JUNI MOSI:Wamasai wa Ngorongoro kutikisa nchi

JUNI MOSI:Wamasai wa Ngorongoro kutikisa nchi

Concrete

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2011
Posts
3,605
Reaction score
552
Tarehe moja mwezi wa Sita mwaka huu, wamasai wa Ngorongoro wameapa kuandamana na kufunga kabisa geti kuu la kuingia hifadhi ya Ngorongoro hivyo kuzuia shughuri yoyote ya utalii kuendelea katika hifadhi hiyo kama serikali haitasikia kilio chao na kutatua tatizo la njaa linalowakabili kutokana na kuzuiwa kulima kilimo cha kujikimu kando ya Hifadhi hiyo.

Hapo kabla Serikali ilipiga marufuku kilimo cha kujikimu kando kando ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa madai kuwa kinaharibu makazi asilia ya wanyama.

Mamia ya wamasai hao walikuwa wamekusanyika wakiwa na viongozi wao wa kijadi na kijamii na kutoa kauli moja.

Waziri wa Maliasili na Utalii Hamis Kagasheki ulipoulizwa kuhusu swala hilo alijibu kwa hasira kwa kusema, vitisho hivyo havimbabaishi na hana mamlaka ya kushughulikia suala hilo kwani linahitaji uteuzi wa mkurugenzi mpya wa Hifadhi hiyo na hiyo ni kazi ya rais.

*SOURCE: Channel Ten
 
Huku Mtwara! Kule Ngorongoro! Kikwete unakazi!
 
Na kama wataamua kufanya kweli wale ni noma! tulipigana nao vita ya kuibiana n'gombe miaka 50 iliyopita kati ya wasukuma na wamasai ilikuwa noma,sijui itakuwaje! na kwa kauli za majivuno na kejeli za mawaziri wa JK ..... ngoja tuone.
 
Tarehe moja mwezi wa Sita mwaka huu, wamasai wa Ngorongoro wameapa kuandamana na kufunga kabisa geti kuu la kuingia hifadhi ya Ngorongoro hivyo kuzuia shughuri yoyote ya utalii kuendelea katika hifadhi hiyo kama serikali haitasikia kilio chao na kutatua tatizo la njaa linalowakabili kutokana na kuzuiwa kulima kilimo cha kujikimu kando ya Hifadhi hiyo.

Hapo kabla Serikali ilipiga marufuku kilimo cha kujikimu kando kando ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa madai kuwa kinaharibu makazi asilia ya wanyama.

Mamia ya wamasai hao walikuwa wamekusanyika wakiwa na viongozi wao wa kijadi na kijamii na kutoa kauli moja.

Waziri wa Maliasili na Utalii Hamis Kagasheki ulipoulizwa kuhusu swala hilo alijibu kwa hasira kwa kusema, vitisho hivyo havimbabaishi na hana mamlaka ya kushughulikia suala hilo kwani linahitaji uteuzi wa mkurugenzi mpya wa Hifadhi hiyo na hiyo ni kazi ya rais.

*SOURCE: Channel Ten
Kiburi cha Waziri Balozi Kagasheki itatuweka pabaya katika tasinia ya utalii. Kikwete achukue hatua!
 
Huu uwaziri wa kupeana kama pipi ndio mazara yake na ukizingatia anaempa hajapevuka kiakili.
 
Mbona ngoma inogile......na Masai akisema amesema........
 
Kiboko yao ni polisi na FFU....hawatafurukuta
 
Hivi hawa Viongozi wakitoaga kauli huwa wanafikiria mara mbili kweli?!
 
Ushauri wa bure tu kwa serikali hii.Wamasai ni watanzania wenzetu wanaostahili kupewa huduma kama raia wengine.Suala la njaa halikuanza leo kwa wananchi hawa wanaoishi kando kando ya hifadhi ya Ngorngoro na wamekuwa wakiishi na kulinda wanyama hawa kwa muda mrefu hata kabla ya kuanzishwa hifadhi hiyo.Ni kabila ambalo wanaheshimu sana wanyama pori na ni mwiko kwao kuua wanyama pori achilia mbali hata kula nyama yao.Serikali imeshindwa kuwapelekea chakula cha msingi hapa uanzishwe utaratibu wa wao kupewa maeneo ya kulima kilimo cha kujikimu kwa mpango maalumu ambao hautaathiri ecolojia ya Ngorongoro.Kama miaka ya nyuma iliwezekana kwa nini leo ishindikane?Mtadharau kama mlivyodharrau ya Mtwara matokeo yake yameonekana mnaanza kusingizia vyama vya upinzani.CCM chukueni hatua mapema wananchi wamekata tamaa.
 
Lakini dai lao lingine ni kuwa hawamtaki Kaimu Mhifadhi Mkuu aliyeteuliwa hivi karibuni, Bwana Martin Loibooki (Mmasai mwenzao) na madai yao yameungwa mkono na Mbunge wa Ngorongoro Mh. Telele
 
Ni vizuri kuwa sikiliza. Swala la chakula ni la msingi. Hata katiba yetu imebainisha kinaga unaba kwamba kila mtu anahaki ya kuishi.... Sasa kama mnawazuia kulima afu hawapatiwi chakula, hapo kwa kweli katiba ya nchi itakuwa imekiukwa. Afu waziri husika anaongea kwa jeuri. Utawala wa sheria upo kweli hapo???
 
Ndg unapanswa kutambua kuwa Tz na vyote vilivyopo n vyetu na vizaz vijavyo vya watz. Miaka hyo wakat wanaruhusiwa kulima kando ya hifadhi idad yao ilikuwa ndogo sn na ivo hawakuathiri kitu. Wakat huo walikuwa na mifugo mingi ivo hawakuwasumbua wanyama. Leo wamasai wa ngorongoro n wengi na wakiruhusiwa kulima ngorongoro itakuwa hatarin kutoweka. Je, wewe upo tayar uone ngorongoro inafanywa makaz?
 
nimesema mambo ya mabavu yameshapitwa na wakati viongozi husika kaeni na hao watu kabla mambo hayajaharibika,na utalii ndio umeanza hatupendi wageni waone haya mambo jamini,serikali ya kijiji na mkuu wa wilaya,mbunge kaeni mara moja mtupe majibu
 
Back
Top Bottom