Jumapili niende Mkutano gani?

Jumapili niende Mkutano gani?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Mimi ni mmiliki wa bodaboda. Lowassa anazungumza na vijana wa bodaboda Jumapili.Nataka niende kusikiliza anachowaambia na kuwaahidi.Nataka kujua sumu anayoimwaga kwa 'waajiriwa' wetu. Lowassa akiwanunulia kila mtu bodaboda yake,zetu ataendesha nani? Nataka kwenda...

Mimi ni kada mkongwe wa CCM. Jumapili kutakuwa na Maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama chetu. Ni kule Mbeya.Nataka kuwepo. Mwaka ule Mwenyekiti alitangaza 'kuvua gamba' katika sherehe kama hizi. Nataka kujua mwaka huu atatangaza 'operesheni' gani tena ya kichama.Nataka kuwepo Mbeya kusikia na kuona. Hata nauli nimeshapata. Nataka kwenda...

Mimi ni mtanzania. Nahusika na hoja za Katiba mpya na Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Maboresho ya daftari hilo ni muhimu. CHADEMA watakuwa Viwanja vya Jangwani kuzungumzia hoja hizo. Watakuwepo manguli wa hotuba uwanjani pale. Hoja nzito;watu machachari. Ningependa niwepo pale ili nisikie na kuona kitakachosemwa. Nataka kwenda...

Je,niende wapi? Njia panda!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Nenda kwa manguri wa siasa wanajua mustakabari wa nchi wanajua mipango ya kuivusha nchi salama kiuchumi wanataka kurejesha sura za furaha kwa watanzania nenda jangwani ukajissikilizie sijui chombo cha habari kitawesek ukursa wa mbele habr gani
 
Kaka VUTA NKUVUTE nenda wa Chama cha UPINZANI CDM ili ujue mbivu na mbichi waweza kurudi ukawa umeokoka ghafla.:thinking:
 
Hiyo nayo kali!!! Nenda jangwani kwani hakuna nauli ila utapata yaliyo bora kwa maisha ya Watanganyika.
 
Mkuu nenda Mbeya huko kuna hela za bure kwa wahudhuriaji sisi tuiliopo huku tutakujuza yaliyojiri jangwani
 
wewe ni mwenyeki wa mke wako na watoto wako na wala si ccm.
 
Nenda kanisani tu, siasa za bongo ni uchwara km alivyosema rostam aziz
 
Mimi nafikiri Uende Jangwani kwa Chadema kwa sababu Lowasa anaenda kuchangisha watu na hakua kitu jipya hapo.
Maadhimishi ya CCM nako hakuna jipya.

Hoja ya Katiba Mpya ni Muhimu na Kusikia Msimamo wa Chama ambacho kitashika Dola muda si Mrefu ni hoja ya Msingi sana.
 
Hahaaaa usiende mbeya umeshagundua ahadi ni hewa huko kwa lowasa hana sera ni hongo anatoa kuhadaa vijana ili yeye aingie madarakani atimize ndoto zake za kuzisaga rasilimali za Watanzania, huko kwenye mustakabali wa daftari na katiba mpya kuna nuru nenda ukaulize nafasi ya kijana,mkulima, mfugaji, mlemavu, mzee, wanawake na rasilimali zetu ziko vipi kwenye rasimu.
 
Lowasa hana lolote la kuwaambia ni kuwadanganya tu! yeye sio mwajiriwa wa serikali.
Vilevile Lowasa awe makini asije akatoa kauli za kuwachanganya watu watendaji na Mamlaka mbalimbali kwani itabidi awajibike yeye.
 
hahahahaaa hio sio njia panda nadhani maadamu ziko tatu itakua ni nia Pinda ooorr sorry ni njia Punda hahahahahaaaaaaa
 
jangwani nakumbuka ulipewa jina jipya
gani?
 
Nenda penye Maslahi ya Taifa letu la Tanzania, Duh na kweli hapo ni Njia Panda.
Kwa maelezo yako tu, Jangwani ndio jibu muafaka, kwa sababu kwa Lowassa umelalamika, Mbeya umelalamika.

Mimi ni mmiliki wa bodaboda. Lowassa anazungumza na vijana wa bodaboda Jumapili.Nataka niende kusikiliza anachowaambia na kuwaahidi.Nataka kujua sumu anayoimwaga kwa 'waajiriwa' wetu. Lowassa akiwanunulia kila mtu bodaboda yake,zetu ataendesha nani? Nataka kwenda...

Mimi ni kada mkongwe wa CCM. Jumapili kutakuwa na Maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama chetu. Ni kule Mbeya.Nataka kuwepo. Mwaka ule Mwenyekiti alitangaza 'kuvua gamba' katika sherehe kama hizi. Nataka kujua mwaka huu atatangaza 'operesheni' gani tena ya kichama.Nataka kuwepo Mbeya kusikia na kuona. Hata nauli nimeshapata. Nataka kwenda...

Mimi ni mtanzania. Nahusika na hoja za Katiba mpya na Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Maboresho ya daftari hilo ni muhimu. CHADEMA watakuwa Viwanja vya Jangwani kuzungumzia hoja hizo. Watakuwepo manguli wa hotuba uwanjani pale. Hoja nzito;watu machachari. Ningependa niwepo pale ili nisikie na kuona kitakachosemwa. Nataka kwenda...

Je,niende wapi? Njia panda!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Mimi ni mmiliki wa bodaboda. Lowassa anazungumza na vijana wa bodaboda Jumapili.Nataka niende kusikiliza anachowaambia na kuwaahidi.Nataka kujua sumu anayoimwaga kwa 'waajiriwa' wetu. Lowassa akiwanunulia kila mtu bodaboda yake,zetu ataendesha nani? Nataka kwenda...

Mimi ni kada mkongwe wa CCM. Jumapili kutakuwa na Maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama chetu. Ni kule Mbeya.Nataka kuwepo. Mwaka ule Mwenyekiti alitangaza 'kuvua gamba' katika sherehe kama hizi. Nataka kujua mwaka huu atatangaza 'operesheni' gani tena ya kichama.Nataka kuwepo Mbeya kusikia na kuona. Hata nauli nimeshapata. Nataka kwenda...

Mimi ni mtanzania. Nahusika na hoja za Katiba mpya na Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Maboresho ya daftari hilo ni muhimu. CHADEMA watakuwa Viwanja vya Jangwani kuzungumzia hoja hizo. Watakuwepo manguli wa hotuba uwanjani pale. Hoja nzito;watu machachari. Ningependa niwepo pale ili nisikie na kuona kitakachosemwa. Nataka kwenda...

Je,niende wapi? Njia panda!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Ukoo wa panya na chama chakavu!
Nenda jangwani ukamsikilize Dr.Slaa achana hao ukoo wa panya!
 
Back
Top Bottom