Jumuiya ya Afrika Mashariki zitenge Tanzania na Burundi

cutelove

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
3,317
7,509
Nchi za Kenya, Uganda na Rwanda hongera kwenu,mnaonyesha kwa vitendo juhudi zenu katka kupambana na janga la covid 19

Mmeonyesha wananchi wenu namna mnavyopambana na covid 19 kwa mikakati mbalimbali kama lockdown na kupima watu

Nchi za Tanzania na Burundi hazijaonyesha mikakati muhimu katika kupambana na covid 19,licha ya serikali zao kusema wapo mbele kupambana na covid 19 hamna cha zaidi walichofanya zaidi ya kusitisha sherehe za serikali,mikutano ya kisiasa na shule na vyuo

Nchi hizi zimefikia hatua hata jumuiya za kimataifa zimeanza kutilia mashaka kuhusu data zao kuhusu covid 19

Katika kufanikisha vita hii ndani ya Jumuiya lazima nchi wanachama waende kwa pamoja ili kufanikisha hii vita lakini wenzenu Tanzania na Burundi watasababisha msishinde hii vita

Tanzania na Burundi hawapimi watu wala hawaonyeshi mbinu zaidi ya kuzuia maambukizi nchi nzima,ni hatari kwa nchi hizi maambukizi kwa sasa yapo mpaka vijijini

Ni wakati mwafaka sasa Jumuiya ya Afrika Mashariki mkajitenge na hizi nchi,serikali zao zipo kimaslahi zaidi kuliko maisha ya watu,kule wanawaza uchaguzi ,huku wanawaza mapato
 
Nashauri pia JF wakupige ban ya maisha, haiwezekani mwanaume utumie ID ya kike you must not be right upstairs.
Ujumbe nauhakika kaupata.

Ila nawaza, halafu nacheka, sijui in real life unawezaje kutamka maneno kiusahihi, haswa hilo 'upstairs' na hayo mapengo hapo.
 
kwa mfano wewe ukisimamishwa mbele ya marais, mawaziri wakuu na mawaziri wa afya wa hizo nchi ulizotaka zitengwe, ungewashauri wafanye nini kupambana na huo ugonjwa?
 
Burundi wao wanasema Taifa lao limebarikiwa na Mungu na wanaendelea na ligi ya mpira fresh kabisa.
 
Hii yetu ni nchi ya kijinga sana sana.......
FIVE YEAR FAILED PRESIDENT
 
Rafiki nakuhakikishia Corona itakapoisha huko kwingine Tanzania itabakia ni kitovu cha kuzalisha Corona duniani na itapigwa lockdown na mataifa yote, yaani hakuna raia yeyote wa kigeni ataruhusiwa kuingia nchini wala ng'ombe atakaeruhusiwa kutoka Tanzania kwenda nje!
 
Back
Top Bottom