Wakuu salama.
Wandugu jumatano,tarehe 05.11.2014 natakiwa niende angaza kupima UKIMWI hapa nilipo confidence ni zero inaelekea negative.
Kwa kawaida mimi huwa najiamini kupita kawaida kwa kila jambo nalofanya lakini hili la ukimwi confidence imedrop significantly.
Kiukweli sijawahi kupima ukimwi toka nimezaliwa,kuna binti kaniambia hawezi kukubali kutoka nami bila kupima,alinipa interval ya miez 3 nikamshawishi hadi akakubali tufanye angalau test 1.
Sitaki kumkosa huyu binti na naogopa kupima,ebu nipeni makonfidensi wakuu
Mkuu,
Nenda kapime, nadhan ni bora Ukapime kwa hiyari, kuliko mazingira yakulazimishe kupima. Nasema hivyo kwa sababu moja... Kupima Afya ni One step towards awareness ya huu Ugonjwa, Pia Utafundishwa namna ya kuuepuka, au namna ya kufanya Ngono Salana hii kwa ambae hajaoa, alieoa, ni kufundishwa namna ya kufanya tendo la ndoa salama... Nakumbuka mm nilipima nilipokuwa naaoma high school pale JITEGEMEE, ila kilicho pelekea kupima, ni kuwa, nilimpiga denda mdada flani, kisha baadae nikaja ambiwa ni HIV+, sasa kwakukosa uelewa juu ya huu Ugonjwa, nikaanza kukonda kwa Mawazo.
Nakumbuka niliingia kipindi cha Dini Alhamisi, muhubiri siku hiyo akawa anazungumza masuala ya Afya, Marq mwili ni Hekalu la Mungu, basi nilipotoka, nikasema "Liwalo na Liwe" nakwenda kupima "NGOMA" Leo, basi baada ya Pindi nikaenda nikapima, Namshukuru Mungu majibu yalikuwa Negative... After that, Nikakaa miezi mitatu nikarudi tena, still Negative... Hapo sasa ndio maisha mapya yakaanza... Japo kupima hakumaanishi umepata kinga ya Ukimwi, but knowing all about HIV... Inakufanya unakuwa careful, responsible of ur own actions pia, somehow ina kuset Free from Fear. Kapime alone, kisha nenda na Mchumba mkapime, Mshauriwe namna ya kustay Negative. Hapo mambo ya Condom na mamaa yanakuwa ni kujikinga Na Mimba zisizojarajiwa....
Goodluck Man.