JWTZ, wafanikiwa kutegua bomu lililokuwa limetegwa visiwani Zanzibar

Kama hio habari ni ya kweli basi nina hakika kwa 100% kuwa ni Usalama wa Taifa ili wawshingizie Viongozi CUF wawatie ndina na Wapate Huruma kutoka Mataifa ya Nje waweze kubakia Madarakani Zanzibar

Ni wenyewe hao askari na majeshi, kama cuf wanamabomu wangekuwa washamiripua jecha
 
Pasco kweli wewe unawakilisha akili za waandishi wa habari wa Tanzanzia.

Yani mtu apate huruma kwa watu wengine lakini asijionee huruma yeye mwenyewe kitachomtokea baada kukubali kwamba katega bomu?

Na unaenda zaidi kusema akimtaja mtu aliyemtuma aachiwe huru ��.
 
Msituletee hadithi za kuchonga hapa. Eti bomu. Nani anamabomu nchi hii. Nani mwenye utaalamu na mabomu kama sio nyie wenyewe. Mnaojuwa kutega na kutegua. Michezo yenu tuu hiyo.

mkuu ww kama ni mweupe kama mwanamke nanga usikiri kila mtu yupo hvyo. Wangapi wamestaafu jeshi? Wangapi wamefukuzwa kaz za ulinzi na usalama?
Wangapi wanatoka nje ya nchi kuchukua mafunzo ya kigaidi? Watu wengne sijui mlizaliwaje
 
Lingine limelipuka muda sio mrefu leo hii maeneo ya michenzani barabara zimefungwa pale roud about.

Bomu gani linalipuka mita chache na askari bila madhara yeyote? Usaniii mtupu. Wanalipua baruti halafu wanaruka na kukanyagana. Wanzazibari we weee ,yaani burudani tosha.
 
Pasco kweli wewe unawakilisha akili za waandishi wa habari wa Tanzanzia.

Yani mtu apate huruma kwa watu wengine lakini asijionee huruma yeye mwenyewe kitachomtokea baada kukubali kwamba katega bomu?

Na unaenda zaidi kusema akimtaja mtu aliyemtuma aachiwe huru ��.
Mkuu tatizo ni uelewa!. Mambo ya mabomu ni terrorism, sometimes hawa wahusika wakikamatwa na kuadhibiwa, ndio unahamasisha zaidi, kwa sababu wameaminishwa mambo ya matridom.

Zanzibar enzi za Karume, baada ya yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, kuna watu walioyapinga. Jee uliwahi kusikia kesi zozote zikiendeshwa kwa waliompinga Karume?!, ilikuwa ukijulikana tuu ni 'kimya kimya' you v
anish into thin air!, hata unywele hautaonekana!.

Wamerekani walipomkamata Osama, unadhani walishindwa kumshika, na kumshitaki?!, au walishindwa nini kuutoa mwili wake kwa familia yake wauzike kwa heshima na kaburi liwepo?!. Kuna vitu huwa vinaepukwa, hivyo mambo yanamalizwa 'kimya kimya!', hivi ndivyo inabidi wa deal na Wazanzibari, hizo 'kimya kimya' wenzetu waliishazizowea!.

Pasco
 
njia pekee ya kuzuia machafulo zanzibar either ya mda mfupi au mrefu ni kumpa maalim self ushindi wake na si vinginevyo maana hata uchaguzi ukiridiwa na akashinda wa CCM ,cuf hawata kubali na machafuko yataendelea milele.

na hata kabla ya hvyo pia watu wanaweza kuacha kupiga kura yakapiga majimbo yale ya unguja tu yenye wanachama wa CCM.
CCM kweli hawana akili,maalimu ameshinda majimbo yote pemba na baadhi ya majimbo unguja mwenzio Dr.shain hajashinda jimbo hata moja pemba huoni umisha shindwa?

Kama Seif alijua kashinda kwanini asingesubiri kutangazwa na tume kama mshindi badala yake kaamua kuiamrisha tume imtangaze yeye kama mshindi... Hiyo power kaitoa wapi hili pia linatutia wasiwasi na uchaguzi lazima urudiwe kuna makosa mengi sana yamefanyika katika uchaguzi wa Zanzibar.
 
Sidhani kama kimya kimya ni suluhisho la matatizo, Hapa haki itende kazi tu, ubabe hauna maana, Kwani ni lazima wao tu ndio wawe watawala, democrasia iko wapi? kisiwa cha amani kiko wapi?
 
Je ni kweli katiba inasema adhabu ya kujitangaza mapema ni kufuta uchaguzi? kama unaamini haisemi hivyo basi watunge a
dhabu mbadala, Na pia lazima ujue chanzo cha makosa yote yaliyobainishwa sio ya vyama ni ya tume, hivyo tume ndiyo inapaswa kuwajibika na sio kufuta uchaguzi, je unafikili tume hiyo tena itaaminika.
 
kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi mh .lubuva zanzibar ni nchi kamili yenye katiba yake na rais wake kwa hiyo matokeo yaendelee kutangazwa kuingilia nchi nyingine utakuwa umeivamia na kitendo cha kuiacha kauli hii ngumu kisheria ingawa ipo kikatiba ilikuwa inahitaji tafsir laini tusijenge ufa .huu kesho unaingilia watakuuliza hawa umetumia kanuni gani ,ihali umeshajenga ufa mkubwa. Na umeshatoa tafsiri,
 
Mkuu tatizo ni uelewa!. Mambo ya mabomu ni terrorism, sometimes hawa wahusika wakikamatwa na kuadhibiwa, ndio unahamasisha zaidi, kwa sababu wameaminishwa mambo ya matridom.

