M-bongotz
JF-Expert Member
- Jan 7, 2010
- 1,734
- 405
Kwenye Gazeti la Dira ya Mtanzania la leo kuna taarifa kuwa makamanda wa JWTZ wamempiga mkwara mzito 'Kapteni' Lowassa kwa ile kauli yake ya wiki iliyopita kwamba JWTZ ipo tayari kuingia vitani na Malawi iliyoambatana na kutoa taarifa za utayari wa jeshi letu kwa vita hiyo. Kwa mujibu wa makamanda hao,mtu mwenye mamlaka ya kutoa kauli kama hiyo ni Rais pekee.