Duuu, pole kwa mpwao kwa yaliyomkuta. Nafikiri kama ana akili zilizotulia vzr, tukio hili limfundishe kubadili tabia. Mimi binafsi singali bado nikiamini kuwa uanaume wangu ni sababu ya kubadili wanawake nipendavyo. Tabia hii siyo nzuri, nami huwa naitafsiri ni kama kuzitesa na kutokuzitendea haki nafsi za wapenzi wenu ambao mnawabadilisha kila siku. Jiweke kwenye position ya Mpwao, ingekuwa yeye ndiyo kafumania angejisikiaje?
Mshauri rafiki yako aachane na tabia hizi, maana akiendelea huwenda yakamkuta makubwa kuliko haya! Jaribu kupiga picha kama mmoja wa hao angukuwa hata na silaha ya jadi, na kwa bahati mbaya akamuua aliyemfumania, hali ingekuwaje kama si kupelekana jela?
Ni vizuri kuwa waungwana,waaminifu na wastaarabu katika mahusiano yetu ya kimaisha na kimapenzi.
tafakari, chukua hatua!