Zanzibar enzi za Karume, baada ya yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, kuna watu walioyapinga. Jee uliwahi kusikia kesi zozote zikiendeshwa kwa waliompinga Karume?!, ilikuwa ukijulikana ni 'kimya kimya' into thin air!, hata unywele hautaonekana!.

Wamerekani walipomkamata Osama, unadhani walishindwa kumshika, na kumshitaki?!, au walishindwa nini kuutoa mwili wake kwa familia yake wauzike kwa heshima na kaburi liwepo?!. Kuna vitu huwa vinaepukwa, hivyo mambo yanamalizwa 'kimya kimya!', hivi ndivyo inabidi wa deal na Wazanzibari, hizo 'kimya kimya' wenzetu waliishazizowea!.

Pasco

Pasco Alikuwa UKAWA kama video ya watu!!!
 
Kama Seif alijua kashinda kwanini asingesubiri kutangazwa na tume kama mshindi badala yake kaamua kuiamrisha tume imtangaze yeye kama mshindi... Hiyo power kaitoa wapi hili pia linatutia wasiwasi na uchaguzi lazima urudiwe kuna makosa mengi sana yamefanyika katika uchaguzi wa Zanzibar.

Kama tume wana matokeo yote tatizo liko wapi? Si wangeonesha matokeo tu yaishe.

Inamana Ahmad Rashid nae angesema hesabu zao kutoka vituoni zinaonesha kashinda wangefuta matokeo?

Ndio maana kuna umuhimu wa matokeo yaruhusiwe kupingwa mahakamani. ZEC wangetaza matokeo yao alafu wangewaambIa wale wanayoyapinga waende mahakamani hili pande zote zioneshe ushahidi.

Tume ya uchaguzi hairuhusiwi kupingwa mahakamani lakini tume hio hio inataka Seif akamatwe apelekwa mahakamani.
 
Hivi kweli kuna watu wanaamini kwamba bomu lile limetegwa na Mzanzibari kwa ajili ya kuwaua Wazanzibari wenzake wasio na hatia badala ya kuwalenga viongozi wa CCM ambao ndio mahasidi wao kwenye sakata hili?

Kinachoendelea ni CCM kutumia vyombo vya dola kuweka mazingira ya kuwatisha Wazanzibari wasijitokeze kwa ajili ya maandamano ya amani ya kudai haki yao ya Urais wa Maalim Seif waliopokonywa kininja na CCM.

Dhambi hii ya taifa masikini la kutupwa kulitawala taifa lingine kwa mabavu na hivyo kulisababishia umaskini maradufu itaendelea kutuandama sisi Watanganyika milele kwani hata huku Tanganyika itakuwa vigumu kuin'goa CCM katika mfumo huu wa muungano. Mfano mzuri ni sasa hivi kwenye uchaguzi huu. Juu ya kwamba kuna wizi wa kura wa wazi uliofanyika na kumnyima ushindi Lowassa, macho yote ya ulimwengu yamehamishiwa Zanzibar kutokana na ubabe wa kihuni kabisa uliowahi kutokea hapa duniani wa kufuta matokeo ya uchaguzi Zanzibar wakati huo huo kuruhusu uchaguzi huo huo uliofutwa kutambulika kwenye kura za Muungano!!!
 
Hilo bomu wamelitega wenyewe ili wapate uhalali wa kuendelea kukaa mitaani kwa hoja ya kuwa cuf wanahatarisha usalama
 
mkuu ww kama ni mweupe kama mwanamke nanga usikiri kila mtu yupo hvyo. Wangapi wamestaafu jeshi? Wangapi wamefukuzwa kaz za ulinzi na usalama?
Wangapi wanatoka nje ya nchi kuchukua mafunzo ya kigaidi? Watu wengne sijui mlizaliwaje

CCM mmetega bomu na kulitegua wenyewe.
 
zanzibar mjini kote kuna ccctv cameras zenye uwezo wa kuvuta mpaka km moja. Mtu yoyote akifanya uhalifu anaoneka na kurekodiwa,
 
Mkuu umeongea kwa jazba sana kiasi kwamba umesababisha ujumbe wako kuonekana una upendeleo flani na chuki juu ya znz. Hata ndoa za kikanisa zikishindikana basi kuna chombo kinazingenisha ambacho hakikuhusika kufungwa kwake.
Huyo unayesema angeweza kumpiga kufuli maalimu yuko wapi, mtafute kwenye baraza zote kama utamuona, hata ungepewa ukalale nae kwenu asinge kufaa kitu kwani mfalme wa wafalme amemnyamazisha na kumfanya dhalili akiliwa na wadudu. Hakuna jabari atakedumu milele afanye dhulma atakavyo. Huyo jamaa yako hakufika hata theluthi ya firauni, je leo unasikia sauti ya firauni??? Amegeuzwa kinyago watu wenda kumsanifu na kujiuliza ni ujuha kiasi gani aliokuwa nao akidhani yeye ndo alfa na omega???

Kamfufue basi umwambie sefu amechaguliwa na wananchi na hakuna wakumnyamazisha uone kama atakujibu chochote. Mwisho wasiku na wewe pia utapiga mishuzi mimacho yatakutoka hunachako tena duniani. Hakuna hila wala namna. Fikiri kabla yakusema na kutenda, twendako si mbali
 
Back
Top Bottom