Jumapili niende Mkutano gani?

Jumapili niende Mkutano gani?

Mimi ni mmiliki wa bodaboda. Lowassa anazungumza na vijana wa bodaboda Jumapili.Nataka niende kusikiliza anachowaambia na kuwaahidi.Nataka kujua sumu anayoimwaga kwa 'waajiriwa' wetu. Lowassa akiwanunulia kila mtu bodaboda yake,zetu ataendesha nani? Nataka kwenda...

Mimi ni kada mkongwe wa CCM. Jumapili kutakuwa na Maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama chetu. Ni kule Mbeya.Nataka kuwepo. Mwaka ule Mwenyekiti alitangaza 'kuvua gamba' katika sherehe kama hizi. Nataka kujua mwaka huu atatangaza 'operesheni' gani tena ya kichama.Nataka kuwepo Mbeya kusikia na kuona. Hata nauli nimeshapata. Nataka kwenda...

Mimi ni mtanzania. Nahusika na hoja za Katiba mpya na Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Maboresho ya daftari hilo ni muhimu. CHADEMA watakuwa Viwanja vya Jangwani kuzungumzia hoja hizo. Watakuwepo manguli wa hotuba uwanjani pale. Hoja nzito;watu machachari. Ningependa niwepo pale ili nisikie na kuona kitakachosemwa. Nataka kwenda...

Je,niende wapi? Njia panda!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Jtatu utapima kwenye media na mtaani kwako, je gumzo litakuwa wapi jangwani ama Mbeya?

Maana maccm na watanzania wote watataka kujua CHADEMA wamesema nini kwenye uwanja wao "Chadema Square"

Pima jipime
 
NENDA JANGWANI UONE HARAKATI ZA CHAMA AMBACHO MWENYEKITI WAKO ALISEMA NI CHAMA CHA MSIMU.
Mbeya usiende maana makao makuu ya chama chako yako dasi-lama, mbeya mjini hamna hata mbunge wa chama chenu waenda umekaribishwa na mbunge mwenye jiji!sugu?
Kwa Lowasa kama uko kambi yake pia waweza kutenga dakika chache ukaenda maana una bodaboda hautakaa foleni, ivyo nenda kwa Luwasa na malizia jangwani ukapate mkate na upako maana kila Mtanzania anatamani kilichochema!
 
Mnanichanganya. Kwani Lowassa yeye hatakuwa Mbeya na chama chake? Ina maana anafanya mambo tofauti na wenzake? Naomba msaada. Au ni Lowassa kwanza chama baadaye.
 
Bila V8 usiende Mbeya Mkuu...
Ni hatar kupakiwa kwenye fuso kutoka Dar Mpaka Mbeya
 
1. Kama una shida ya mkwaja nenda kwa Lowassa
2. Kama unataka ubwabwa nenda Mbeya
3.Kama unataka kushangaa Chopa nenda Jangwani

Mkuu umenichekesha sana. Ila pia nikasikitika kuona humwamini mtu/ chama na bado tu utaongozwa na yeyote kati yao...zaidi cdm.

Dar. nani wakushangaa chopa kama zinazagaa angani wakati wote.
 
Hiyo mkuu ni VUTA. NKUVUTE ila mi. Ntaenda kwa mkuu wa anga
 
Nenda Jangwani!...kama musa alivyopitisha wana wa israel kuelekea nchi ya ahadi.Chdm inaenda kukamilisha mchakato huo.Huko kwingine ni kujilisha upepo!
 
Sasa usiumize kichwa, Mwite Mwajuma pale APPLE GUEST HOUSE, umpe haki yake, hapo ndipo kuna mustakabali wa kizazi chako!
 
Mkuu nenda mbeya upige posho , bila kusahau ukienda Jangwani kwa Manguli wa siasa utahojiwa Lumumba ilikuwaje ukakosekana Mbeya...........
 
Kwa magamba uchuro tu,nenda kwenye ukombozi huko Jangwani,ukapate maji ya ukombozi.
 
Mnanichanganya. Kwani Lowassa yeye hatakuwa Mbeya na chama chake? Ina maana anafanya mambo tofauti na wenzake? Naomba msaada. Au ni Lowassa kwanza chama baadaye.

Hapo ndipo utaona udhaifu wa magamba na chair wao. Upuuzi huo ukitokea cdm nakulipa.
 
Mimi ni mmiliki wa bodaboda. Lowassa anazungumza na vijana wa bodaboda Jumapili.Nataka niende kusikiliza anachowaambia na kuwaahidi.Nataka kujua sumu anayoimwaga kwa 'waajiriwa' wetu. Lowassa akiwanunulia kila mtu bodaboda yake,zetu ataendesha nani? Nataka kwenda...

