Jumuiya ya Afrika Mashariki na Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jumuiya ya Afrika Mashariki na Zanzibar

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MsandoAlberto, Apr 20, 2011.

 1. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwenye gazeti la Guardian la tar. 20/4/2011 ukurasa wa mbele kuna picha yenye maneno yafuatayo....

  'Heads of EAC partner states stand attention as their national anthems are played at the start of the 9th extraordinary summit in DSM yesterday. From L are President Yoweri Museveni of Uganda, Mwai Kibaki of Kenya, Pierre Nkurunzinza of Burundi and J. Kikwete of Tanzania. With them are Rwanda Prime Minister Bernard Mukuza and Zanzibar President Dr. Ali Mohamed Shein'....

  Najiuliza, je Dr. Shein ameenda kama mualikwa au msikilizaji? Nafasi yake katika hicho kikao ni ipi?

  Je, kiitifaki nani anaanza kwenye mpangilio wa kukaa na kutajwa, Raisi au Waziri Mkuu? Iweje Waziri Mkuu wa Rwanda akae kabla ya Raisi wa nchi? Au ndio confirmation kwamba Dr. Shein alialikwa tu?

  Mwenye uwezo wa kutufahamisha tusiojua ushiriki wa Dr Shein kwenye kikao hicho atufahamishe.

  Natanguliza shukrani.
   
 2. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mh maskini Zanzibar!
   
 3. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mpevu, najaribu kuyaweka maneno hayo moyoni mwako naona uchungu ulionao! Ni matumaini yangu suluhu itapatikana!
   
 4. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  kwa jinsi hali ilivyo sasa-sitashangaa zanzibar nao waombe kuingia EAC kama wao-maana ilitakiwa Shein asiwepo hapo-nashindwa kujua kama Jey kei nae anashindwa kumshangaa mwenzie anangoja nni sehem kama hizo-maana kama EAC nchi inayatambulika ni Tanzania-binafsi sijaona sababu za Shein kuwepo hapo
   
 5. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Sasa hizo nyimbo za taifa kupigwa; walipiga wimbo wa taifa la Zanzibar?

  Kama hapana well alisindikiza kwa kunuia kujiunga!!!
   
 6. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Yaani ni vululu vululu tu,
  Tutajichanganya weeee na huu "muungano wa pekee" duniani
   
 7. N

  Nonda JF-Expert Member

  #7
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Pitia hii doc ipo link hii

  Eastern African Centre for Constitutional Development - Document Details | Aii.Shirikisho Ndani ya Shirikisho:Uzoefu wa Muungano wa Tanzania by F. Jjuuko & G. Muriuki. Swahili

  Halafu soma ukurasa wa 90-98. Unaweza kupata jibu lakini pia inawezekana kuona tatizo lipo wapi.

  Kwa kuchangia hapo cheo cha waziri mkuu wa Rwanda anawakilisha Rais wake, sijui itifaki ikoje lakini kimantiki anakalia kiti cha rais wa wake.

  Zanzibar kulingana na set up ya muungano ulivyo bado hawezi kuwa mwananchama wa EAC lakini hayo utayapata katika ukurasa wa 90-98. Itakuwa Dr, Shein ni mwalikwa tu lakini pia ni kiashiria kuwa members wa EAC wanataka kuona Serikali ya Muungano inaunda mechanism ambayo itaiwezesha Zanzibar kujiwakilisha yenyewe katika EAC kwa sababu mambo mengi ya EAC sio mambo ya Muungano katika ile orodha ya mambo ya Muungano wa TZ.
   
 8. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #8
  Apr 20, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Huu muungano ni wa kuangaliwa upya... NUKTA! na kwanini serikali ya chama cha mapinduzi wanajifanya kama hawalioni hili..?!!.. inakera kweli. na itazidi kukera kama wakiweka serikali tatu. znz inatakiwa iwe nchi jirani.
   
 9. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Hii ndio maana waZanzibari hawautaki muungano kwani una kasoro nyyingi sana ikiwapo hiyo.

  Hata muswada wa katiba mpya ULICHANWA hadharani.
   
 10. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nonda nakushukuru sana. Nitapitia halafu nitarudi. Natumia ka-mobile kangu ila nikirudi ofisini nitautendea haki mjadala huu.

  Huu mkanganyiko wala hauna haja ya kuangalia mambo makubwa, kitendo cha mwandishi na mpiga picha kushindwa kumtaja Shein na nafasi yake katika jumuiya ni kiashiria tosha kuna tatizo. Lakini bado watu wataangalia pembeni kama hawaoni.
   
