Kaa kimya ufe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kaa kimya ufe!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Oct 3, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Oct 3, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Imebainika kwamba wanandoa ambao wakikasirishwa wanatoa hasira zao, wanaishi zaidi kuliko wale ambao hukaa kimya lakini wanaumia kwa ndani.

  Kuna wanandoa ambao wanaitwa wapole, ambao wala sio wapole, bali tu wakiudhiwa na wenzao huwa hawasemi.Sio kwamba hawasemi kwa sababu wamesamehe, hapana. Hawasemi kwa sababu wanazozijua, wakati ambapo ndani wanaumia sana kihisia.

  Jambo la maana ni juu ya wanandoa kufurahia kutoa hasira zao pale wanapoudhiana kuliko kuwa kimya na kuugulia ndani. Wanandoa ambao wana kawaida ya kuficha hasira walizonazo baada ya kukorofishana zina vifo vingi kuliko ndoa ambazo zinatoa nafasi za mtu aliyeudhiwa kutoa dukuduku lake ili kupooza hasira.

  Ndoa inaweza kuonekana kuwa ni ya amani kwa nje, kwa sababu mwanandoa mmoja ana uwezo wa kuficha hasira zake. Ukweli ni kwamba ndoa hii haina amani hata kidogo na ni ndoa ya kifo. Ni afadhali ile ndoa ambayo wanandoa wanaambiana ukweli, hata kwa kelele, kwani hapo afya zao haziharibiki.
   
 2. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  asante kwa kutujuza, sasa unashauri kuwa wote tuwe wasemaji ili tusife nayo moyoni au
   
 3. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  kweli kabisa ni njia mojawapo ya kukupatia amani maana umetoa yale yaliyomo moyoni.............. sema tu nimegundua wanaume wengi huwa hawapendi wanawake wanaosema.
   
 4. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  100/100!!
   
 5. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #5
  Oct 3, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Nisahihi baba but vp wale wanaotoa hasira zao kwa kutoa kichapo kwa mkosaji au kukimbizana mitaani na kurushiana maneno?
   
 6. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #6
  Oct 3, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  wengi hupenda kuficha aibu hivyo wanakufa na tai shingoni
   
 7. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #7
  Oct 3, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Umesema kweli Mkuu. Mimi nikikerwa na wife wangu huwa sifugi kitu. Huwa nampa black and white hapo hapo. Na tunaendelea na life kama kawaida. Yanini kujitia dhiki ya roho.
   
 8. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #8
  Oct 3, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mwanangu hapo sasa ni mambo ya Police case.............. ninachomaanisha ni wanandoa kutoa madukuduku yao kwa lugha za kistaarabu na sio kwa kutumia lugha za kashfa na matusi huko ni kuvuka mipaka........ Mara nyingi mtu anayetumia mabavu katika kujenga hoja, basi huyo ni dhaifu na hajiamini.............
   
 9. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #9
  Oct 3, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Takwimu yako umeipatia wapi? Tupatie source
   
 10. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #10
  Oct 3, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hiyo ni kweli kabisa mkuu, mara nyingi unapoweka vitu rohoni, baadae vinapandana na kulipuka na mara nyingi huleta matokeo mabaya........ tumeshasikia mwanandoa kunywa sumu, kuuwa watoto na yeye kujiua, kuuwa mwanandoa mwenzie...nk.
  Tunapolimbikiza hasira zetu pale tunapokosewa na wenzi wetu, tunajiweka kwenye nafasi ya kuumia rohoni na kutafuta namna ya kulipa kisasi. kulipa kisasi huko kunaweza kuwa ni kwa kujidhuru wenyewe au kuwadhuru wengine.......... na hii hutuletea majuto..........
  Lipo jambo moja, kuna baadhi ya wanandoa, hasa wanaume, wana kawaida ya kutokubali kushindwa, na pale wenzi wao wanapotaka kutoa dukuduku zao huwakata kalma na badala yake wao ndio wanaoongea peke yao wakikandamiza upande wa pili, hawako tayari kusikiliza upande wa wenza wao, na mara nyingi wao ndio wako sahihi............... Hii ni hatari kwa ustawi wa Ndoa. Wanandoa wanatakiwa wawe na plain ground, kila mmoja kwa nafasi yake ajisikie huru kutoa lililoko moyoni mwake, na upande wa pili uwe tayari kukubali kukosolewa.
   
 11. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #11
  Oct 3, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280  HA HA HA maefanya upembuzi yakinifu / Feasibility study
   
 12. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #12
  Oct 3, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Mimi kwangu bana NYEUSI NI NYEUSI na NYEUPE INABAKI KUWA NYEUPE! kufuga ugonjwa moyoni ni mbaya sana, bora utoe uwe mweupe kabisa!
   
 13. N

  Natalie Senior Member

  #13
  Oct 3, 2011
  Joined: Sep 25, 2011
  Messages: 165
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni kweli kabisa, wengine unakuta wana hasira za tokea kwenye uchumba, hawazisemi eti ili waolewe, wasiachwe kwa sababu tu umri umekwenda, halafu akiingia kwenye hiyo ndoa, matatizo yanazidi, anajutia na uamuzi wake wa kuikimbilia ndoa na mtu kama huyo, unakuta hana raha, mtu unatakiwa kusema, hata kama mpango wa ndoa utakufa, ufe, wengine wa kuoa wapo, pigania maisha yenye amani kwa kiasi kikubwa, sio kujiingiza kwenye matatizo, kwani asipo kuoa, unakufa?, na walio kwenye ndoa, toa dukuduku lako hata kwa kuhitisha kikao cha familia kama ni mbishi wa kukera.
   
 14. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #14
  Oct 3, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Tatizo kubwa ni wanaume! Hawa viumbe wengi wao huwa hawapendi mwanamke atoe yaliyomkera na ukikuta mke muoga ndo hasemi kabisa na matokeo yake anaambulia msongo na madonda ya tumbo kwa sana! Au siku likimkaba sana anaamua kujilipua na hatimae kujikuta akiprovoke hata mambo yasiyofaa kwa references za mwaka 47, wengine visasi vyao ndugu ni balaa!
   
Loading...