Kila mtu anataka kuwa mwanasisa kwa sababu ya maslahi mazuri zaidi, matokeo yake wataalamu hawaoni haja ya kutumikia jamii katika nyanja zingine zaidi ya siasa inayolipa zaidi.
Vurugu katika kuwania nafasi za kisiasa ni kwa sababu tu ya kipato na wala siyo wito kama wachache wanavyodanganya.
Tunahitaji mfumo ambao kipato kinachotokana na siasa kwa nafasi kama MP, DC, RC, kiwe kidogo kuliko kinchotokana na utaalamu uliobobea ili tupate wanasiasa wa wito na wtaalamu wabaki kwenye fani zao.
Wanasiasa walio wengi sasa hivi ni watu waliojaa tamma, wezi au washirika wao, mafisadi au washirika wao na ni wachache sana unaoweza kuwatenganisha na maovu yanayoangamiza wananchi wa kawaida.
Mfumo wa kisiasa uliopo sasa umewapumbaza wananchi na kujiona kuwa wanyonge wasiostahili maisha mazuri, na bdala yake wao ni watumwa na wapiga debe tu wa wanasisa.
Mifano halisi ya utumwa wa akili na kuwapigia debe wanasisa na familia zao inapatikana humu humu unaposoma posts za wanaJF.
Lazima tujue kwamba mwenye shibe hajui njaa na hivyo kutegemea utetezi kutoka kwa wanaolipwa zaidi ya mara hamsini ya mshahara wa mfanyakazi wa kawaida haiwezekani.
Tunahitaji tujenge jamii ambayo walio wengi ambao siyo wanasiasa na ni wazalishaji wanaweza kuwa na uwiano sawa kimapato na wachache wasio na tija kwa asilimia kubwa (kwa hali halisi ilivyo sasa), ambao ni wanasisa.