 11. N

  Nonda JF-Expert Member

  #11
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Na namna nyingine ya kuhakikisha ushiriki wa Zanzibar katika
  Jumuiya ya Afrika Mashariki ni kuhudhuria kwa watumishi wa
  serikali wa Zanzibar au viongozi katika vikao vya Jumuiya hiyo.
  Imeelezwa kuwa, Tanzania inapokuwa mwenyekiti, kunakuwapo na
  ushiriki mkubwa zaidi wa Zanzibar katika mikutano ya Jumuiya ya
  Afrika Mashariki. Kwa hiyo rais wa Zanzibar amehudhuria mikutano
  ya Wakuu wa Nchi pale Tanzania inapokuwa mwenyekiti. Lakini​
  mialiko kama hiyo haitolewi kama si hivyo. ukurasa wa 101
   
 12. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #12
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Poleni wazanzibar, lakini kwa nini msijitoe muungano.. mnasubiri nini?. Si waambieni tu wabunge wenu wanaohudhulia vikao vya bara, makamu wa rais na wazanzibar wachache wanaoishi bara warudi kwenu then tangazeni Zanzibar huru bila ya Tanganyika. Mnaweza mkapata mahala pazuri pa kuanzia kama mkianza na hilo manake linatekelezeka kama mkiwa na umoja
   
 13. data

  data JF-Expert Member

  #13
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 16,747
  Likes Received: 6,524
  Trophy Points: 280
  Msipoteze muda kwa msilolijua.. Mpigieni cm Dk.shein mumuulize alialikwa kama nani..? Okoeni muda wa wana JF wataopita hapa. AHSANTENI
   
 14. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #14
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  <p>
  </p>
  <p>&nbsp;</p>
  asante kwa kutujuza.lakini nadhani japokuwa jk alikuwepo,shein kama kiongozi mkubwa pia wa nchi mwenyeji wa mkutano ana haki ya kuwepo na kupokea heshima yake.isingekuwa busara kwa mkutano muhimu awepo rais wetu pekee na waziri husika na wahudumu/support staff. jaokuwa complications za muungano zina sehemu yake in this.
   
 15. J

  JokaKuu Platinum Member

  #15
  Apr 20, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,768
  Likes Received: 4,982
  Trophy Points: 280
  Nonda,

  ..nje ya mipaka ya Tanzania, Zanzibar haitambuliki kama nchi.

  ..sidhani kama kuna taifa la nje linaloweza kufanya makosa ya kuwaalika kwa wakati mmoja maraisi wa Tanzania na yule wa serikali ya mapinduzi smz.

  ..hata vyombo vya fedha vya kimataifa haviwezi kuikopesha ZNZ kwasababu hawana Benki Kuu, na zaidi siyo nchi. ZNZ ikitaka kukopa lazima idhaminiwe na serikali ya muungano/Tanganyika.
   
 16. N

  Nonda JF-Expert Member

  #16
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Usuli huu ni sahihi ikiwa mtu anataka kuuelewa vyema mtazamo
  wa baadhi ya Wazanzibari kuhusu juhudi mpya juu ya Shirikisho
  la Afrika Mashariki, na kuhusu Muungano wenyewe vile vile. Ni
  muhimu kuelewa vile vile kuwa Muungano ulikuja wakati nchi zote
  mbili zilikuwa wanachama ya Umoja wa Huduma za Pamoja wa
  Afrika Mashariki (EACSO), ambao uliendesha huduma za pamoja,
  Umoja wa forodha na sarafu ya pamoja.

  Mwaka 1977, ile iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki
  ilisambaratika. Miongoni mwa mambo mingine, kuna matukio
  mawili muhimu ambayo yana umuhimu maalum kwa Muungano,
  ambayo yanatokana kwa upande mmoja na kusambaratika kwa
  asasi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hilo moja ni mahasusi na
  linahusiana na rasilimali za Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki
  ambayo ilivunjwa mwaka 1966 na haihusiani moja kwa moja na
  iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kila nchi ililipwa hisa
  zake za rasilimali ya Bodi. Hisa za Zanzibar zilikabidhiwa kwa
  Tanzania. Ni fedha hizi ndizo zilizotumika kuanzisha Benki Kuu ya
  Tanzania. Pesa za kutoka Bodi ya sarafu inasemekana kuwa zilikuwa
  asilimia 12% ya mtaji wa Benki Kuu. Hili limethibitika kuwa ni
  jambo linalolalamikiwa sana Zanzibar. Ilisisitizwa na watu wengi
  waliohojiwa Zanzibar, kuwa Zanzibar ilistahili ipatiwe hisa zake.
  Hili ni jambo moja la msingi linaloifanya Zanzibar iwe hairidhiki

  Muungano na Kuunganishwa kwa Afrika Mashariki
  95
  na Muungano. Kwa baadhi ya watu, hili linahusishwa na Zanzibar
  kutaka kuwa na sarafu yake yenyewe.

