kubwa ambayo hataki wewe ujue!!
   
 7. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #7
  Nov 22, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  wala usipate taabu unajua wengine wanazaliwa na viuchawi vyao toka utoto we kuwa mpole fatilia taratibu utajua tu kuna siku atajisahau hata kwa dakika utamchambua huko kweny kabati na kupata majibu na maswali yako yaanzie hapo lakini ukianza na maneno bwatu tegemea ugomvi na kubakia kwenye giza halafu hata kama ana siri huko kabatini anaweza hamishia sehemu nyingine unapotaka kufanikiwa kwenye jambo lolote lazima uwe malengo yako yakiambatana na uvumilivu kwenye njia utazopita mpaka mafanikio
   
 8. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #8
  Nov 22, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,001
  Trophy Points: 280
  kaambiwa wanawake hawana siri, wakiona tu watasema

  Dada Nasra umefungiwa kabati unawauliza wana JF kabla ya kumuuliza mwenzio kwanza, ukiona Mkono wa Albino (Kama alivyosema FL1) si utakuja kutoa siri tena humu JF?
   
 9. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #9
  Nov 22, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  kuna tunguli humo hataki uzijue
   
 10. N

  Nasra82 Member

  #10
  Nov 22, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani mara ya mwanzo nilimuuliza hakuwa na jibu lolote na msingi na naweza sema hakujibu kabisa, na kwakweli cna tabia ya kuchunguza sana kabati yake yaani mpk ninapomsafishia nguo ndio nakumbuka kuzirudisha kabatini! nimejaribu kumuuliza sshv km mlivoshauri kanijibu aaah kakosea tu na hana uhakika km kafunga, lakn ukweli ni kuwa mr yupo makini sana hivo hajakosea ila kipo alichokuwanacho ambacho mie sikijui!
   
 11. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #11
  Nov 22, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Detective anza kampuni yako ya investigation ............
  usimwachie mpaka akueleze nini kiko huko kabatini....
  au mpaka uone mwenyewe.......
   
 12. chobu

  chobu JF-Expert Member

  #12
  Nov 22, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Bi nasra pole sana! Hebu akirudi safari yake mpokee vizuri kwa bashasha baadaye akipumzika jaribu kumuuliza kwa lugha laini: Kulikoni mwenzangu mbona unafunga kabati? Nami nahitaji kuzipasi na kupanga vizuri nguo zako mpenzi!!!!!!!! Akibadilika na kukasirika basi jua kuna jambo kubwa kama si uchawi basi mwenzio ni positive hiv ana vidonge anameza kavificha. Utulie tuli wala usijibu mapigo kuwa mpole; ukipata muda chukua kipande cha sabuni kuku, hicho ni laini chukua funguo wake wa kabati kwa chati bonyezea kwenye hicho kipande cha sabuni; itatoka picha halisi ya funguo; basi shoga nenda kachongeshe funguo. Hapo ndipo utavizia kasafiri tena; ufungue kabati na usachi ujue kulikoni?????????utakachokikuta tujuze wana fj; usigombe wala kumuuliza, maana ulishamuuliza akaja juu......!!!!!!!!!!wasikia bibie??????????!!!!!!!!
   
 13. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #13
  Nov 22, 2010
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160
  Umechakachuliwa mumeo rafiki
   
 14. B

  Bi. Mkora JF-Expert Member

  #14
  Nov 22, 2010
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 375
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Hivi kwanini usifungue hilo kabati? Fungua ujionee mwenyewe vilivyomo humo ndani kisha funga akili kichwani.
   
 15. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #15
  Nov 22, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  FL1 umenichekesha eti, yaweza kuwa kaficha mkono wa albino! nimeona mapya sana kwangu hakuna kabati lake ila mi tu nimempangia sehemu ambayo ataona huku ni nguo zake tu!
   
 16. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #16
  Nov 22, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kuna vi herizi na vitunguli alivyopewa na sangoma hataki uvione. Na hiyo Khanga uliyoikuta ilitumika wakati anaogeshwa kwa madawa ili awe na mvuto wakati wa uchaguzi. Mumeo si aligombea udiwani kupitia Chadema, au?
   
 17. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #17
  Nov 22, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  kweli labda mshirikina huyo lkn hiyo kanga nayo,
   
 18. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #18
  Nov 22, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,287
  Likes Received: 22,047
  Trophy Points: 280
  Ukome na kiherehere chako
   
 19. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #19
  Nov 22, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Pole sana Nasra kwa yanatokukumba ndoani mwako.....! Lakini inaonesha humo ndani kuna hali kama hizi;

  1. Mmoja kati yenu, au wote mna tabia za kishirikina, au mnaamini hivyo....!
  2. Iwapo tatizo hilo lipo kwako, basi hata na mwenzio ana imani hiyo....!
  3. Zero uwaminifu baina yenu, na hii itakuwa imeanzia kwenye simu (kama wengi wanavyodai kuwa simu ni personal...!). Na kama simu ni personal kati yenu, why not kabati?
  Suluhisho:
  Kaa chini na mwenzio mzungumze, na iwapo tatizo litabainika, basi m-act accordingly....!
   
 20. N

  Nasra82 Member

  #20
  Nov 22, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Konakali yani huwezi amini ktk ushirikina huyo mwanaume hayupo kabisa maana nawafaham kwao vizuri sana labda sababu zingine tu! ila la ushirikina nina uhakika hakuna maana ningeona baadhi ya mambo, kwa mfano nimejifungua karibuni tu lakn mtoto hana shada lolote la uganga zaidi kasomewa hakika tu na kwa watu washirikina mtoto huyo angekuwa na kamba mwanzo mwisho! kwa wale wakrisitu hakika ni dua ambayo anasomewa mtoto wa kiislam akizaliwa ipo ktk quran hiyo hivo sio shiriki! kipo anachoficha lakn sio dumba
   
Loading...