Mimi ni kada mkongwe wa CCM. Jumapili kutakuwa na Maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama chetu. Ni kule Mbeya.Nataka kuwepo. Mwaka ule Mwenyekiti alitangaza 'kuvua gamba' katika sherehe kama hizi. Nataka kujua mwaka huu atatangaza 'operesheni' gani tena ya kichama.Nataka kuwepo Mbeya kusikia na kuona. Hata nauli nimeshapata. Nataka kwenda...

Mimi ni mtanzania. Nahusika na hoja za Katiba mpya na Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Maboresho ya daftari hilo ni muhimu. CHADEMA watakuwa Viwanja vya Jangwani kuzungumzia hoja hizo. Watakuwepo manguli wa hotuba uwanjani pale. Hoja nzito;watu machachari. Ningependa niwepo pale ili nisikie na kuona kitakachosemwa. Nataka kwenda...

Je,niende wapi? Njia panda!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Jumapili saa mbili asubuhi hadi saa nne kamili nenda kanisani pale sinza mori word alive church. Ibada ikiisha tu! Unganisha ibada yahoo pili pale Efatha Mwenge. Utakuwa umejitendea haki mwenyewe?
 
Mimi ni mmiliki wa bodaboda. Lowassa anazungumza na vijana wa bodaboda Jumapili.Nataka niende kusikiliza anachowaambia na kuwaahidi.Nataka kujua sumu anayoimwaga kwa 'waajiriwa' wetu. Lowassa akiwanunulia kila mtu bodaboda yake,zetu ataendesha nani? Nataka kwenda...

Mimi ni kada mkongwe wa CCM. Jumapili kutakuwa na Maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama chetu. Ni kule Mbeya.Nataka kuwepo. Mwaka ule Mwenyekiti alitangaza 'kuvua gamba' katika sherehe kama hizi. Nataka kujua mwaka huu atatangaza 'operesheni' gani tena ya kichama.Nataka kuwepo Mbeya kusikia na kuona. Hata nauli nimeshapata. Nataka kwenda...

Mimi ni mtanzania. Nahusika na hoja za Katiba mpya na Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Maboresho ya daftari hilo ni muhimu. CHADEMA watakuwa Viwanja vya Jangwani kuzungumzia hoja hizo. Watakuwepo manguli wa hotuba uwanjani pale. Hoja nzito;watu machachari. Ningependa niwepo pale ili nisikie na kuona kitakachosemwa. Nataka kwenda...

Je,niende wapi? Njia panda!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Acha njaa zako wewe. Wewe ni mwana siasa au unavizia buku 7, pilau na pombe za kienyeji?

Ingia cdm acha tamaa kamanda. Utajiri usiutake mapema kivile.
 
Umesahau pia,kuna mechi ya yanga ccm na mbeya cc..chadema wamesogeza mbele wa kwao,kumtega lowasa
 
Mimi ni mmiliki wa bodaboda. Lowassa anazungumza na vijana wa bodaboda Jumapili.Nataka niende kusikiliza anachowaambia na kuwaahidi.Nataka kujua sumu anayoimwaga kwa 'waajiriwa' wetu. Lowassa akiwanunulia kila mtu bodaboda yake,zetu ataendesha nani? Nataka kwenda...

Mimi ni kada mkongwe wa CCM. Jumapili kutakuwa na Maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama chetu. Ni kule Mbeya.Nataka kuwepo. Mwaka ule Mwenyekiti alitangaza 'kuvua gamba' katika sherehe kama hizi. Nataka kujua mwaka huu atatangaza 'operesheni' gani tena ya kichama.Nataka kuwepo Mbeya kusikia na kuona. Hata nauli nimeshapata. Nataka kwenda...

Mimi ni mtanzania. Nahusika na hoja za Katiba mpya na Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Maboresho ya daftari hilo ni muhimu. CHADEMA watakuwa Viwanja vya Jangwani kuzungumzia hoja hizo. Watakuwepo manguli wa hotuba uwanjani pale. Hoja nzito;watu machachari. Ningependa niwepo pale ili nisikie na kuona kitakachosemwa. Nataka kwenda...

Je,niende wapi? Njia panda!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

kwanza miliki uchumi-bodaboda na mambo mengine baadae
 
Mzee TupaTupa tupa kule kila kitu uende kanisani Jumapili
 
Back
Top Bottom