  Tukio jingine muhimu lililotokana na kuvunjika kwa iliyokuwa
  Jumuiya ya Afrika Mashariki ni kuongezwa kwa mambo ya
  Muungano kutoa 11 ya asili. Kwa mujibu wa mawazo ya pamoja
  ya Zanzibar, kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kumetoa
  fursa kwa Muungano ya kuumeza taratibu uhuru na utambulisho wa
  Zanzibar kwa kuongeza orodha ya mambo ya Muungano ambayo
  sababu zake za kimantiki zitakuwa ni Muungano wa serikali moja.
  Hati ya kisheria &#8211; Mkataba wa Muungano &#8211; haukugusia juu ya
  mambo yaliyokuwa yakiendeshwa na Umoja wa Huduma za Pamoja
  wa Afrika Mashariki; ulijikita katika vipengele 11. Katiba ya 1977
  iliyokuja baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki
  iliifanyia marekebisho orodha hiyo na kuyaingiza mambo yote
  ambayo hapo awali yalikuwa yakiendeshwa na Jumuiya ya Afrika
  Mashariki kuwa ni mambo ya Muungano. Ukurasa 94-95

   
 17. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #17
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu, Zanzibar imesikia wito wako lakini kwa taarifa yako imeshaanza kuchukua hatua ya kuelekea huko.

  Unaweza kuangalia Mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984.

  Kuhusu umoja pia ni dhahir shahir baada ya kupitisha Mswada wa kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

  Sisi hatutaki kufarikiana na ndio maana tunachukua hatua kidogo kidogo.

  Zanzibar for Zanzibaris
   
 18. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #18
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0


  Hapo zamani labda, sio sasa. Angalia hapa tafadhali:(Mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar ya 1984)


  (9)(i) Zanzibar itakuwa ni NCHI ya kidemokrasia na haki za kijamii.

  (9)(2)(a) Mamlaka ya kuendesha NCHI ni ya wananchi wenyewe &#8230;

  (10) Kwa madhumuni ya kuendeleza umoja na maendeleo ya watu na ustawi wa jamii katika NCHI itakuwa ni wajibu wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar:

  (10)(3) Itadhibiti uchumi wa NCHI kufuatana na misingi na madhumuni yaliyoelezwa na katiba hii.

  (12)(3) Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtu yatalindwa na kuamuliwa na mahkama pamoja na vyombo vya NCHI na vinginevyo vilivyowekwa na sheria.

  (21)(i) Kila Mzanzibari anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa NCHI&#8230;

  (23)(2) Kila mtu ana wajibu wa kulinda maliasili ya Zanzibar, mali ya NCHI pamoja na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi&#8230;
   
 19. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #19
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sawa kiongozi nimekuelewa lakini kwa mantiki ya muungano huu ukiangalia vyombo vilivyounganishwa ni vyombo vya dora vile muhimu vyenye cohesive apparatus kama jeshi, polisi, uhamiaji, usalama wa taifa, fedha, foreign affairs na CCM kama play maker. Ukitazama kwa angle nyingine mabadiliko hayo ya katiba unayoyataja wazungu wanasema You are just beating around the bush, your not beating a snake. Kama mkianza kupangua na hivyo vyombo vya dola ndio kweli mtakuwa mnaanza kufanya kazi. Sanasana hayo mabadiliko ya katiba is just a cosmetic change, na yanaonekana wazi yamefanywa ili kucompromise kundi flani nalo lishiliki katika kula Zanzibari's cake. Na huu ubia wenu wa CCM na CUF mlioujenga kwa sasa,unafanya iwe vigumu kutambua vision ya political elite wa visiwani , maana vyama hivyo viwili vinavision tofauti ya muungano. Na sio siri kuwa kuna wanasiasa visiwani kuwapo kwao kwenye siasa kunategemewa nguvu ya CCM bara. Sasa nao ninaimani hawatapenda wapotee kisiasa hivihivi
   
 20. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #20
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu mimi ukizungumza hivi nakuelewa sana na ni kweli sio mabadiliko makubwa yaliofanyika. Nimewahi kueleza pahala pengine kwenye kurasa hizi za JF juu ya hili.

  Huu "Muungano" umedumu kwa muda mrefu na tunajua kuwa kuna viongozi wa pande zote mbili wananufaika nao na ndio maana imekuwa vigumu kuung'oa au kuuvunja. Hata hivyo, nahisi upepo wa mabadiliko umeanza na haitakuwa rahisi kuuzuia.

  Napata nguvu nikisikia maneno kama haya kutoka kwa vigogo wetu, tena wa CCM:


  *"Ule wakati wetu na Nyerere tulikuwa tunakubali lakini hawa vijana wa leo hawakubali, Bw. Sitta, ITS OVER*".
  Sisi vijana wa zamani tulishindwa lakini naamini hawa wa sasa wataweza.
   
Loading...