Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
Imebainika kwamba wanandoa ambao wakikasirishwa wanatoa hasira zao, wanaishi zaidi kuliko wale ambao hukaa kimya lakini wanaumia kwa ndani.
Kuna wanandoa ambao wanaitwa wapole, ambao wala sio wapole, bali tu wakiudhiwa na wenzao huwa hawasemi.Sio kwamba hawasemi kwa sababu wamesamehe, hapana. Hawasemi kwa sababu wanazozijua, wakati ambapo ndani wanaumia sana kihisia.
Jambo la maana ni juu ya wanandoa kufurahia kutoa hasira zao pale wanapoudhiana kuliko kuwa kimya na kuugulia ndani. Wanandoa ambao wana kawaida ya kuficha hasira walizonazo baada ya kukorofishana zina vifo vingi kuliko ndoa ambazo zinatoa nafasi za mtu aliyeudhiwa kutoa dukuduku lake ili kupooza hasira.
Ndoa inaweza kuonekana kuwa ni ya amani kwa nje, kwa sababu mwanandoa mmoja ana uwezo wa kuficha hasira zake. Ukweli ni kwamba ndoa hii haina amani hata kidogo na ni ndoa ya kifo. Ni afadhali ile ndoa ambayo wanandoa wanaambiana ukweli, hata kwa kelele, kwani hapo afya zao haziharibiki.