Jumanne saa Nne na Nusu Tegeta kibaoni

Jumanne saa Nne na Nusu Tegeta kibaoni

Darz

Member
Joined
Sep 24, 2016
Posts
11
Reaction score
2
Daah... Nimeamini watu wakisema ukiona mwenzako ananyolewa we jiandae zamu yako na hii ilinikuta wakati narejea nyumbani kutoka kazi.

Ilikuwa mida ya saa tatu hivi usiku nilikuwa nimechoka vibaya sana baada ya hapa kazi tu siku nzima nimetokea maeneo ya k/koo narejea nyumbani nikaingia zangu katika dara dara kuelekea home nilipofika mwenge niliamua kupanda gari la kuelekea tegeta na wakati huo magari yalikuwa hamna kabisa nikaamua kupanda Noah kwa Elfu moja iliniweze fika nyumbani mapema..lakini yote Mungu tu ndiyo ajuaye mbele yangu nikiwa na Ka Smartphone kangu kazuri niliipenda vibaya sana ilinisaidi kupata News tofauti tofauti kutoka Youtube, Jamiiforum n.k na wakati wote ilikuwa nikiniweka busy na kunitoa stress za hapa na pale ...

Wakati Noah inaelekea na safari nilikuwa nimeketi siti ya nyumbani nikiperuzi thread za Jf na kutabasamu peke yangu glafla na dakika zili yoyoma bin vuuu tukafika tegeta kwa ndevu abiri kadhaa walishuka tukabaki watu wawili mi nikawaambia dereva nashukia tegeta kibaoni ambapo ndo mwisho wa safari yangu na tulipofika nilijikwatu kwenye siti Mdogo mdogo kushuka nje ya Noah na nilijaribu kutembea hatua chache tu ili nipande boda boda wakati naelekea kuchukua boda boda glafla jamaa mmoja na boda boda yake ametoka huko kwa fujo kanakwamba alikuwa anaelekea kunigonga glafla nikajikuta nimeduaah na kutamani kupaa ili nimrukie...

Daah kichozi chembamba kilinitoka na cha hasira yule mtu wa boda boda alisha kwapua hile simu niipendayo niliwaza mengi lakini mwisho wa siku nikashukuru mungu lakini nimejifunza..
 
Back
Top Bottom